Science ina support uwepo wa Mungu

Science ina support uwepo wa Mungu

Imani ni kutokuwa na uhakika juu ya jambo au kitu fulani.

Hii maana umeitoa wapi kijana ? Hakuna maana ya Imani ya hivi. Ongeza umakini, kama huna hoja achana na huu mjadala.
Unaelewa maana ya infinity?

Infinity maana yake, Hakuna mwisho.

Hii sio maana ya Infinity, maana yake ni kisicho mpaka au kisicho na mwisho. Hata Kiswahili kina kushinda kuandika. Hakuna mwisho ndio nini ?
 
Kiranga acha kucheza na maneno mkuu. Ni kitu ( Maada) ipi hiyo isiyoundwa na atom?

Na hapa ndipo walipo feli hawa watu, wanaona kucheza na maneno ni uhaisia bali ni mchezo tu ambao haugusi hoja.

Sasa jambo dogo la "KITU" nalo analeta ngonjera nyingi. Chohcote ambacho kipo kiwe maada au kimiminika au visivyo kuwa hivyo vyote ni kitu.
 
Kwanza thibitisha uwepo wa huyo Mungu, USITUMIE Vitu ambavyo tayari vipo kwenye existence vyenyewe, kusema kwamba viliumbwa na huyo Mungu wenu wa kufikirika.

Thibitisha uwepo wa huyo Mungu, yeye kama yeye.

Au ukishindwa, Mwambie huyo Mungu wako aje ajidhihirishe mwenyewe na kujithibitisha yupo, Kama ana huo uwezo.

Jibu kwanza maswali niliyo kuuliza. Ndio maana huwa naweka sharti la ulazima wa kujibu maswali, sababu najua huwa hamjibu maswali na hamna hoja.

Jibu maswali niliyo kuuliza, ili tuendelee.
 
Twende taratibu utaelewa tu ,nitajenga hoja na majibu ya maswali yako moja moja ,ujue nyie Atheist sijui mnajitoa fahamu

Twende taratibu utaelewa tu

1. Je, Mungu Yupo Nje ya Wakati na Nafasi?
Mungu hayupo.

Ninyi ndio mnadai yupo na wala hamuwezi kuthibitisha uwepo wake.
Swali: Ulijuaje Mungu yupo nje ya wakati (time) na nafasi (space)?
Mungu hajawahi kuwepo na hayupo.

Sikusema Mungu yupo.

Mungu hajawahi kuwepo na hayupo.

Una elewa?
Falsafa ya Kibinadamu: Ikiwa Mungu ni chanzo cha kila kitu,
Mungu sio chanzo cha kila kitu, Ni wewe tu ndio unalazimisha Kwamba Mungu ni chanzo cha kila kitu.

Hakuna Mungu, Mungu hajawahi kuwepo na hayupo.
basi lazima awe nje ya mfumo wa vitu alivyoumba. Muda na nafasi ni sehemu za ulimwengu huu; hivyo Mungu, kama chanzo, lazima awe huru kutoka kwenye hizo dhana.
Mungu sio chanzo.

Ni wewe tu, unafosi na kulazimisha Mungu ni chanzo.

Mfano wa Kisayansi: Kabla ya Big Bang, hapakuwa na muda au nafasi; haya yalianza kuwepo baada ya tukio hilo. Chanzo cha Big Bang ni kitu ambacho kiko nje ya muda na nafasi. Hii inaendana na dhana ya Mungu kama chanzo kisicho cha kawaida.
Nadharia ya "Big- Bang" pamoja na Nadharia ya " Mungu" Zote hazijitoshelezi kutoa majibu yenye uhakika na uthibitisho.

Kwa hivyo "Big- Bang" pamoja na "Mungu" ni nadharia zisizo na ukweli wowote ule.
2. Je, Mungu Yupo au ni Fikra za Akili ya Binadamu?
Mungu hayupo.

Mungu mmemtunga vichwani mwenu ndio maana hamuwezi kuthibitisha uwepo wake.

Mungu ni mawazo yenu ya kufikirika tu, imaginations just an illusion.
Swali: Mungu hakuwa mahali au kabla, kwa hiyo hawezi kuwepo.

Hili linategemea dhana ya kibinadamu kuhusu kuwepo. Kwa mfano, kitu kisicho cha nyenzo hakihitaji "mahali." Hii ni sawa na dhana ya namba au sheria za mantiki. Hazipo mahali fulani, lakini zinaonekana kuwa kweli kila mahali.
FB_IMG_1732140393706_1.jpg

Mungu, kama kiumbe wa kiroho, hana umbo la kimwili na kwa hivyo hayuko "mahali" kama tunavyofahamu nafasi. Hii haimaanishi kuwa Mungu hayupo, bali ana asili tofauti na vitu vya ulimwengu wa nyenzo.
Ulijuaje Mungu yupo kabla ya kujua ni wa kiroho?

Usirukie kusema Mungu ni wa kiroho, kabla hujathibitisha uwepo wake.

Thibitisha kwanza, Ulijuaje Mungu yupo?

Kisha ndio uthibitishe, Ulijuaje ni wa kiroho?
3. Je, Mungu ni Chanzo Kisicho na Chanzo?

Swali: Ulijuaje Mungu ni chanzo kisicho na chanzo?

Hoja ya Kifalsafa: Mlolongo wa sababu hauwezi kwenda nyuma bila kikomo; lazima kuwe na sababu ya kwanza ambayo haikuhitaji kusababishwa. Hii ndiyo dhana ya "uncaused cause."
Hata huyo Mungu hawezi kuwepo tu mwenyewe bila sababu ya kwanza iliyo mfanya awepo.

Unathibitisha vipi kwamba ulimwengu ulisababishwa na huyo Mungu?
Mfano wa Nishati: Katika fizikia, nishati haiumbwi wala kuharibiwa. Ikiwa tunaweza kukubali kwamba kitu kama nishati kinaweza kuwepo bila chanzo, kwa nini isiwezekane kwa Mungu? Mungu anachukuliwa kuwa wa milele (necessary being), ambaye kuwepo kwake ni lazima kwa vitu vingine kuwepo.
Kama Energy(nishati) imeweza kuwepo bila kuwa created, Kwa nini ulazimishe tena kuna Mungu?

Kwa nini unafosi Mungu awepo?

Energy ipo, Haijawa created na wala Haimuhitaji huyo Mungu wako unaye jaribu kufosi awepo.
4. Je, Tunaweza Kuthibitisha Uwepo wa Mungu?

Swali: Ulijuaje Mungu yupo, na unathibitishaje hivyo?

Hoja ya Ontolojia: Dhana ya Mungu kama kiumbe mkamilifu zaidi inamaanisha kuwa lazima awepo. Kitu kisichokuwepo hakiwezi kuwa kikamilifu.
Una thibitisha vipi hiyo hoja ya
"ontolojia" ina ukweli?

Hiyo dhana ya " Mungu" inatoka wapi?
Hoja ya Maadili (Moral Argument): Uwepo wa sheria za maadili zinazofanana ulimwenguni kote huonyesha chanzo cha nje ambacho kimeweka misingi ya mema na mabaya.

Uzoefu wa Kibinafsi: Watu wengi ulimwenguni pote wanaripoti uzoefu wa kiroho unaoonyesha uwepo wa nguvu ya juu, ambayo inaitwa Mungu.
Bado huu si uthibitisho wa uwepo wa huyo Mungu.

Huo "uzoefu wa kiroho" hauna tofauti na Hallucinations.
5. Je, Mungu Anaweza Kujidhihirisha Mwenyewe?

Swali: Kwa nini Mungu hajidhihirishi mwenyewe?

Mantiki ya Uhuru wa Binadamu: Ikiwa Mungu angejidhihirisha waziwazi, kila mtu angeamini bila hiari. Hii ingeondoa uhuru wa kuchagua, ambao ni kipengele muhimu cha uhusiano wa kiroho.
Unathibitisha vipi kwamba Mungu angejidhihirisha waziwazi, Kila mtu angeamini bila hiari?

Kwa nini huyo Mungu anataka kuaminiwa badala ya kujulikana na kuonekana waziwazi kwamba yupo?
Mfano wa Ulimwengu: Ulimwengu wenyewe unaweza kuonekana kama ushahidi wa uwepo wa Mungu kwa wale wanaotafuta kuelewa. Sheria za asili, uhai, na mpangilio wa ulimwengu vinaweza kuchukuliwa kama dalili za Muumba.
Kama ni "dalili" tu za muumba,

Kwa nini sasa unahitimisha moja kwa moja kusema kwamba ulimwengu uliumbwa, ilihali hujui kama ulimwengu uliumbwa au hauku umbwa.

Kwa nini unahitimisha moja kwa moja kusema kuna muumba?

Huoni kwamba unafosi ulimwengu uwe umeumbwa kwa kuhitimisha moja kwa moja kuna muumba, Wakati Hujui kama ulimwengu haukuumbwa?
6. Je, Mungu ni Tungo ya Akili ya Binadamu?

Swali: Mungu ni mawazo tu ya kufikirika?

Historia ya Fikra za Kidini: Karibu kila tamaduni ulimwenguni ina dhana ya Mungu au miungu, hata zile ambazo hazijawahi kuwasiliana. Hii inaonyesha kwamba wazo la Mungu si tu tungo bali ni hitaji la msingi la binadamu kutafuta maana.
Hizo dhana za Mungu/ Miungu ni dhana za uongo ambazo zimerithishwa vizazi kwa vizazi.

Ndio maana huyo Mungu hajawahi kujidhihirisha mwenyewe kwamba yupo.

Ni watu tu, kama wewe unahangaika kumwelezea huyo Mungu na kuridhisha watu wengine dhana hii hii.

Na kwa kufanya hivyo, Mna endeleza kizazi cha kurithishana Mungu ambaye hata hamuwezi kuthibitisha uwepo wake.

Mna ng'ang'ana tu, yupo! yupo!, Wala hata hamjui yuko wapi?
Sayansi na Dini: Wanasayansi kama Einstein na Newton walikiri uwepo wa nguvu ya juu inayotawala ulimwengu, hata kama walikuwa na tafsiri tofauti za Mungu. Hii inaonyesha kwamba hata akili za hali ya juu hazikuona wazo la Mungu kama tungo tu.
Einstein na Newton kukiri uwepo wa Mungu, Hakuthibitishi na wala Hakudhihirishi uwepo wa huyo Mungu.

Hizo zitabaki imani na mitazamo yao tu isiyokuwa na uthibitisho wowote ule.
Nahitimisha kwa kukujulisha

Mungu hakuwa "mahali" au "kabla" kwa sababu muda na nafasi ni sehemu za ulimwengu alioumba.

Mungu si nothing; Yeye ni asili isiyo ya nyenzo ambayo haitegemei dhana za muda na nafasi.

Uwepo wa Mungu unaweza kuonekana kupitia falsafa, uzoefu wa kibinafsi, na ushahidi wa mpangilio wa ulimwengu.

Hoja ya kwamba Mungu ajidhihirishe inaendana na uhuru wa binadamu; Mungu ameacha dalili za uwepo wake, lakini haimlazimishi mtu kuamini.
Mungu hajawahi kuwepo, hayupo na hatakaa awepo.

Ni ninyi tu mnahangaika kumwelezea na kumtetea huyo Mungu ambaye hajawahi kuwepo na hayupo kujiongelea mwenyewe na kujidhihirisha mwenyewe kwamba yupo.
 
Ila mpaka sasa Allah huyo Kashindwa kujitetea mwenyewe kwamba yupo, Ni nyie tu mnahangaika kumwelezea na kumtetea "Allah mchovu na mdhaifu" ambaye hawezi hata kujitetea mwenyewe kwamba yupo.

Sasa mwenye nguvu sana na uwezo sana, kwa lipi ajiteteee, huoni kama kujitetea ni sifa ya udhaifu.

Allah anafanya anafanya anavyotaka na wala haulizwi kwayo, hii ndio maana ya ukamilifu.
 
Kutumia Quran kama uthibitisho wa Mungu ni sawa na kutumia Comic book kusema ndio uthibitisho wa Harry Potter.

Ndio maana huwa nataka mkosoe hoja, hapa ungekuja na ushahidi kuonyesha ya kuwa Qur'an haifai kuwa ushahidi, unaweka na vielelezo kuliko kulinganidha vitu viwili visivyo fanana huu ni upungufu wa akili.
 
1. Kuelewa Hoja ya Fine-Tuning

Hoja ya fine-tuning haisemi moja kwa moja kwamba Mungu lazima yupo. Inasema:

Kuna hali ya ajabu ambapo sheria za msingi za fizikia na vigezo vya ulimwengu (universal constants) zimepangwa kwa namna fulani ili kuwezesha maisha.

Hali hii ni ngumu kuelezeka kama matokeo ya bahati nasibu au jambo lisilo na mwelekeo.

Kwa sababu hiyo, uwepo wa mpangiliaji wa hali hii (akili ya juu) unakuwa maelezo bora zaidi.

Mfano wa Kiakili (Analogy):

Fikiria unakuta kompyuta imewashwa na inaendesha programu changamani sana. Huenda usijue nani aliyeiunda au hata vipi ilitokea, lakini ni mantiki kusema kuna mtu au kitu kilichosababisha kompyuta hiyo kuwepo na kufanya kazi hivyo. Huwezi kusema kompyuta ilijitokeza tu bila sababu.

2. Kujibu "Anthropic Bias"

Anthropic bias inasema kwamba tunapokaa katika ulimwengu unaoruhusu maisha, tunahisi kana kwamba ulimwengu umepangiliwa kwa ajili yetu kwa sababu hatungeweza kuishi katika ulimwengu tofauti. Hii ni sahihi kiasi, lakini haifuti haja ya kuuliza:

Kwa nini ulimwengu una sheria ambazo zinafaa kwa maisha?

Je, hizi sheria za fizikia (kama nguvu ya mvuto, nguvu za kielektroni) zilitokea kwa bahati tu, au kuna chanzo?

Mfano wa Bahati Nasibu:

Fikiria unasimama mbele ya kikosi cha wanajeshi 100 wakijaribu kukupiga risasi, na kila mmoja anakosa. Baada ya kunusurika, unaweza kusema: "Niko hai kwa sababu kila mmoja alikosa." Lakini si mantiki kuuliza kwa nini wote walikosa? Inawezekana kulikuwa na sababu zaidi ya bahati nasibu.

3. Fine-Tuning Inaweza Kutokana na Nini?

Hoja za kitheolojia husema kwamba kuna vyanzo vitatu vikuu vinavyoweza kuelezea fine-tuning:

1. Bahati Nasibu (Chance): Vigezo vya ulimwengu vilijipanga kwa bahati tu.

2. Sheria za Asili (Necessity): Hakuna njia nyingine; sheria za asili zilazimisha vigezo hivyo.

3. Mpangiliaji (Intelligent Designer): Kuwepo kwa akili ya juu inayoweka mpangilio huu.

Kwanini Bahati Nasibu na Sheria za Asili Zina Changamoto?

Bahati Nasibu: Uwezekano wa vigezo hivyo kuonekana kwa bahati ni mdogo mno. Wanasayansi kama Roger Penrose wameonyesha kuwa nafasi za kutokea kwa ulimwengu unaofaa kwa maisha ni trilioni nyingi kwa sifuri nyingi baadaye.

Sheria za Asili: Ikiwa sheria za asili zililazimisha hali hizi, bado tunapaswa kuuliza: Nani au nini kilitengeneza sheria hizo za asili?

Mfano wa Sheria:

Sheria ya mvuto inaeleza jinsi vitu vinavyovutana, lakini haielezi chanzo cha mvuto. Mpangiliaji anaweza kutoa maelezo zaidi ya chanzo hicho.

4. "Mpangiliaji Ana Hitaji Mpangiliaji Mwingine"

Hii ni hoja inayotegemea dhana kwamba kila kitu lazima kiwe na chanzo. Lakini falsafa na sayansi hufanya tofauti kati ya vitu viwili:

Vitu Vilivyo na Chanzo: Hivi ni vitu vinavyotegemea vingine (kama ulimwengu).

Vitu Vilivyo Bila Chanzo (Necessary Being): Hivi havihitaji chanzo. Mungu, kama chanzo cha kila kitu, huchukuliwa kama "Necessary Being."

Mfano wa Falsafa (Cosmological Argument):

Kila kitu chenye mwanzo kina sababu ya kuwepo.

Ulimwengu una mwanzo (Big Bang).

Kwa hiyo, ulimwengu unahitaji chanzo nje yake.

5. "Kuthibitisha Mungu"

Hoja hii inasisitiza kwamba hatuwezi kusema Mungu yupo mpaka tumthibitishe moja kwa moja. Hii ni kweli kwa kiwango fulani, lakini kuthibitisha mambo katika falsafa na sayansi mara nyingi huchukua njia ya kiashirio (inference):

Hatuthibitishi moja kwa moja mvuto, lakini tunaona athari zake.

Hatuthibitishi moja kwa moja chanzo cha Big Bang, lakini tunaona ushahidi wa matokeo yake.

Je, Tunaweza Kuona Athari za Mungu?

Mpangilio wa ulimwengu (fine-tuning).

Uwepo wa sheria za asili zisizobadilika.

Uwezo wa wanadamu kufikiri juu ya maswali ya msingi kama haya.

Unaandika kauli nyingi ambazo hazina uthibitisho kama uthibitisho wa Mungu ambaye hana uthibitisho.

Kwa mfano.

Unaandika sheria za asili zisizobadilika.

Unathibitishaje sheria za asili hazibadiliki?

Toa mfano wa sheria moja ya asili ambayo haibadiliki na tueleze umethibitisha vipi haibadiliki.
 
Ili mjadala ulete maana, unapo ulizwa swali jibu swali kwanza kisha uendelee.

Kutokea wapi ni swali la uongo, sababu hiyo nayo ni nafasi ambayo ameiumba mwenyewe. Uliza swali la maana linamsadifu Mola muumba.
Kwa nini unalazimisha ulimwengu una mola muumba?
Kwahiyo akijitokeza ndio utaamini yupo au kwamba yupo ? Hili ni swali la kitoto na hoja muflisi, sababu uwepo wa kitu sio lazima uonekane kwa macho, bali kuna vingine vinakuwepo huthibitisha uwepo wa kingine moja kwa moja. Mfano kuwepo kwako hakulazimishi tutake baba yako ajitokeze ili tujue yupo.
Hata kuwepo kwa ulimwengu, Hakuhitaji kuwepo huyo Mungu wako, unayefosi na kulazimisha awepo.

Una elewa hilo?
Wapi nimesumbuka ? Sijawahi wala sitokuja kusumbuka sababu uwepo wake unajieleza na uko wazi, ni mtu tu kuamua kuelewa na kufikiri kwa usahihi. Katika jambo jepesi ni kuthibithsa juu ya uwepo wake.

Hana haja hiyo sababu yeye ni muweza wa yote wala hana shida hiyo sababu yeye amejitosheleza.
Huyo Mungu kama ni muweza wa vyote, Alishindwaje kuumba dunia isiyo na uovu wala mabaya?
Kumtaka wewe afanye unavyotaka ndio udhaifu wenyewe. Yeyey hana haja ya kujitokeza kuna vingi viko wazi vinadhihirisha uwepo wake. Itakuwa hujui maana ya UDHAIFU kijana.
Thibitisha uwepo wa huyo Mungu, yeye kama yeye.

USITUMIE vitu ambavyo tayari vipo kwenye existence vyenyewe, kusema eti ndio uthibitisho wa uwepo wa huyo Mungu.
Sisi hatuhangaiki bali tuna washangaa nyie ambao hata hili dogo la uwepo wa Mungu mnashindwa kulitambua na mshindwa kulithibitisha.
Hujathibitisha Mungu yupo, ila unafosi kutumia vitu ambavyo tayari vipo kwenye existence vyenyewe, kusema ndio uthibitisho wa Mungu.

Nilikwambia na Ninakwambia hivi, Thibitisha uwepo wa huyo Mungu( Yeye kama yeye).

USITUMIE vitu ambavyo tayari vipo kwenye existence vyenyewe, kusema kwamba viliumbwa na huyo Mungu wako wa kufikiria na kusadikika.
Leta ushahidi hapa nani alimtunga na ilikuwa lini ?
Muhammad S.A.W ndio alimtunga huyo Allah, Ilikuwa kipindi cha huyo mtume wenu Mudi.

Wewe kisai na wenzako wote wa imani ndio mliandikiwa huyo Mungu(Allah) na kuwekewa kwenye kitabu mnacho kiita Quran.
Sharti la kuja hadharani ni udhaifu na ni upungufu wa akili. Yeyey ni mkamilifu na ameshajidhihirisha uwepo wake kwa uwepo wako na ulimwengu kwa ujumla.
Uwepo wa ulimwengu, Hauhitaji uwepo wa huyo Allah.

Ni wewe tu unafosi na kulazimisha hivyo.
Hujajibu swali nililo kuuliza, tuambie ilikuwaje vikawepo ? Je vimejiumba vyenyewe au vimetokana pasi na chochote ?
Ulimwengu na vyote vilivyomo except man-made things, Vimekuwepo milele.

Havijaumbwa na yeyote.

Vimekuwepo ndio maana tumevikuta vipo na vitaendelea kuwepo.

Visingekuwepo tusingevikuta vipo.
Muanzilishi wa kila kitu anakuwaje na chanzo kijana ? Maana hata hicho unachodai lazima kiwe kimemuumba nacho ni KITU pia.
Basi huyo Mungu wenu pia Si kitu.

Huyo Mungu wenu ni Nothing.

Hayupo.
Infinity ina exist ? Kwa akili yako tu ndogo.
Infinity= isiyo kuwa na mwisho.

Hata ulimwengu hauna mwisho.
 
Thibitisha hili, ukiweza kuthibitisha hili mimi naacha kuchangia humu jf.
Huyo Allah wa kwenye Quran, Hajawahi kuonekana physically.

Hana tofauti na Abunuwasi wa kwenye Hekaya.

Huu ni uthibitisho tosha kwamba hiyo Quran yenu ni hadithi kama hadithi zingine tu.
 
Sasa mwenye nguvu sana na uwezo sana, kwa lipi ajiteteee, huoni kama kujitetea ni sifa ya udhaifu.
Hata kutaka kuswaliwa, kuaminiwa na kuabudiwa ni sifa ya udhaifu.

Ndio maana mnakaa kila siku kuswali swala tano kwa Allah mdhaifu na mchovu ambaye hawezi hata kuwapa mahitaji yenu mpaka msali kumkumbusha na kumuomba.
Allah anafanya anafanya anavyotaka na wala haulizwi kwayo, hii ndio maana ya ukamilifu.
Allah wenu huyo ana exist kwenye kitabu cha Quran tu, wala hajawahi kuwepo na hayupo popote pale.

Huyo Allah wenu hana tofauti na Abunuwasi ambaye ana exist kwenye kitabu pia.
 
Ndio maana huwa nataka mkosoe hoja, hapa ungekuja na ushahidi kuonyesha ya kuwa Qur'an haifai kuwa ushahidi, unaweka na vielelezo kuliko kulinganidha vitu viwili visivyo fanana huu ni upungufu wa akili.
Quran sio ushahidi ni hadithi za kusadikika na kufikirika tu za kitabuni.

Kwa sababu huyo Allah ana ongelewa kwenye Quran yake tu(kitabuni), Tofauti na hapo hayupo kwingine popote pale.

Sawa tu na Abunuwasi, ana ongelewa kwenye hekaya zake tu(kitabuni),
Tofauti na hapo hayupo kwingine popote pale.

Bado tu huoni hiyo "Quran" yako sio ushahidi?

Unahangaika kufosi fosi tu hadithi zenu uchwara za kwenye Quran eti ndio uthibitisho!!!
 
Unaandika kauli nyingi ambazo hazina uthibitisho kama uthibitisho wa Mungu ambaye hana uthibitisho.

Kwa mfano.

Unaandika sheria za asili zisizobadilika.

Unathibitishaje sheria za asili hazibadiliki?

Toa mfano wa sheria moja ya asili ambayo haibadiliki na tueleze umethibitisha vipi haibadiliki.

Sheria za asili niazosema hapa ni kanuni za msingi zinazotawala uhalisia wa ulimwengu. Ingawa hatuwezi kuthibitisha kwa uhakika wa asilimia 100 kuwa hazitabadilika milele (kwa sababu hatuwezi kuangalia kila wakati na mahali), Bali tuna ushahidi wa kutosha wa kihistoria na wa majaribio kwamba zipo na zinadumu.

Mfano wa Sheria za Asili Ambazo Hazijabadilika:

Sheria ya Graviti (Newton's Law of Universal Gravitation): Sheria hii inaelezea mvuto kati ya miili miwili kulingana na uzito na umbali kati yao. Katika majaribio yote na uchunguzi wa miaka mingi, mvuto umeendelea kufuata kanuni ile ile.

Uthibitisho: Uchunguzi wa mizunguko ya sayari, mwendo wa vitu duniani, na majaribio ya Galileo hadi leo.

Sheria ya Hifadhi ya Nishati (Law of Conservation of Energy): Nishati haiwezi kuundwa wala kuangamizwa, inaweza tu kubadilika kutoka aina moja kwenda nyingine. Sheria hii imethibitishwa mara nyingi katika fizikia, kemia, na uhandisi.

Uthibitisho: Maendeleo ya teknolojia kama injini za mwako wa ndani na umeme yanategemea utendaji wa sheria hii.

Sheria hizi hazijawahi kuonyesha dalili za kubadilika katika vipimo vyote vya kisayansi vilivyofanyika. Kwa kuwa uhalisia unategemea kanuni hizi, tunachukulia kuwa ni za kudumu hadi ushahidi wa kinyume utakapotolewa.

Hatuwezi kuthibitisha kwa njia ya kimalizio kwamba sheria hizi hazibadiliki, lakini tunaweza kutumia hoja zifuatazo:

Empirical Evidence (Uchunguzi wa Kipekee): Vipimo na majaribio vimeonyesha kuwa sheria hizi zimekuwa thabiti kwa muda wote wa uchunguzi wa kisayansi (maelfu ya miaka).

Predictability: Sheria hizi zinatumika kutabiri matukio yajayo. Mfano, tunatumia sheria za mvuto kutuma satelaiti angani, na inafanya kazi kila mara.

Lack of Contradictory Evidence: Hakuna ushahidi wa kubadilika kwa sheria hizi, hata kwa uchunguzi wa kina wa kisayansi.

Kama sheria za asili ni za kudumu, lazima kuwepo na chanzo cha msingi kilichoweka sheria hizo. Chanzo hiki ni kile ambacho wanateolojia na wanafalsafa wengi hukiita Mungu.

Ikiwa sheria za asili zinatokana na bahati nasibu, ni vigumu kuelewa kwa nini zipo kwa mpangilio mkamilifu na ni thabiti. Uwepo wa sheria za asili zinazofanya kazi ni hoja ya kidokezo cha chanzo cha akili (intelligent source).
 
Mungu hayupo.

Ninyi ndio mnadai yupo na wala hamuwezi kuthibitisha uwepo wake.

Mungu hajawahi kuwepo na hayupo.

Sikusema Mungu yupo.

Mungu hajawahi kuwepo na hayupo.

Una elewa?

Mungu sio chanzo cha kila kitu, Ni wewe tu ndio unalazimisha Kwamba Mungu ni chanzo cha kila kitu.

Hakuna Mungu, Mungu hajawahi kuwepo na hayupo.

Mungu sio chanzo.

Ni wewe tu, unafosi na kulazimisha Mungu ni chanzo.

Nadharia ya "Big- Bang" pamoja na Nadharia ya " Mungu" Zote hazijitoshelezi kutoa majibu yenye uhakika na uthibitisho.

Kwa hivyo "Big- Bang" pamoja na "Mungu" ni nadharia zisizo na ukweli wowote ule.

Mungu hayupo.

Mungu mmemtunga vichwani mwenu ndio maana hamuwezi kuthibitisha uwepo wake.

Mungu ni mawazo yenu ya kufikirika tu, imaginations just an illusion.

View attachment 3158253

Ulijuaje Mungu yupo kabla ya kujua ni wa kiroho?

Usirukie kusema Mungu ni wa kiroho, kabla hujathibitisha uwepo wake.

Thibitisha kwanza, Ulijuaje Mungu yupo?

Kisha ndio uthibitishe, Ulijuaje ni wa kiroho?

Hata huyo Mungu hawezi kuwepo tu mwenyewe bila sababu ya kwanza iliyo mfanya awepo.

Unathibitisha vipi kwamba ulimwengu ulisababishwa na huyo Mungu?

Kama Energy(nishati) imeweza kuwepo bila kuwa created, Kwa nini ulazimishe tena kuna Mungu?

Kwa nini unafosi Mungu awepo?

Energy ipo, Haijawa created na wala Haimuhitaji huyo Mungu wako unaye jaribu kufosi awepo.

Una thibitisha vipi hiyo hoja ya
"ontolojia" ina ukweli?

Hiyo dhana ya " Mungu" inatoka wapi?

Bado huu si uthibitisho wa uwepo wa huyo Mungu.

Huo "uzoefu wa kiroho" hauna tofauti na Hallucinations.

Unathibitisha vipi kwamba Mungu angejidhihirisha waziwazi, Kila mtu angeamini bila hiari?

Kwa nini huyo Mungu anataka kuaminiwa badala ya kujulikana na kuonekana waziwazi kwamba yupo?

Kama ni "dalili" tu za muumba,

Kwa nini sasa unahitimisha moja kwa moja kusema kwamba ulimwengu uliumbwa, ilihali hujui kama ulimwengu uliumbwa au hauku umbwa.

Kwa nini unahitimisha moja kwa moja kusema kuna muumba?

Huoni kwamba unafosi ulimwengu uwe umeumbwa kwa kuhitimisha moja kwa moja kuna muumba, Wakati Hujui kama ulimwengu haukuumbwa?

Hizo dhana za Mungu/ Miungu ni dhana za uongo ambazo zimerithishwa vizazi kwa vizazi.

Ndio maana huyo Mungu hajawahi kujidhihirisha mwenyewe kwamba yupo.

Ni watu tu, kama wewe unahangaika kumwelezea huyo Mungu na kuridhisha watu wengine dhana hii hii.

Na kwa kufanya hivyo, Mna endeleza kizazi cha kurithishana Mungu ambaye hata hamuwezi kuthibitisha uwepo wake.

Mna ng'ang'ana tu, yupo! yupo!, Wala hata hamjui yuko wapi?

Einstein na Newton kukiri uwepo wa Mungu, Hakuthibitishi na wala Hakudhihirishi uwepo wa huyo Mungu.

Hizo zitabaki imani na mitazamo yao tu isiyokuwa na uthibitisho wowote ule.

Mungu hajawahi kuwepo, hayupo na hatakaa awepo.

Ni ninyi tu mnahangaika kumwelezea na kumtetea huyo Mungu ambaye hajawahi kuwepo na hayupo kujiongelea mwenyewe na kujidhihirisha mwenyewe kwamba yupo.

Umebaki unalalamika tu Kuwa Mungu hayupo ,Mungu hayupo

Ok ngoja nikujuze kuhusu hoja zako, japo unarudi kule kule kila mara

1. “Ulijuaje Mungu yupo kabla ya kujua ni wa kiroho?”

Hoja ya "kujuaje Mungu yupo kabla ya kusema ni wa kiroho" inahitaji kueleweka ndani ya muktadha wa dhana za ontolojia (nature of being) na epistemolojia (how we know).

Jibu: Dhihirisho la uwepo wa Mungu linatokana na tafakuri juu ya mambo yasiyoelezeka kirahisi kupitia asili ya ulimwengu. Wanafilosofia kama Thomas Aquinas walijenga hoja za kimantiki, kama ile ya "Kila kitu chenye mwanzo lazima kiwe na sababu ya kuwepo." Hii inamaanisha kwamba lazima kuwe na chanzo cha mwisho kisicho na mwanzo (uncaused cause), ambacho ni Mungu. Tafakuri hii haimlazimishi Mungu awe wa kiroho moja kwa moja, bali inahitimisha uwepo wa chanzo kisicho cha asili. Hali ya kuwa Mungu ni wa kiroho hujengwa kutokana na dhana kwamba chanzo hicho hakiwezi kuwa cha kimwili kwa kuwa kipo nje ya muda na nafasi.

2. “Thibitisha kwanza, ulijuaje Mungu yupo?”

Hoja hii inahitaji mjadala wa kina kuhusu ushahidi wa uwepo wa Mungu.

Jibu: Mungu anaweza kueleweka kupitia ishara za ulimwengu (evidence of design) na hoja za kifalsafa kama vile:

Fine-tuning: Ulimwengu unaonekana kuwa umewekwa kwa ustadi mkubwa ili kuleta uhai. Sababu ya hali hii haielezeki kwa bahati tu. Hata atheists kama Fred Hoyle alikiri kwamba "design seems to have been fine-tuned."

Moral Law (Sheria ya Maadili): Binadamu wana maadili ya asili ambayo hayawezi kuelezewa na mchakato wa kibaolojia tu. Kama sheria zipo, lazima kuwe na Sheria Kuu (Moral Law Giver).

Hoja ya Ontolojia: Uwepo wa dhana ya Mungu unashawishi kuwepo kwa Mungu. Wazo la kuwa na Mungu Mkamilifu halingetokea bila chanzo kamili.

Uzoefu wa Kiroho: Milioni ya watu duniani wamepata uzoefu wa kiroho. Hata wanasayansi wa akili wanakubali kuwa uzoefu wa aina hii ni halisi kwa wahusika. Ingawa unaweza kusemwa kuwa hallucination, huwezi kupuuza ushuhuda mkubwa kiasi hiki.

3. “Unathibitisha vipi kwamba ulimwengu ulisababishwa na huyo Mungu?”

Hoja ya sababu kuu inabainisha kwamba kila kitu kilicho na mwanzo lazima kiwe na chanzo.

Jibu: Ulimwengu unaonyesha kuwa ulianza kuwepo (Big Bang theory). Kama ulianza, lazima kuwe na chanzo chake. Chanzo hiki hakiwezi kuwa cha asili kwa sababu chanzo cha asili kingekuwa ndani ya ulimwengu wenyewe, na hivyo kuhitaji chanzo kingine. Mungu ndiye chanzo hicho kisicho cha kimwili, kisicho cha wakati, na kisicho na mwanzo.

4. “Kama Energy imeweza kuwepo bila kuwa created, kwa nini ulazimishe kuna Mungu?”

Jibu: Hoja ya nishati kama chanzo cha kila kitu inapingwa na ukweli kwamba nishati haiwezi kujieleza yenyewe au kuamua kitu kwa hiari. Nishati haina akili, lakini ulimwengu unaonyesha ushahidi wa akili kubwa iliyojipanga. Hii inatupeleka kwa chanzo chenye uwezo wa kuumba kwa hiari, ambacho ni Mungu.

5. “Unathibitisha vipi kwamba Mungu angejidhihirisha waziwazi, kila mtu angeamini bila hiari?”

Jibu: Mungu ameacha dalili wazi za uwepo wake (design, moral law, and spiritual experiences), lakini amehifadhi uhuru wa mwanadamu wa kuchagua. Imani si suala la kulazimishwa; ni uamuzi wa hiari. Kama Mungu angejidhihirisha waziwazi kwa kiwango cha kumlazimisha kila mtu kuamini, uhuru wa hiari ungeondolewa, na mahusiano ya kiroho hayangekuwa ya kweli.

6. “Kwa nini unahitimisha moja kwa moja kusema kuna Muumba?”

Jibu: Hoja ya muumba inatokana na asili ya ulimwengu. Kama kila kitu chenye mwanzo kina chanzo, basi ulimwengu lazima uwe na chanzo. Uchunguzi wa kina hauoneshi chanzo kingine chochote chenye sifa zinazolingana na Mungu wa kiroho: asiye na mwanzo, wa milele, na mwenye uwezo wote.

7. “Dhana za Mungu ni za uongo ambazo zimerithishwa vizazi kwa vizazi.”

Jibu: Hoja kwamba Mungu ni dhana ya kubuni hupuuzilia mbali ushuhuda wa kihistoria, kijamii, na kiroho. Historia inaonyesha kwamba wazo la Mungu linatokea kwa watu wa kila tamaduni, hata zile ambazo hazijawahi kuwasiliana. Hii inaonyesha kuwa dhana ya Mungu si matokeo ya kurithishana tu, bali ni sehemu ya uelewa wa kina wa mwanadamu.

8. “Einstein na Newton kukiri uwepo wa Mungu hakuthibitishi kwamba yupo.”

Jibu: Einstein na Newton hawakuthibitisha uwepo wa Mungu moja kwa moja, lakini walikubali kwamba kuna akili ya juu kutokana na uzuri na utaratibu wa ulimwengu. Ingawa ushuhuda wao hauhitimishi mjadala, unatoa msingi mzuri wa kuelewa kwamba wazo la Mungu halipingani na akili za juu zaidi.
 
Ok, nitakujibu hivi hoja zako,then tutaendelea zaidi

Mungu, kulingana na falsafa ya teolojia, si sehemu ya halisia inayozingatia ulimwengu wa nyenzo (material reality) bali ni chanzo cha halisia hiyo. Hii ni kwa sababu:
Samahani unaweza kunipatia tafsiri ya neno halisia?
 
Sheria za asili niazosema hapa ni kanuni za msingi zinazotawala uhalisia wa ulimwengu. Ingawa hatuwezi kuthibitisha kwa uhakika wa asilimia 100 kuwa hazitabadilika milele (kwa sababu hatuwezi kuangalia kila wakati na mahali), Bali tuna ushahidi wa kutosha wa kihistoria na wa majaribio kwamba zipo na zinadumu.

Mfano wa Sheria za Asili Ambazo Hazijabadilika:

Sheria ya Graviti (Newton's Law of Universal Gravitation): Sheria hii inaelezea mvuto kati ya miili miwili kulingana na uzito na umbali kati yao. Katika majaribio yote na uchunguzi wa miaka mingi, mvuto umeendelea kufuata kanuni ile ile.

Uthibitisho: Uchunguzi wa mizunguko ya sayari, mwendo wa vitu duniani, na majaribio ya Galileo hadi leo.

Sheria ya Hifadhi ya Nishati (Law of Conservation of Energy): Nishati haiwezi kuundwa wala kuangamizwa, inaweza tu kubadilika kutoka aina moja kwenda nyingine. Sheria hii imethibitishwa mara nyingi katika fizikia, kemia, na uhandisi.

Uthibitisho: Maendeleo ya teknolojia kama injini za mwako wa ndani na umeme yanategemea utendaji wa sheria hii.

Sheria hizi hazijawahi kuonyesha dalili za kubadilika katika vipimo vyote vya kisayansi vilivyofanyika. Kwa kuwa uhalisia unategemea kanuni hizi, tunachukulia kuwa ni za kudumu hadi ushahidi wa kinyume utakapotolewa.

Hatuwezi kuthibitisha kwa njia ya kimalizio kwamba sheria hizi hazibadiliki, lakini tunaweza kutumia hoja zifuatazo:

Empirical Evidence (Uchunguzi wa Kipekee): Vipimo na majaribio vimeonyesha kuwa sheria hizi zimekuwa thabiti kwa muda wote wa uchunguzi wa kisayansi (maelfu ya miaka).

Predictability: Sheria hizi zinatumika kutabiri matukio yajayo. Mfano, tunatumia sheria za mvuto kutuma satelaiti angani, na inafanya kazi kila mara.

Lack of Contradictory Evidence: Hakuna ushahidi wa kubadilika kwa sheria hizi, hata kwa uchunguzi wa kina wa kisayansi.

Kama sheria za asili ni za kudumu, lazima kuwepo na chanzo cha msingi kilichoweka sheria hizo. Chanzo hiki ni kile ambacho wanateolojia na wanafalsafa wengi hukiita Mungu.

Ikiwa sheria za asili zinatokana na bahati nasibu, ni vigumu kuelewa kwa nini zipo kwa mpangilio mkamilifu na ni thabiti. Uwepo wa sheria za asili zinazofanya kazi ni hoja ya kidokezo cha chanzo cha akili (intelligent source).
Gravity umeichunguza kwa miaka mingapi ukagundua haibadiliki?

Umehakikishaje kuwa sheria ya gravity haibadiliki?

Umeipima kwa kipimo gani na kupata matokeo kwa unit gani isiyobadilika kuhakikisha gravity haibadiliki?

Unajuaje sheria haibadiliki kweli na si kwamba wewe unafanya fallacy of induction tu?
 
Salaam wakuu,

Science inasema, kila kitu kimeundwa na atom, bt maandiko yanasema, kila kitu kimeundwa Mungu.

Science inasema atom imeundwa na sehem 3(proton, neuron & electron bt maandiko yanasema Mungu anaundwa na sehem 3(Mungu baba, mwana & roho mtakatifu).

Kwa mtiririko huo, nahitimisha kwa kusema, science inasupport uwepo wa Mungu kwa 100%.
Mkuu linapokuja suala la Mungu sayansi sio kipimo sahihi cha kuthibitishia/ justify uwepo wa Mungu. Kwasababu kubwa mbili

1.sayansi yenyewe ni matokeo ya uumbaji wa MUNGU.

2. sayansi kwakua ni jitihada za binadamu kutafiti uumbaji wa MUNGU hivyo haina access katika ulimwengu wa ROHO yenyewe ina deal na ulimwengu unaonekana tu sasa je vipi kuhusu ulimwengu wa roho ambako huko pia Mungu anatawala kwa mfumo huo.
 
Samahani unaweza kunipatia tafsiri ya neno halisia?
Kwa uelewa wangu "halisia" humaanisha kitu au jambo ambalo ni la kweli, lililopo, au linalojulikana kuwa halisi, tofauti na kitu cha kufikirika au cha kubuni.
 
Mungu Ni Nje ya Halisia ya Kawaida: Kila kitu kinachojulikana kupitia hisia zetu kipo ndani ya mfumo wa nafasi na muda (time and space). Mungu, kwa mujibu wa hoja za kidini na kifalsafa, yupo nje ya mfumo huo, akiwa chanzo chake.
Vilivyo nje ya halisia ni vile ambavyo vipo kinadharia.

Yani kwa neno rahisi naweza kusema kinyume cha neno uhalisia ni kufikirika.

Kwa hiyo ukim-term Mungu kwa option hiyo ya kutokuwa halisia utakuwa umemuweka kundi moja na fictional characters wote ambao hawako reality.

Spiderman hayupo kihalisia, Unicorn naye si kiumbe ambaye yupo kihalisia. Hiyo ni mifano michache tu ya vitu ambavyo havipo kihalisia.
 
Kifupi ni kwamba hoja ya fine tuning haithibitishi Mungu yupo, tukiichunguza zaidi tunapata maswali zaidi kama hata hiyo fine tuning ipo kweli ama tunaona fine tuning kwa sababu ya anthropic principle tu.

Hujathibitisha Mungu yupo.

Umetaka kuthibitisha Mungu yupo kwa hoja ya fine tuning.

Tukaona hujathibitisha hata kama hiyo fine tuning ipo.

Mwishowe, hujathibitisha Mungu yupo wala fine tuning ipo.
hamis77 Hujajibu hii bado.
 
Back
Top Bottom