View attachment 1618016
UINGEREZA YATAKA UCHUNGUZI HURU UFANYIKE KUHUSU UCHAGUZI WA TANZANIA
Kulingana na taarifa iliotolewa na Uingereza na kuchapishwa tarehe mosi mwezi Novemba, Taifa hilo sasa linajiunga na mataifa mengine katika kuitisha uchunguzi huru ufanywe ili kuondoa wasiwasi unaozidi kuenea katika taifa La Tanzania
Waziri wa masuala ya Afrika James Duddridge amesema kwamba Uingereza inashangazwa na ripoti za ghasia na kiwango cha juu cha maafisa wa polisi katika vituo vya kupigia kura ikiwemo suala zima la kukamatwa kwa baadhi ya viongozi wa upinzani.
Amesema kwamba Uingereza pia ina wasiwasi kuhusu madai ya kuingiliwa kwa uchaguzi huo, kujazwa kwa kura katika masanduku ya kupigia kura na kuzuiliwa kwa mawakala wa vyama vya upinzani kuingia katika vituo vya kupigia kura.
Vilevile taifa hilo limeshangazwa na madai ya ripoti za ghasia na kiwango kikubwa cha maafisa wa polisi katika vituo vya kupigia kura wakati wa uchaguzi, ikiwemo kukamatwa kwa baadhi ya viongozi wa upinzani.
Kulingana na taarifa hiyo , Uingereza imesema kwamba kwa Tanzania kuwa dhabiti na kustawi katika siku za usoni , itahitaji mchakato wa kidemokrasia ulio huru na wa haki, unaoungwa mkono na vyombo vya habari vilivyo huru.
Source: BBC