Andrew Nyerere
JF-Expert Member
- Nov 10, 2008
- 3,007
- 2,451
- Thread starter
- #21
Linalosemwa hapa ni kwanba kuna maendeleo makubwa sana kiasi kwamba siku hizi inawezekana kumtengeneza binadamu. 1. Mwaka 1947 mfizikia wa Hungary . Dr. Dennis Gabor aligundua jinsi ya kutengeneza picha za 3-dimension,yaani picha inayoonyesha urefu,upana na unene:tofauti na picha ya kawaida ambayo inaonyesha tu urefu na upana. Hii picha aliyoigundua. Dr. Gabor inaitwa hologram. Ulikuwa ni ugunduzi mkubwa na miaka 24 baadaye 1971, . Dr. Gabor alipata tuzo ya. Nobel. 2.. Ugunduzi wa. Dr. Gabor ulianzisha holografi,lakini bado wakati ule haikuwezekana kutengeneza hologram. Kilichohitajika ilikuwa ni kitu kinaitwa mwangaza ambao ni monochromatic,yaani mwangaza ambao upo katika wimbi moja tu. Hakuna aliyejua jinsi ya kutengeneza mwangaza wa namna hiyo 1947. Lakini 1960 mambo yalibadilika ghafla laser zilipogundulika.. Laser ni njia ya kutengeneza mwangaza ambao muonzi wake unakwenda mbele bila kusambaratika.. Laser zinaweza kufanya hivyo kwa sababu zina monochromatic light. Kwa hiyo sasa ilikuwa inawekana kutengeneza picha za hologram,picha za 3-d.