Eiyer.
Nimependa mada yako kwani inahitaji uchambuzi wa kina kuhusu sayansi na uchawi.
Kweli hata mimi natamani sana kujua ni kwanini wanasayansi hawana ushahidi juu ya uchawi na hawataki kuuzungumzia ktk tafiti zao.
Nimekuwa nikifanya tafiti juu ya sayansi na uchawi na ninavyofikiria ni kuwa wanasayansi wanatambua uwepo wa natural force ambazo zipo ktk dunia. Kuna nyingine zinaweza kuthibitishwa na nyingine haziwezi kuthibitishwa kama uchawi. Niliwahi kupewa kitabu na mtu mmoja cha FORBIDEN KNOWLEDGE kwa sasa sinacho kiliibwa.
Kitabu hicho kilikuwa kinahusu mambo ya anga na maajabu yake ambayo hayawezi kufikirika kama yapo. Pia kilikuwa kinachambua na baadhi ya spell ambazo unaweza kuzitamka pindi unapokutana na maajabu hayo ili yasikudhuru na wala kusitokee ajali yoyote hasa kwa wale wanaosafiri kwa ndege au wanaokwenda anga za mbali.
Wanasayansi wanajua ukweli ila hawataki kuzungumzia hayo mambo kwa purpose zao(THE RULERS)