Science ina support uwepo wa Mungu

Kwa uelewa wangu "halisia" humaanisha kitu au jambo ambalo ni la kweli, lililopo, au linalojulikana kuwa halisi, tofauti na kitu cha kufikirika au cha kubuni.
Unapotoa maana ya halisi, usirudie kutaja tena halisi, hilo ndilo neno linalokuwa defined.

Mpaka hapo ushafeli.
 
Gravity umeichunguza kwa miaka mingapi ukagundua haibadiliki?

Umehakikishaje kuwa sheria ya gravity haibadiliki?

Umeipima kwa kipimo gani na kupata matokeo kwa unit gani isiyobadilika kuhakikisha gravity haibadiliki?
Sheria ya uvutano wa Newton na nadharia ya uhusiano wa Einstein zimethibitishwa mara kwa mara kupitia uchunguzi wa kimajaribio na wa asili kwa karne nyingi. Kwa mfano:

Hakuna ushahidi wowote wa kisayansi unaothibitisha kuwa sheria ya uvutano imewahi kubadilika katika historia yote inayoweza kupimika ya ulimwengu,kama upo ushahidi Ulete hapa.

Uchunguzi wa vyanzo vya mwanga wa nyota, mienendo ya sayari, na mionzi ya mabaki ya mlipuko wa Big Bang (cosmic microwave background radiation) unaonyesha uthabiti wa sheria hii kwa mabilioni ya miaka.

Teknolojia za kisasa kama vile satelaiti na vipimo vya upinzani wa atomi (atomic clocks) zimethibitisha uvutano kwa usahihi wa hali ya juu. Sheria hizo zimeendelea kudumu bila mabadiliko.

Sheria za asili, kama sheria ya uvutano, hazitegemei muda wa uchunguzi wa binadamu. Badala yake:

Sheria hizi Zimeundwa Kutokana na Tabia za Ulimwengu Wetu: Gravity haijabadilika kwa mabilioni ya miaka, na hii inaonyeshwa na mienendo ya sayari na galaksi kwa historia yote ya ulimwengu. Ikiwa ingekuwa inabadilika, tungeona athari kubwa kama sayari kuondoka kwenye njia zao au kuharibika kwa miundo ya ulimwengu.

Ni muhimu uelewe kuwa nadharia za kisayansi (kama nadharia ya Einstein kuhusu uvutano) zinaweza kusasishwa, lakini sheria za asili zenyewe (mfano, uvutano unaokuwepo) hazibadiliki. Sheria hizi ni za msingi kwa kuwepo kwa ulimwengu kama tunavyoujua.


Sheria ya uvutano haijathibitishwa kubadilika kupitia majaribio ya kihistoria na ya sasa, lakini hii haimaanishi kuwa 100% hatuwezi kufikiria mabadiliko. Kinachothibitishwa ni kuwa kadri tunavyojua, uvutano umebaki thabiti kwa mabilioni ya miaka kutokana na data nyingi za kisayansi.

Swali jingine
 
Kwa uelewa wangu "halisia" humaanisha kitu au jambo ambalo ni la kweli, lililopo, au linalojulikana kuwa halisi, tofauti na kitu cha kufikirika au cha kubuni.
Kwa maana hiyo ukisema Mungu yupo ila si halisia unakua umekubali kuwa dhana ya Mungu sio ya kweli. Si ndio?
 
Kwa maana hiyo ukisema Mungu yupo ila si halisia unakua umekubali kuwa dhana ya Mungu sio ya kweli. Si ndio?
Soma vizuri nilichosema ,wewe umekata kakipande

Mungu, kama anavyofasiriwa katika falsafa na dini nyingi, ni kiumbe asiye wa kimwili (immaterial), asiye na mipaka ya nafasi (spaceless) au wakati (timeless). Kwa hivyo, hatuwezi kusema Mungu si halisia kwa sababu hafanyi kazi kama vitu vya kimwili.

Halisia haimaanishi lazima kitu kionekane au kishikwe; kwa mfano, hisabati, maadili, au nadharia za kisayansi kama gravity ni halisia hata kama si za kimwili.

Kwa hiyo, dhana ya Mungu inaweza kuwa halisia hata kama haifuati vigezo vya uhalisia wa kimwili.
 
Unaposema sheria ya uvutano haibadiliki unakusudia kumaanisha nini?

Umeipima kwa accuracy gani kujua haibadiliki?

Unajuaje kuwa haibadiliki na kwamba si kweli kwamba inabadilika ila kwa kiwango kidogo sana ambacho hatujaweza kukitambua kwa vipimo vyetu vya sasa tu na labda katika miaka billion 100 na maendeleo makubwa ya sayansi mabadiliko haya yataweza kuonekana vizuri?
 
Hakuna Maandiko yanayosema MUNGU anaundwa na sehemu 3
Kwa mtiririko huo, nahitimisha kwa kusema, science inasupport uwepo wa Mungu kwa 100%.
Hapo ndo umethibitisha 🤣🤣🤣

Ok maana wanasema Mj*** Mpe cheo tuseme kweli Kuna andiko (Japo hakuna) linalosema Mungu kaundwa na Sehemu tatu...

Sijaelewa Point yako...

Yaani Ni sawa na Kusema kwakuwa Kiongozi wa Ulaya Ni Malkia na Kwakuwa Tanzania Wanaongozwa na Mwanamke basi Tanzania Ni ulaya..

Really Hiyo nd Factual Comparison??
Kama intelluctual kabisa uliyesoma????

Kwakweli kama umesoma Basi ulienda Kupoteza Elimu badala ya Kuongeza
 
Nimekujibu labda useme una majibu mengine
Hapana.

Ulichojibu kuhusu anthropic principle ni sawa na mtu aliyepata bahati nasibu ya one in a billion. Kwa kuwa yeye ndiye kapata bahati hiyo, na ni kitu cha nadra sana, anasema lazima kuna mtu alimkusudia yeye apate bahati hiyo.

Wakati ukweli kwamba the odds of one in a billion do not mean a zero chance.

Why is this so hatd to see?
 
Mpaka sasa hakuna aliyethibitisha Mungu yupo.

Ukiwaambia watu wathibitishe Mungu yupo wanaleta longolongo nyingi ambazo nazo hazijathibitishwa pia.
 
Mkuu ndio umeamua kutumia chatgpt kutujibu, chatgpt wame icommand ikubali uwepo wa mungu ili kuondoa sintofahamu kwenye jamii.
 

Ninaposema sheria ya uvutano haibadiliki, namaanisha kwamba mpaka sasa, vipimo vyote na majaribio yameonyesha kuwa uvutano (gravity) unafuata muundo fulani uliotabirika, unaoelezewa vizuri na mifumo ya kihisabati kama vile:

Sheria ya Newton ya Uvutano wa Wote (Newton's Law of Universal Gravitation), inayoeleza mvuto kati ya miili miwili kutokana na misa yao na umbali kati yao.

Nadharia ya Einstein ya Uhusiano wa Jumla (General Relativity), ambayo inaonyesha uvutano kama athari ya miili mikubwa kwenye ugani wa nafasi na wakati.


Kwa hivyo, "haibadiliki" haimaanishi kwamba haina nyongeza za uelewa au maboresho, bali inaonyesha uthabiti wa matokeo yetu ya majaribio ndani ya mipaka tuliyo nayo sasa.

Hatujui kwa uhakika wa 100% kwamba uvutano hauwezi kubadilika, lakini kuna sababu kadhaa zinazoimarisha hoja ya uthabiti wa sheria hii,

Sheria ya uvutano imepimwa kwa kiwango cha juu sana cha usahihi kwa zaidi ya karne tatu. Imethibitishwa kuwa inafanya kazi:

Mvutano wa dunia, mabomu hurushwa kwa mwelekeo maalum, na ndege zinadhibitiwa kwa kufuata sheria hizi.

Nje ya Dunia Sheria za uvutano zinatabiri vizuri mienendo ya sayari, mwezi, nyota, na hata matukio ya anga kama mikwaruzo ya nyota (black holes).

Sheria za asili (kama uvutano) zimeonyesha kuwa ni za kimfumo, yaani, haziathiriki na wakati au mahali.

Mfano nakupa Sheria za Relativity za Einstein zimetabiri matukio mengi, kama vile kuenea kwa mawimbi ya uvutano (gravitational waves), ambayo yameonekana baadaye.

Mpaka sasa, hakuna ushahidi wa kubadilika kwa uvutano. Kama uvutano ungebadilika hata kidogo, tungeona athari kubwa kwenye mfumo wa nyota, sayari, na mahesabu ya anga.

Hatuwezi kukataa kabisa uwezekano wa kwamba uvutano unaweza kubadilika kwa kiwango kidogo au kwa muda mrefu sana, lakini:

Kiwango cha Mabadiliko Ikiwa uvutano hubadilika, kiwango chake ni kidogo mno hadi kufikia kuwa hakionekani katika vipimo vya sasa. Mabadiliko yoyote yangeathiri matukio makubwa kama mwendo wa sayari au mienendo ya nyota, lakini hatujaona dalili zozote.

Sayansi inajenga maarifa kila mara. Ikiwa miaka bilioni 100 baadaye tutaweza kupima mabadiliko ya uvutano, basi hiyo itakuwa hatua mpya ya maarifa. Lakini kwa sasa, msingi wetu wa uelewa upo sahihi ndani ya mipaka yetu.

Ikiwa sheria inabadilika kwa muda, basi ni sheria yenyewe inayokuwa si thabiti au inawezekana kuwa hatujafikia kiwango cha uelewa wa kugundua mambo kama hayo.


Kwa sasa, ushahidi wote unaonyesha kuwa uvutano haufanyi kazi kwa njia tofauti mahali popote au wakati wowote. Ikiwa hali itabadilika katika siku zijazo, basi tutachukulia hilo kama sehemu ya utafiti wa kisayansi unaoendelea.
 
Acha kutumia chatgpt kutujibu hoja zetu wee jamaa,
Chatgpt inakubali uwepo wa mungu.
 
Ukisema "sheria ya uvutano imepimwa kwa kiwango cha juu sana" halafu ukashindwa ku quantify kiwango hicho na kuonesha hakibadiliki, umeshindwa kuonesha sheria ya uvutano haibadiliki.

Pia, sio tu umeonesha kushindwa kuonesha sheria ya uvutano haibadiliki, lakini zaidi, umeonesha kuwa huwezi hata kuiweka sheria ya uvutano kinambari.

Unapiga hadithi za maneno kwenye mambo ambayo yanaweza kuwa quantified kwa namba na kupimwa kwa namba.
 
Bado huelewi tu,

Tukutane kesho
 
Acha kutumia chatgpt kutujibu hoja zetu wee jamaa,
Chatgpt inakubali uwepo wa mungu.
Unalazimisha ?

Badala ujibu hoja unalalamika natumia sijui nini ,

Nimetumia biblia mmekataa ,wewe jibu hoja acha kulialia ,kama huwezi kaa pembeni
 
Musk sio Atheist ni mkristo na anaamini uwepo wa Creator. Fatilia vizuri interview zake mkuu.
 
Kwa bahati mbaya cosmological argument sio hoja za uthibitisho.

Ni majaribio ya hoja zilizotolewa katika kujaribu kuthibitisha uwepo wa Mungu.

Hata hivyo zilishindwa.

Kama chanzo cha kwanza kinaweza kufikiriwa kutokuwa na chanzo na kwamba ni lazima iwe hivyo, kwanini tusifikirie hivyo hivyo na ulimwengu kuwa ulikuwepo milele na milele na hauna chanzo???

Kama kuna Deity anayekuwa exception kwenye mahitaji ya "kila kitu kuwa na chanzo" basi the same exception iwe applied kwenye Ulimwengu.

Na hata kama mtu akiamua kukubali hiyo nadharia kuwa kuna uncaused case bado hakuna kitu katika hiyo cosmological argument kitacho indicate kuwa huyo being ni huyu ambaye watu wamekuwa wakimuabudu kwa kumpa jina la Mungu.

Kwa hiyo the first mover au first cause haishabiani na tabia za deities ambao wanaabudiwa.
 
Unalazimisha ?

Badala ujibu hoja unalalamika natumia sijui nini ,

Nimetumia biblia mmekataa ,wewe jibu hoja acha kulialia ,kama huwezi kaa pembeni
Vyanzo vyako vya taarifa sio sahihi, ss unatumika bible na chatgpt kama reference, huoni kuwa unafanya vichekesho
 
Bado huelewi tu,

Tukutane kesho
Hapana, wewe ndiye huelewi.

Umeshindwa hata kuweka muktadha wa hoja yako kwa namba.

Unasema sheria ya uvutano haibadiliki.

Nakuuliza jana ilikuwa ngapi na leo iko ngapi ili tujue haibadiliki?

Umeshindwa kujibu.

Zaidi, hata ikiwa sheria za asili hazibadiliki, hilo linathibitishaje hazibadiliki kwa sababu zimewekwa na Mungu na si kwamba hazibadiliki zenyewe tu na hii ni anthropic principle tu, zingebadilika usingekuwapo kusema zimebadilika?

Huoni kwamba sheria za asili kubadilika au kutobadilika haithibitishi kwamba Mungu yupo?
 
Wala hayachanganyi mkuu, atheist ni wagonjwa wa akili, haiwezekani 3\4 ya watu duniani wana-experience ya deities alafu wao pekee wanaopinga deities ndo wajione wapo sahihi, huo ni ugonjwa wa akili.
Mental fitness or psychological well-being doesn't inherently depend on one's religious beliefs or lack thereof. An atheist, like anyone else, can be mentally fit if they maintain healthy coping mechanisms, emotional stability, and resilience in facing life's challenges.

Mental fitness is influenced by various factors, such as:

Self-awareness and purpose: Atheists might find purpose through personal values, relationships, or contributions to society rather than religious beliefs.

Support systems: Connection with family, friends, or like-minded communities can support mental well-being.

Mental health practices: Regular exercise, mindfulness, self-care, and seeking therapy when needed are key.

Ultimately, whether someone is mentally fit depends more on their habits, mindset, and circumstances than their spiritual or religious outlook.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…