Mkuu, mtoto asie na ufaham wa kujua/kutojua uwepo wa deities, hawezi kua sawa na mtu anaetumia ufaham wake kupinga uwepo wa deities.
Kama mtoto hana ufahamu hawezi kuwa na imani ya deity yeyote yule.
Hana ufahamu, Hana imani.
Atheist tuna ufahamu, ila hatuna imani.
Ufahamu upo kwa mtu yeyote yule anayefikia umri wa kuwa nao, regardless awe Theist au Atheist.
Tofauti ni kwamba, Theists mnatumia ufahamu huohuo, Kusema kuna Mungu, Kwa sababu ndivyo mlivyo aminishwa na wazazi/walezi wenu.
Wewe unasema kuna Mungu kwa sababu uliambiwa na kuaminishwa na wazazi/walezi wako kwamba kuna Mungu.
Usingeambiwa na kuaminishwa hivyo, Ungebaki bila imani ya kuamini kuna Mungu
Na mtoto hawezi kusema kuna Mungu, Unless aambiwe hivyo.
Lakini asipo ambiwa habari zozote zile za uwepo wa Mungu, Mtoto huyo Atakuwa na ufahamu, ila Hatokuwa na imani ya Mungu. Unless aambiwe na kuaminishwa na watu wengine
Mkuu, hata kua na mtizamo/maoni tofauti juu ya jambo fulani ni imani pia.
Imani ni kutokuwa na uhakika juu ya jambo fulani.
Huwezi kuwa na imani ya kwamba kuna Miti🌳, Wakati tayari unajua na kuiona miti ipo.
Unakuwa na imani kwa kitu ambacho hakipo na wala hujui kama kipo na huwezi kuthibitisha uwepo wake.
Ndivyo ilivyo kwa huyo Mungu mnaye amini yupo, ila hamuwezi kuthibitisha uwepo wake.