SBF hajapoteza utajiri wa USD 16 billion bali walomwamini ndo wamepoteza na yeye ame-gain, Hana tofauti na Ivar Kreuger "The Match King" wa 1920s

SBF hajapoteza utajiri wa USD 16 billion bali walomwamini ndo wamepoteza na yeye ame-gain, Hana tofauti na Ivar Kreuger "The Match King" wa 1920s

kali linux

JF-Expert Member
Joined
May 21, 2017
Posts
2,192
Reaction score
5,685
Hello bosses...

Kipindi cha nyuma TerraUSD na Luna zilipopata anguko niliandika uzi humu kwa sababu hilo tukio nlikua nategemea lije kutokea kutokana na mechanics za namna hizo coins zilivokua zinafanya kazi uzi uko hapa CRYPTO-FUNZO KWA WAKURUPUKAJI: Luna coin ilikua ni sawa na $85 wiki ilopita lkn kwa sasa ni takataka(trash coin)

Lakini hili la FTX na FTT kiukweli nilikua sijategemea kama lingetokea. Bila tamaa na uhuni wa Samuel Bankman-Fried anaejulikana kama SBF hili tukio lisingetokea. Luna na TerraUSD zilifail kwa sababu ya technical problems na namna algos zao zilivokua zinafanya kazi ila hii issue ya SBF ni kwa sababu ya tamaa na uhuni. Hata kama CZ angeuza zile tokens isinge-affect sana kama FTX wangekua na management nzuri ya funds.

Kiufupi kabisa wanaodhani SBF kapoteza fedha basi wamedanganyika. Huyu jamaa alikua anatumia fedha za wateja wake kufanya manunuzi binafsi na kucover losses kwenye biashara zake nyingine. Hawa ni watu wanaochezea Balance Sheets za makampuni yao ili kuonesha utajiri usiokuwepo kiuhalisia na kuficha matumizi mabaya ya fedha za wateja wao. Na kizuri cha kuchezea balance sheets ni kwamba huwezi ficha madudu hayo milele, kuna siku tu yatajionesha, mfano mzuri ni kama case ya ENRON au huyu jamaa Ivar Kreuger ambae alijizolea jina la "Match King" kwa sababu ya kumiliki zaidi ya robo tatu ya viwanda vilivokua vinatengeneza viberiti "matches" kwenye miaka ya 1920s. Ivar Kreuger alicheza michezo hatari sana kwenye finance iliofanana kwa kiasi fln na hii hii aliocheza SBF. Tofauti tu ni kwamba Ivar alijiuwa baada ya madudu yake kuonekana. Story kuhusu huyu mwamba ntaandika siku nyingine nikipata muda.

Inasemekana wazazi wa SBF wanamiliki majumba ya kifahari huko Bahamas na mali nyingine ghali ambazo kwa kazi zao na vyanzo vyao vya fedha ni ngumu sana (kama sio impossible) kumiliki. Wazazi wake ni lecturers wa Stanford lakini majumba wanayomiliki ni juu zaidi ya makadirio ya utajiri wao. Inasemekana SBF aliingiza fedha kwenye manunuzi ya hizo mali. Bado hatujui huyu jamaa fedha nyingine kaweka wapi lkn inaonekana kwa asilimia kubwa alikua ana-reallocate hizo fedha kwa njia mbalimbali huku akiwaachia numbers tu wateja wake na ulimwengu ulokua unamfuatilia. Pia inasemekana jamaa alikua anatumia fedha za wateja wake kufanya trading na kucover hasara kwenye biashara zake nyingine.

Huwezi sema huyo mtu wa aina hio kapoteza coz yeye amesha spend hio hela kwa mambo yake, na kaficha hivo hadi ulimwengu ulipokuja kugundua. Waliopoteza ni watu walomwamini na kuinvest kwake. Utafiti unaendelea na kila baada ya siku mbili au moja kuna habari mpya kuhusu huyu jamaa. Upelelezi unaoendelea unaweza onesha huyu jamaa kaficha wapi hizo fedha nyingine, japo kwa juujuu inatengenezwa picha ionekane kweli SBF kapoteza lkn ntakua mtu wa mwisho kuamini hilo.


Happy trading....
~ kali linux
 
Mambo ya sarafu mtandao ni magumu sana kwangu yaan kila nikitaka kujifunza nielewe bado , ila naendelea kujifunza ! Huwa nasoma mtandaoni kwamba hizi pesa huwa ni mali yako binafsi ni tofauti na mfumo bank kwamba wala hakuna mtu anayeweza kuwa na access hizo pesa wala kucontrol account yako isipokua wewe tu !! Sasa huyu bwana mkubwa anawezaje kuingia akachukua hizo pesa na akawaachia namba tu wadau ?
 
Sasa huyu bwana mkubwa anawezaje kuingia akachukua hizo pesa na akawaachia namba tu wadau ?
Iko hv. FTX ni crypto exchange. Ni sehemu mtu anaweza badili au kununua hizo cryptos. Sasa baadhi ya watu hufanya deposit na kuacha coins zao humo, na hao ndio waliopata shida na hata baada ya FTX kuwa bankrupt walisitisha kufanya withdrawals coz hawakuwa na fedha ya kuwapa hao wanaowithdraw.

Ni kama wewe uwe unatunza hela zako MPESA au bank. Unawapa access hao jamaa watumie hela zako ila kuna protocol zinazoguide kutumia fedha ya mteja wako kwenye mazingira hayo. Sasa FTX hakua anafuata hizo protocols.

Kama unataka kuinvest kwenye crypto safely unaweza ziweka kwenye "Cold Storage" huko mtu hawezi kukugusa.
 
Back
Top Bottom