Security alert kwa Serikali yetu: Tuwe makini sana na Marekani, kuna kitu kinapangwa halafu wajifanye walionya kabla. Je, wanapanga kutu-Libya?

,Tuliwanyima wapinzani nafasi ya kusema ndani ya nchi wakatafuta wa kuwsemea nje ya nchi.Mlitaka kwa sababu mmewabana ndani ya nchi wafanyaje?
Kwa nini mnazusha!!! Ilisemwa kila mwanasiasa afanye siasa kwenye eneo lake la uwakilishi!!! Hapo uzuiaji unatoka wapi!?
 
Tafuta majibu mwenyewe!! No spoon feeding here, Mkuu. Ha ha haaa!
Zingatia kwamba,Mtanzania anao uhuru wa kuishi popote na kufanya chchote mradi havunji sheria za nchi.Sasa unaposema Eneo lake lazima uweke sawa eneo lake ni lipi?Huwezi kuchanganya Mikutano ya Wabunge na mikutano ya wanasiasa.Wanasiasa sio lazima wawe wabunge/madiwani.

Huwezi kuzuia Mwanasiasa ambaye pia ni Mbunge kushiriki katika shughuli kisiasa popte Tanzania kwa sababu tu yeye sio wa eneo hilo hio ni kinyume na katiba.Kwa ufupi Kauli hio ilitafsiriwa kama uminyaji wa uhuru wa watu ambao huo ndio ukweli wenyewe.
 
You are free but not to that extent

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wewe nae mtu mzima lazima lakini unaandika maujinga tu kila uchwao hapa jf.

Hivi huo uchumi wa kati mmeingia wewe na nani wakati maisha ya mtanzania kwa miaka minne au mitano yamezidi kuwa magumu.

Au viongozi wakiishi maisha mazuri kwa kuwalalalia walalahoi ndio mnaita uchumi wa kati ?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Acha lolote litokee .tutaanza moja kujenga taifa letu .tupigane tuuwane kisha tujirekebishe .nchi nyingi zenye viongozi wapumbavu zilipita huko na sisi lazima tupite
 
Hawa hawa na Magufuli wao wanakwambia serikali za majimbo zitaleta ubaguzi wakati wao wenyewe kabla hata ya uwepo wa hizo serikali za majimbo wameanza kutugawa kwa lazima tena.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Awamu ya tano kwa maamuzi ya JPM kutotoka nje ya Afrika ni sababu tosha ya wao kutomchukulia kama ni “rafiki” yao.

Awamu hii imefufua shirika la ndege na inataka liwe na ushawishi katika dunia, Marekani hawezi kuipenda hali hiyo kwani anahisi sehemu ya ushawishi wake itapungua.

Awamu hii inaufanyia kazi kwa vitendo ushauri wa Obama juu ya ushirikiano wa kikanda kiuchumi kuelekea ushirikiano wa Africa nzima, ushauri ni wa aliyekuwa rais wa Marekani lakini wale wazungu wenyewe hawapendi jambo hilo lifanikiwe.

Awamu hii inalinda rasilimali tulizonazo kwa vitendo, wazungu wanapenda wawe na maamuzi ya mwisho linapokuja suala la rasilimali za dunia nzima.

Wazungu wanapenda kunyenyekewa wakijidanganya kwamba wao kwa asili ni bora, JPM anayo natural pride ambayo hawawezi kuipenda.

Muhimu kwa Tanzania ni kwamba kabla ya uhuru hii nchi ilikabidhiwa kwa Mungu, hatukukurupuka tu kutaka kuwa nchi huru, Mungu alitangulizwa na Waislam pamoja na Wakristo.
 
Mkuu nimejaribu kusoma thread yako lakini nilipofika mstari namba 2, ambapo umeuita uchaguzi wa serikali za mitaa ambao ccm ilishinda kwa asilimia 99.9% ,kwamba ulikuwa Huru na Wa Haki! Ikabidi niishie hapo maana mauzauza yaliyofanyika kwenye ule uchaguzi hata wenyeviti wa ccm waliopitishwa bila kupingwa wanakiri walibebwa na dola, hivyo haingii akilini leo ukauita ni huru na wa haki!

Naipenda sana nchi yangu ya Tanzania, napenda sana kuona tunakuwa huru tena si uhuru tu wa bendera na mamlaka bali pia uhuru wa fikra!

Lakini tunapolazimishana kutawaliwa au kuongozwa na viongozi ambao hatukuwachagua, hapa pia uhuru wetu haupo, ni ukoloni chini ya wafrika na zaidi watanzania wenzetu walioshika dola!
Kitendo hiki ndicho kinavunja umoja wetu kama taifa, pia ndicho kinafanya mataifa mengine yaanze kutujadili na katika namna hii utengano wetu ndio unaoweza kutoa mwanya wa kuingiliwa kupitia ule upande ambao unakandamizwa!

Imagine kama katika kila chaguzi zetu kila chama kingeheshimu demokrasia na haki za wengine, kila mshindi akapatikana kihalali bila hujuma wala figisu, Ofcourse tungekuwa na umoja wa kihistoria! Tungekuwa mbali sana hata kimaendeleo, sababu pesa nyingi sasa hivi inatumika na chama tawala kuhakikisha tu kinasalia madarakani badala ya kupelekwa kwenye miradi ya maendeleo!

Kuna ushetani wa kila aina ndio maana mataifa makubwa kama Marekani wakijaribu kufumbua mdomo kidogo tu, tunaanza kuwa hofu, siku zote mtu asiyeishi katika haki, ukizungumzia haki ni kama unazungumzia mwisho wa maisha yake!

Hivyo basi wenye hofu na hizi kauli za wito wa Marekani lazima ni waovu na hawataki kujirudi!
 
Mbona ni Wasukuma tu tena wale wenye Njaa ndo wanaona mafanikio ya Msukuma mwenzao yaliyopatikana ndani ya miaka 5? Ni wao tu na maCCM ndo wamepewa macho ya paka ya kuona SGR imefika Morogoro kwetu tangu Novemba, 2019 na umeme wa Stiegler's wananchi wa Kibiti wanafaidi na Wasukuma wa Chato sasa wanasafiri kwa madege badala ya Musukuma Bus Service?

Sisi wa pembezoni tuna macho lakini mnayoyaona hatuyaoni hata kwa darubini tunayasikia tu toka kwenu, Njaa tunazo na teuzi tunatafuta lakini hatuteuliwi mnateuana hukohuko, tunaunga mkono juhudi miradi hatupati mnapata hukohuko ingawa kodi tunalipa, viwanda 4000 vya cherehani 4 vya Mwijage mnavyo hukohuko sisi bado tunavaa mitumba, mnaishi kama malaika sisi tunaendelea kuishi kama mashetani. Ahsante mpeni na kura mpeni sisi hatumpi ng'oo tunataka mabadiliko!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…