Sayansi na uchawi !

Sayansi na uchawi !

Inapotokea mtu ambaye haujui ugonjwa wa malaria ukoje na hapohapo anadai kuwa hakuna huo ugonjwa. Basi itakuwa ni vigumu kumthibitishia kuwepo kwa ugonjwa wa malaria hali ya kuwa hajui hata malaria ikoje.

Na ndiyo kitu kinachotokea hapa kwamba mtu hajui uchawi ni nini na anadai kuwa hakuna huo uchawi.
 
ebo! nimesema hakuna uchawi labda nikiuona ndo ntakubali uchawi upo, shida iko wapi hapo? niami tu kuwa uchawi upo kwa vile wewe umesema?

Kwanza umejuaje kama unaonekana?

Sio kila kilichopo unapaswa ukione ndipo ukubali uwepo wake ...

Lakini ni kitu gani kimekufanya useme hakuna uchawi?

Kwa mujibu wa hayo maelezo yako hapo juu ni kwamba huna uhakika kama upo au haupo,hii inamaana kuwa unabahatisha,kwanini unahitimisha wakati huna uhakika?
 
Hakuna mtu anaetibiwa kwa uchawi ukasema shetani hawezi mpinga shetani mwenzie.Mtu aliyerogwa hutibiwa kishilikina ila ni mpaka ujue nguvu iliyotumika kumfanyia huyo mtu ndio inapokuja lamri ili mganga ajue nini kimemsibu Mgonjwa baada ya hapo tiba inaanza.Na ndio mana kuna watu wamekufa kwa kulogwa na inapojulikana kuwa huyu mtu amekufa kwa uchawi kuna uwezo wa kumfanya aludi duniani kwa roho nyingine na kulipa kisasi kwa waliomfanyia kile kitendo ila ni mpaka ndugu mkubaliane ktk hilo.kuna siku nitakuja kulieleza kwa ufupi ili mjue kuwa uchawi upon.
Kwenye dunia yako hakuna herufi R?
 
Eiyer story yako ya majonzi ila mwisho kuzuri

hya mambo ya uchawi ni shida tunayasikia ila ........

kikbwa ni kumtegemea MUNGU PEKEE atatenda miujiza yake ...
 
Last edited by a moderator:
Ishu apa ni kwamba baada ya wazungu kuiona African technology ni kubwa zaidi ya yakwao wakaamua kuiita dark na kukandamiza kwamba ni mila potofu ili tu base kwenye za kwao. Ila hii technology ni kubwa na ya uhakika mnoooo. Ova
 
Eiyer.

Nimependa mada yako kwani inahitaji uchambuzi wa kina kuhusu sayansi na uchawi.

Kweli hata mimi natamani sana kujua ni kwanini wanasayansi hawana ushahidi juu ya uchawi na hawataki kuuzungumzia ktk tafiti zao.

Nimekuwa nikifanya tafiti juu ya sayansi na uchawi na ninavyofikiria ni kuwa wanasayansi wanatambua uwepo wa natural force ambazo zipo ktk dunia. Kuna nyingine zinaweza kuthibitishwa na nyingine haziwezi kuthibitishwa kama uchawi. Niliwahi kupewa kitabu na mtu mmoja cha FORBIDEN KNOWLEDGE kwa sasa sinacho kiliibwa.

Kitabu hicho kilikuwa kinahusu mambo ya anga na maajabu yake ambayo hayawezi kufikirika kama yapo. Pia kilikuwa kinachambua na baadhi ya spell ambazo unaweza kuzitamka pindi unapokutana na maajabu hayo ili yasikudhuru na wala kusitokee ajali yoyote hasa kwa wale wanaosafiri kwa ndege au wanaokwenda anga za mbali.

Wanasayansi wanajua ukweli ila hawataki kuzungumzia hayo mambo kwa purpose zao(THE RULERS)
 
Jamani anayejua mganga Wa ukweli mwanza na siyo tapeli kuna shangazi anatanganga mwaka Wa tatu sasa tumeshamuombea mpaka dar Kwa manabii hakuna kitu ameshindwa kufanya kazi Kwa kuumwa akiombewa mapepo yanasema alitupiwa kutoka Zanzibar akiwa anafata mzigo Wa biashara, nahitaji mtaalam Wa kweli maana ndo mzazi naye mtegemea pekee.
 
Eiyer.

Nimependa mada yako kwani inahitaji uchambuzi wa kina kuhusu sayansi na uchawi.

Kweli hata mimi natamani sana kujua ni kwanini wanasayansi hawana ushahidi juu ya uchawi na hawataki kuuzungumzia ktk tafiti zao.

Nimekuwa nikifanya tafiti juu ya sayansi na uchawi na ninavyofikiria ni kuwa wanasayansi wanatambua uwepo wa natural force ambazo zipo ktk dunia. Kuna nyingine zinaweza kuthibitishwa na nyingine haziwezi kuthibitishwa kama uchawi. Niliwahi kupewa kitabu na mtu mmoja cha FORBIDEN KNOWLEDGE kwa sasa sinacho kiliibwa.

Kitabu hicho kilikuwa kinahusu mambo ya anga na maajabu yake ambayo hayawezi kufikirika kama yapo. Pia kilikuwa kinachambua na baadhi ya spell ambazo unaweza kuzitamka pindi unapokutana na maajabu hayo ili yasikudhuru na wala kusitokee ajali yoyote hasa kwa wale wanaosafiri kwa ndege au wanaokwenda anga za mbali.

Wanasayansi wanajua ukweli ila hawataki kuzungumzia hayo mambo kwa purpose zao(THE RULERS)

Ninachoamini hadi sasa ni kwamba hawa watu wanajua na hawasemi kwasababu zao wenyewe!
 
Pengine, ukitaka kujua uchawi, ni lazima kwanza uweze kujua au kuelewa "mazingaombwe". Nimesikia mara kadhaa wanaofanya mazingaombwe wakisisitiza kuwa kile wanachokifanya sio uchawi. Kwa hivyo ni lazima kwanza kuelewa mazingaombwe yanaanzia wapi ma kuishia wapi.

Wakati mwingine vitu tunavyoita uchawi/mazingaombwe ni "sayansi" isipokuwa tu hatuielewi au wanaoijua hawataki kuielezea ikaeleweka. Kwa uelewa wangu mdogo sana kuhusu mazingaombwe, nimekuwa nikiamini kuwa uchawi ni lazima uambatane na mazingaombwe (mchawi ni lazima ajue kufanya mazingaombwe).

naangalia vitu vya David Copperfield akipaa (flying!):

[video]https://m.youtube.com/watch?v=70U2yybKhKg[/video]
 
Ninachokiamini hata hao wazungu wanaamini Uchawi...Angalia katika matukio yao mengi mengi tuu yapo yanayoashiria kuwa wanaamini ila tuu hawataki kusema kuwa wanaamini...Labda tuseme Sayansi ndio uchawi wenyewe...hapo sitabisha....Ila kama ni uchawi wanao....Mfano mambo ya nyota...wao wanayaamini sana haya...yote hii ni mambo ambayo hakuna dini inaruhusu kwa kusemekana ni ushirikina (uchawi)...., Mfano tamthilia zao mbona hayo mambo yapo tuu wanayaonyesha? kama ile tamthilia ya kale kabibi Tabitha kachawi (siikumbuki jina)....Kina harry potter etc..
Wajerumani nao ndio wanaamini hasa...
Sema tuu sisi tumekuwa tukiutumia uchawi kuwaharibu wenzetu, kutaka wenzetu wasiendelee ila si kimaendeleo yetu wenyewe.
 
Back
Top Bottom