Uchaguzi 2020 Secretary Pompeo azungumzia kinachoendelea Tanzania kuhusu mambo ya Uchaguzi

Uchaguzi 2020 Secretary Pompeo azungumzia kinachoendelea Tanzania kuhusu mambo ya Uchaguzi

Hii request kwa Authorities to “fully address concerns of irreguraties” wala hakuna mtu ndani ya Chama na Serikali atakayeijari. Kuadress maana yake ni kurudia uchaguzi ni hili hawa jamaa hawatolifanya kamwe

Ndio tatizo la kuwa na NEC na Majaji wanaopokea maagizo kutoka kwa Raisi wa Nchi. Hili bila Katiba kufanyiwa amendment, CCM itakaa juu kileleni daima dumu maana kila uchaguzi watakuwa wanakuja na style mpya ya wizi

Ingekuwa ni karatasi hata tano tu za mtihani wa kidato cha nne zimekamatwa nje, wangefuta mtihani wote hawa
 
Siasa za maji taka zipo CCM kuulawiti kuubaka kuunajisi uchaguzi ni siasa za maji taka
vp na wale wanaofukuza watu uanachama kisa wameenda bungeni? vp wale wanaochoma ofisi zao wenyewe alafu wanaita media? tunaziitaji izi siasa?? vp wale wanaosema kuna corona alafu wanafanya kampeni? ivi watoto wako wanajua unaitwa minyoo?
 
stay tuned.... muda si mrefu viraka vinarudi kwa kasi ya 5G....
 
Hofu yangu dozi ikikata halafu wahisani wakagoma kutuletea nyingine itakuwaje.Nawaza mambo mengi sana.Hahahahaaaaa
Kwa mawazo yako ARV zinasambazwa Mataifa ya Afrika free of charge eeeh?
 
Endelea kuabudu hiyo miungu yenu ngozi nyeupe. Tatizo mnafikiri Magufuli anatishiwa na kutishika na hizi sanaa zenu maana hamtaweza kufua dafu. Mpaka Magufuli anamaliza muda wake mtakuwa mmeanza kutafunana wenyewe. HAPANA KAZI TU
 
hatua kali kwa wavurugaji wa uchaguzi mataifa mbalimbali
Uchaguzi wake unamshinda mpaka Trump analalama na kura za 'posta', sasa ndiyo awe naudhubutu wa kuulizia yasiyomuhusu! Kama kuna aliowatuma kuja kutuvuruga ajue ameliwa hiyo ela!
 
Upumbavu,Upumbavu, Upumbavu, Upumbavu, Upumbavu.
Tulijua ni lazima watatoa Matamko. Hao ni wale wale Mabeberu waliotupeleka utumwani. Ndugu walifanywa vibaya sana na Majitu haya wakati wa Utumwa.
Matamko yao hayawezi kubadilisha matokeo.
 
View attachment 1618016


UINGEREZA YATAKA UCHUNGUZI HURU UFANYIKE KUHUSU UCHAGUZI WA TANZANIA

Kulingana na taarifa iliotolewa na Uingereza na kuchapishwa tarehe mosi mwezi Novemba, Taifa hilo sasa linajiunga na mataifa mengine katika kuitisha uchunguzi huru ufanywe ili kuondoa wasiwasi unaozidi kuenea katika taifa La Tanzania

Waziri wa masuala ya Afrika James Duddridge amesema kwamba Uingereza inashangazwa na ripoti za ghasia na kiwango cha juu cha maafisa wa polisi katika vituo vya kupigia kura ikiwemo suala zima la kukamatwa kwa baadhi ya viongozi wa upinzani.

Amesema kwamba Uingereza pia ina wasiwasi kuhusu madai ya kuingiliwa kwa uchaguzi huo, kujazwa kwa kura katika masanduku ya kupigia kura na kuzuiliwa kwa mawakala wa vyama vya upinzani kuingia katika vituo vya kupigia kura.

Vilevile taifa hilo limeshangazwa na madai ya ripoti za ghasia na kiwango kikubwa cha maafisa wa polisi katika vituo vya kupigia kura wakati wa uchaguzi, ikiwemo kukamatwa kwa baadhi ya viongozi wa upinzani.

Kulingana na taarifa hiyo , Uingereza imesema kwamba kwa Tanzania kuwa dhabiti na kustawi katika siku za usoni , itahitaji mchakato wa kidemokrasia ulio huru na wa haki, unaoungwa mkono na vyombo vya habari vilivyo huru.

Source: BBC
Wanasubiri wachina waje wawakingie kifua, hivi unaweza kuwaweka kando waingereza kwenye kuasisiwa kwa taifa letu na kutoa mchango mkubwa kwenye maendeleo baada ya hapo, huyo mchina alikuwa wapi?
 
Back
Top Bottom