Hizi jamaii toka mwanzo zilibebwa mno na sera za utawala wa kikoloni, zilipata nafasi kubwa za kiupendeleo kwenye biashara mbalimbali .
Pia ,zilijenga biashara zao katika misingi ya kimtandao katika ngazi ya familia, hii ilichangia biashara zao kupata mrithi aliepikwa kuanzia chini katika mifumo ya kusimamia biashara zao vizuri .
Pia jamii hizi hupata mikopo na kuaminika kirahisi kwenye bank na taasisi mbalimbali kutokana na mifumo yao ya kibiashara walivyo iunda, inakua rahisi kuaminika kwa sababu ni mifumo imara mno .