#COVID19 Sayansi inazidi kutokomeza Corona

#COVID19 Sayansi inazidi kutokomeza Corona

Maambukizi ya awamu ya kwanza yaliondojaje vile,??
We unaonekana hujui kuhusu virusi kabisa. Hivi Mungu anaweza kuwa na majibu yanayoexpire kweli yani kipindi kile atusaidie leo atuache duu. Ukifuata sayansi utajua kwann sahiv tumepigwa kuliko mara ya kwanza achana na imani Mfu.
 
Jifunze kutoka kwa aliyefanikiwa. Dunia siyo Africa pekee. Tungedhamiria tungeweza. Kwanza tulipewa msaada wa zaidi ya bilioni 100 ili kupambana na corona, tungeweza kuitumia hela hii kuwapima watu wetu. Bahati mbaya, tukaitapanya na kupeleka kungine.
Wewe unajua hiyo hela imetolewa kwa ajili ya nini ? Maana madhara ya corona yana mambo mengi

Pili Hiyo 100m unayosemea na kutumika kupima, watu wake , je hao USA and the like kuna Nchi ime achieve hiyo 100% ya watu kupimwa hiyo corona zaidi ya hiyo Israel?? Au ndio kwamba una nafasi ya kuandika basi unaandika.

Unatakiwa kufanya jambo au mambo kufuatana na uwezo wako, sio kufuata fulani kafanya nini, kuiga iga mwishowe utapasuka msamba
 
Umenikumbusha kauli ya Baba Askofu Bagonza, “Tulipokuwa tuna Chuo Kikuu kimoja UDSM hatukuwa na wajinga wengi lakini sasa tuna vyuo vikuu vingi idadi ya wajinga nchini imeongezeka sana.”
Zaidi ni umskini wa kichwani kuliko fedha.
 
Kwenye tafiti za madawa sisi bado sana..
Ndomana utakuta mijitu inalala ikiamka wanakuambia nimeoteshwa dawa...

Wengine ndiyo wale wanakuambia saga pilipili,
Saga tangawiz changanya na limao weka kitungu na karoti weka mwarobaini ongezea ndani majivu hiyoo ni dawa...gadamnnnn

Ova
 
Mkuu ubarikiwe sana kwa kujali waTZ wenzako!! Taarifa yako inatia faraja na matumaini ,Tatizo JIWE anatoa kafara 3% ya wazee + 2% ya wenye VVU.
 
Waisrael wamekufa 5526.
tangu mwaka Jana .
He Tanzania wanafika waliokufa na Corona hyo idadi?.
KWA MUNGU TUNATEGEMEA.na tutashinda.
Mganga MUNGU tu
 
Mungu siyo Lisu wala Amsterdam
Kwa wenzetu Wakristo dunia nzimà, Mungu ni wa Waisrael aliowateua yeye mwenyewe hata Mwanae Mpendwa alizaliwa huko, hao wengine ni miungu tu ikiwa ni pamoja na wa Waitalia, wa Wachina, wa Wasukuma nk. Mungu wa Watanzania anayewalinda wao tu hayupo Mbinguni wala duniani!
 
Waisrael wamekufa 5526.
tangu mwaka Jana .
He Tanzania wanafika waliokufa na Corona hyo idadi?.
KWA MUNGU TUNATEGEMEA.na tutashinda.
Mganga MUNGU tu

Kama takwimu za wagonjwa wa Covd 19 Hamna... Hiyo takwimu ya vifo vya wagonjwa wa Covd 19 utapata wapi?

Acha ujinga
 
Covid 19 haikuiacha Israel, walipata maambukizi, na wapo waliokufa. Mpaka leo idadi ya walioambukizwa ni 744,513, waliokwishafariki ni 5,526, waliokwishapona ni 693,730, ambao bado wana virusi 45,257, na kati ya hao wenye virusi, ni 872 tu ndio wanaumwa hasa.

Hii ina maana kati ya wote waliopata maambukizi ni 0.7% ndio waliofariki. Wastani wa Dunia ni kwamba katika wote wanaoambukizwa corona, 3.5% hufariki.

MAMBO YA TAKWIMU HAYA
 
Tz kuna ignorance wengi cha kuustaabisha hata professional wa matibabu wamekuwa foolish

Wanasayansi pamoja na kusoma na kuwa wataalam wa afya lkn bado wanaburuzwa na wanasiasa... Wapo kimya Kama hawapo.

Awamu hii watu wamezidi kuwa na uoga, hofu na wasiwasi... Huku Ni kujikaza kisabuni huku tukiisha mdogo mdogo...
 
kwani takwimu za wagonjwa wa magonjwa mengine unazo?.
au unadhani wanakufa kwa Corona Tu?.
Kama takwimu za wagonjwa wa Covd 19 Hamna... Hiyo takwimu ya vifo vya wagonjwa wa Covd 19 utapata wapi?

Acha ujinga
 
Tz kuna ignorance wengi cha kuustaabisha hata professional wa matibabu wamekuwa foolish
Tz hakuna madaktari wa tiba wala wanasayansi,tunao wafungia vidonda na wapima kinyesi ndiyo wanajiita madaktari.Laiti kama tungekuwa na wataalamu wa tiba kweli tungeshapatiwa maelekezo mengi ya kitaalamu bila uoga kutoka kwa wanasiasa.
 
... ndio maana wapo waliokuwa wanahoji andiko (thesis) la kisayansi la huyu BWANA linapaticana wapi? Andiko la kutunukiwa PhD halijawahi andikwa bila utafiti wa kisayansi. Madai yale ya kuoneshwa andiko hata kama hayajawahi kutekelezwa yalikuwa na bado yana maana nzito sana.
Ukishskuwa rais wa Tz andiko lako linafichwa.
 
Science itashinda kwa sababu ilishashinda kwa data. watu wengi wanadhani kuamini science ni ukafiri au kutoamini Mungu hapana. Mungu ndio katupa hii elimu na iko katika vitabu vya dini, Mungu katupa maarifa tuyatumie kwa faida yetu. ndio maana baada ya mengi mengi kugunduliwa kama madawa, chanjo na elimu katika utabibu life expectancy katika karne 2 imetoka kutoka 39 Years to 72 years kwa maana leo watu wanaishi mara 2 kuliko ilivyokuwa miaka hiyo.

Na ukienda kwenye chanjo za watoto miaka ya nyuma kidogo watoto walikuwa wanafariki kwa matumbo tu ya kuharisha leo hii hakuna baada ya chanjo. miaka ya sabini watoto na watu wazima walikuwa wanakufa kwa magonjwa ambayo leo yamethibitiwa kwa chanjo.

Science ni zawadi ya Mungu kwa binadamu sio kinyume chake, leo hii watu wanasoma sana vitabu vingi elimu inawafikia watu haraka. ukisoma History hata wafalme wengi walikuwa wanafariki katika 40s na hawa walikuwa na best Dr's sasa watu wa kawaida? leo mpaka 90 wako tu
 
Mimi naungana na wewe,mwaka jana Magufuli kalaumiwa sana mara anaficha corona sijui watu wakufa kimya kimya mara sijui kaamua kuwatoa wananchi wake kafara ila mwishoni wote tukafanya nao kampeni bila tahadhari zozote na sasa wanasema corona ilipungua mwaka jana.
Ilipungua dunia nzima lakini Tanzania pia ilichukuwa hatua kama kufunga shule na kampeni za mask na kunawa mikono lakini tulionywa itakuja second wave badala ya kujiandaa na second wave tukaanza kiburi, ingekuwa hawakujuwa kuwa wave ya kwanza itapungua wasingesema kuna second wave haiwezi kuja ya pili bila kuisha ya kwanza haya mambo yalitabiriwa na wataalamu sasa hata second wave tungewahi kuchukuwa tahadhari na sisemi lockdown tungefanya kama mwanzo tu ingepunguza kiasi.

Wenzetu wakawa busy kutafuta chanjo sababu wanajuwa huu sio mwisho sisi tukasema corona imekimbia Mungu anatupenda hatukujiandaa na second wave ndio unayoona leo haya tumekana mpaka tumeanza kuelewa.
 
Umezunguka,maneno meengi lakini target yako ni Magufuli,we want to win differently mkuu,God is with us don't panic.
 
Hiyo Jewish protocol ungeiweka hapa ili uwe umetoa mchango wako lakini as usual kila mtu analalamika.
 
Back
Top Bottom