Uchaguzi 2020 Secretary Pompeo azungumzia kinachoendelea Tanzania kuhusu mambo ya Uchaguzi

Uchaguzi 2020 Secretary Pompeo azungumzia kinachoendelea Tanzania kuhusu mambo ya Uchaguzi

dikteta2020

JF-Expert Member
Joined
Aug 14, 2018
Posts
595
Reaction score
3,991
We are deeply concerned by reports of election irregularities, politically motivated arrests, and violence during Tanzania’s elections last week. We urge authorities to fully address concerns of irregularities and will review allegations of the use of force against civilians.

20201102_180121.jpg

NB: Kwa wale wasioelewa ni kuwa kwa utaratibu wa Marekani, huyu akishaongea kinachofuata ni hatua za kinidhamu. Yani kwa upande wa Marekani huyu akishazungumza basi jiandae kwa kuchukuliwa hatua maana mwisho wa matamko ni kwa secretary of state.

Pili Marekani akishachukua hatua wanafuata washirika wake wa Ulaya.

Marekani kwa siku za karibuni imechukua hatua kali kwa wavurugaji wa uchaguzi mataifa mbalimbali
 
1604329850305.png



UINGEREZA YATAKA UCHUNGUZI HURU UFANYIKE KUHUSU UCHAGUZI WA TANZANIA

Kulingana na taarifa iliotolewa na Uingereza na kuchapishwa tarehe mosi mwezi Novemba, Taifa hilo sasa linajiunga na mataifa mengine katika kuitisha uchunguzi huru ufanywe ili kuondoa wasiwasi unaozidi kuenea katika taifa La Tanzania

Waziri wa masuala ya Afrika James Duddridge amesema kwamba Uingereza inashangazwa na ripoti za ghasia na kiwango cha juu cha maafisa wa polisi katika vituo vya kupigia kura ikiwemo suala zima la kukamatwa kwa baadhi ya viongozi wa upinzani.

Amesema kwamba Uingereza pia ina wasiwasi kuhusu madai ya kuingiliwa kwa uchaguzi huo, kujazwa kwa kura katika masanduku ya kupigia kura na kuzuiliwa kwa mawakala wa vyama vya upinzani kuingia katika vituo vya kupigia kura.

Vilevile taifa hilo limeshangazwa na madai ya ripoti za ghasia na kiwango kikubwa cha maafisa wa polisi katika vituo vya kupigia kura wakati wa uchaguzi, ikiwemo kukamatwa kwa baadhi ya viongozi wa upinzani.

Kulingana na taarifa hiyo , Uingereza imesema kwamba kwa Tanzania kuwa dhabiti na kustawi katika siku za usoni , itahitaji mchakato wa kidemokrasia ulio huru na wa haki, unaoungwa mkono na vyombo vya habari vilivyo huru.

Source: BBC
 
Dunia inaanza kufunguka matendo yao ya aibu yanazidi kuanikwa, uchaguzi ule haukuwa huru na wa haki hilo halina ubishi, yeyote anayetetea uhuni ule kwasababu yoyote ile ana matatizo ya akili.

Walidhani yatapita hivi hivi, sasa dunia imeanza kuwanyooshea kidole.

The option is simple; fanya wanavyoelekeza, kama hutaki subiri hatma yako, najua sasa huko lumumba hapakaliki, hapalaliki, hata hivi vibuyu vyao humu jf vinatetemeka.
 
Tunataka dunia kwa pamona ije tanzania kujionea jinsi vizazi na vizazi vya wazawa watanzania walionyimwa uhuru,elimu, afya na mengine mengi, tunawaalika wapenda amani na haki duniani kote watuunge mkono katika hili. Libyelebye
 
Dunia inaanza kufunguka matendo yao ya aibu yanazidi kuanikwa, uchaguzi ule haukuwa huru na wa haki hilo halina ubishi, yeyote anayetetea uhuni ule kwasababu yoyote ile ana matatizo ya akili.

Walidhani yatapita hivi hivi, sasa dunia imeanza kuwanyooshea kidole.

The option is simple, fanya wanavyoelekeza, kama hutaki subiri hatma yako, najua sasa huko lumumba hapakaliki, hapalaliki, hata hivi vibuyu vyao humu jf vinatetemeka.
Wasiokuwa na akili ni wale wanaodai kukamata kura feki na kuzichoma moto badala ya kuzihifadhi kama exhibit. Kura watengeze wao wazipige watoe kilio feki halafu kabla ya watu wenye weledi hawajaziona wanazichoma moto. Watanzania hatudanganyiki
 
Kama tungegomea uchaguzi huo uozo wao ungeanikwa vipi nje ya mipaka yetu?!

Ujifunze kufikiria nje ya box old man.
Hakuna jipya.

Uozo umekuwepo siku zote.

Tatizo lenu mko wepesi wa kusahau.

Na mpaka kufika 2025, haya ya 2020 mtakuwa mshayasahau na mtashiriki tena uchaguzi chini ya mazingira haya haya ya leo, jana, juzi, na majuzi.

2015 Lowassa hakukubaliana na matokeo. Unabisha?

2010 Slaa hakukubaliana na matokeo. Unabisha?
 
Back
Top Bottom