Damaso
JF-Expert Member
- Jul 18, 2018
- 6,236
- 10,774
Jana Jumanne bhana nikaamka na dhamira moja—kutafuta ukweli kuhusu ufadhili wa MEXT wa Japan. Nilikuwa na ndoto ya kuwasaidia vijana wangu wanne kufungua milango ya elimu ya kimataifa. Safari yangu iliniongoza hadi barabara ya Ali Hassan Mwinyi, Dar es Salaam, nikiwa na matumaini makubwa, ni huku ndipo yalipo makazi ya Balozi wa Japani nchini Tanzania.
Nilipofika getini, nilipokelewa kwa upole na mlinzi aliyekuwa tayari kunisaidia. Lakini hali ilibadilika ghafla ndani ya dakika kama tano baada ya kamama kamoja kuibuka na kumkemea mlinzi kwa ukali. Nilipoingia ndani, badala ya kupata mwongozo, nilikutana na maneno yaliyovunja moyo—kwamba hakuna haja ya kwenda Japan, na elimu ya hapa inatosha. Zaidi ya hayo, niliambiwa deadline tayari imepita. Kwamba deadline ni mwezi Machi wakati tangazo limetoka Aprili, MAAJABU HAYA.
Nilitoka nje nikiwa na maswali mengi kuliko majibu. Je, taarifa hizi ni sahihi au ni kizingiti kisichoonekana kwa vijana wenye ndoto? Nje, nilikutana na kijana Mjapani aliyeshangaa kwa nini Waafrika wachache huomba ufadhili huo. Nilimjibu kwa huzuni—KWA AFRIKA, WATU NI CONNECTIONNA CONNECTION NI WATU.
Nilitoka mule ndani nimechukia ile mbaya, Waafrika tunapeana wakati mgumu wenyewe, hapo hela za Ufadhili sio zao ila unakuwa kipele hivyo, je ukiweka jero kwenye hizo pesa itakuwaje?