Security alert kwa Serikali yetu: Tuwe makini sana na Marekani, kuna kitu kinapangwa halafu wajifanye walionya kabla. Je, wanapanga kutu-Libya?

Security alert kwa Serikali yetu: Tuwe makini sana na Marekani, kuna kitu kinapangwa halafu wajifanye walionya kabla. Je, wanapanga kutu-Libya?

,Tuliwanyima wapinzani nafasi ya kusema ndani ya nchi wakatafuta wa kuwsemea nje ya nchi.Mlitaka kwa sababu mmewabana ndani ya nchi wafanyaje?
Kwa nini mnazusha!!! Ilisemwa kila mwanasiasa afanye siasa kwenye eneo lake la uwakilishi!!! Hapo uzuiaji unatoka wapi!?
 
Tafuta majibu mwenyewe!! No spoon feeding here, Mkuu. Ha ha haaa!
Zingatia kwamba,Mtanzania anao uhuru wa kuishi popote na kufanya chchote mradi havunji sheria za nchi.Sasa unaposema Eneo lake lazima uweke sawa eneo lake ni lipi?Huwezi kuchanganya Mikutano ya Wabunge na mikutano ya wanasiasa.Wanasiasa sio lazima wawe wabunge/madiwani.

Huwezi kuzuia Mwanasiasa ambaye pia ni Mbunge kushiriki katika shughuli kisiasa popte Tanzania kwa sababu tu yeye sio wa eneo hilo hio ni kinyume na katiba.Kwa ufupi Kauli hio ilitafsiriwa kama uminyaji wa uhuru wa watu ambao huo ndio ukweli wenyewe.
 
Kitu kimoja tu bila kujali chama tusiharibu amani na utulivu wa nchi tufanye siasa safi tushindane kwa hoja bila uadui ila sasa naomba walioko madarakani kuweka mfumo wa haki na uhuru wa kuongea haijalishi unapenda au hupendi kusikia watu wawe uhuru wa kuongea ila kuchochea kuvunja amani isikubalike. sasa sisi kauli zote za kupiga marufuku haki sio sawa mbaya zaidi ikifika wakati mtu hana imani na vyombo vya usalama au mahakama basi ishara mbaya sana ni lazima tuweke mahakama zetu huru kabisa ili sehemu ya kwenda kudai haki na ukishindwa basi uwe umeridhika kuwa haki imetendeka bila kuwa na vitu hivi sio usalama tu utakuwa hatarini hata uwekezaji hautakuja. uchaguzi ni suala lingine linahitaji tume huru 100% lakini hata baada ya uchaguzi system ya kimahakama iwe sehemu pekee ya mtu kukimbilia haki akiona amekosa sehemu ndio msingi bora wa amani.
You are free but not to that extent

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu andoza , ama kweli tuna watu wana macho lakini hawaoni, na masikio lakini hawasikii!, hivi maendeleo yote haya yanayofanyika na yaliyofikiwa hadi Tanzania kuingia nchi ya uchumi wa kati hautaoni?!.
Hebu panda gari pita Ubungo uone mambo!.
Uchaguzi 2020 - Je, Unaweza kupita Ubungo Interchange usiseme asante Magufuli? Mtakubaliana na mimi, asante stahiki ni kura zote kwa Magufuli
midege ile hujaona?
SGR?, Stigler?, etc, etc
P
Wewe nae mtu mzima lazima lakini unaandika maujinga tu kila uchwao hapa jf.

Hivi huo uchumi wa kati mmeingia wewe na nani wakati maisha ya mtanzania kwa miaka minne au mitano yamezidi kuwa magumu.

Au viongozi wakiishi maisha mazuri kwa kuwalalalia walalahoi ndio mnaita uchumi wa kati ?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wanabodi,

Hili ni bandiko la security alert lenye hoja 54 kati ya hoja hizo, hoja 33 ni maswali ya kiusalama kuhusu taifa letu Tanzania.

Angalizo Kuhusu Security Conscious
Ulinzi wa taifa sio jukumu la vyombo vya ulinzi na usalama pekee bali ni jukumu la kila Mtanzania Mzalendo wa taifa lake. Hakuna hujuma yoyote kama ugaidi, inaweza kupangwa na watu wa nje bila ushirikiano na watu wa ndani.

Security Conscious ni uwezo wa kuinusa hatari ya usalama wa taifa kwa mbali kabla haijatokea, hivyo hili ni bandiko la kizalendo la kutoa angalizo kwa vyombo vyetu vya ulinzi na usalama, kuwa kuna kitu hawa mabeberu wa Marekani wanakipanga kuhusu Tanzania kwa siku zijazo, sasa ili kukihalalisha, wanapenyeza watu wao kwa makini kabisa na very strategically kutafuta local collaborators ili muda muafaka wa kufanya yao ukifika, hao local collaborators ndio watatumiwa na kuonekana ni Watanzania wenyewe.

Mpango wenyewe uko hivi:
  1. Kuna mambo ya jinsi rais Magufuli anavyoendesha nchi, Wamarekani hawapendi.
  2. Wamarekani wanalazimisha modal yao ya demokrasia iwe ndio standard democratic modal kwa nchi zote, bila kuzingatia Tanzania tuna modal yetu ya demokrasia ambayo ni part of African Democracy, ambayo inaruhusu nchi ya vyama vingi, kufanya uchaguzi wa vyama vingi na chama kimoja kupata ushindi wa 99.9% na uchaguzi ukawa ni wa kidemokrasia, huru na wa haki kama ilivyo kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa. Wao mabeberu hawa wa Marekani hawataki kukubali hilo
  3. Kufuatia ushindi wa CCM wa kishindo cha asilimia 99.9% kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa, na sasa ndicho kinachokwenda kutokea kwenye uchaguzi Mkuu wa mwaka huu, ili hili lisitokee, Marekani itatumia fedha nyingi sana kufund political dissidents ili kuonyeshea dunia jinsi rais Magufuli anavyopingwa.
  4. Baada ya ushindi wa kishindo cha asilimia 90+% kwa rais Magufuli na CCM, kwa uchaguzi wa mwaka huu, kuna watu watapangwa kuleta chokochoko na vitendo vya kigaidi, hivyo kupitia mkataba wa ugaidi na Marekani, Marekani inaweza kuingia nchi yoyote kwa kisingizio cha kusaka magaidi ila lengo lao sio kusaka magaidi bali ku fund dissidents kum distabilize Magufuli.
  5. Pia Marekani inataka kulazimisha human rights records zake kuwa ndio standards records kitendo cha kumzui Makonda kuingia Marekani, mlengwa sio Makonda, Makonda ni chambo tuu, lengo ni kuichafua taswira ya nchi yetu kimataifa tuonekane tuna bad human rights records, wakati kiukweli Marekani ina worse human rights records kuliko sisi!.
  6. Katika utekelezaji wa nia hii ovu, Marekani kwa kutumia taasisi zake, imeanza kusambaza taarifa za uongo na uchochezi kwa kudai kuwa serikali ya rais Magufuli inaendeshwa kwa mfumo Kistu hivyo ku fund Muslim extremist na fundamentalists kuwa magaidi na kufanya vitendo vya kigaidi.
  7. Tayari baadhi ya Taasisi za Kimarekani zimeanza kuandika utabiri wa kuibuka kwa ugaidi Tanzania baada ya rais Magufuli kushinda.
  8. Mtanzania Mzalendo mwenye security conscious akisoma mahali na kubaini kuna kitu ambacho sio kizuri kinapangwa dhidi ya nchi yake, jukumu lake ni kusema tuu alichokisoma na anacho kiona.
  9. Ni jukumu la vyombo vyetu vya usalama, sio kuzingatia kila kinachosemwa mitandaoni kuhusu usalama wa taifa letu lakini pia wakisikia kitu sio kuzipuuzia.
  10. Mimi kama Mzalendo nimetimiza wajibu wangu, sasa niwapeleke kwenye makala yenyewe ya bandiko hili ambayo imetokana na bandiko hili la mwana jf dada yetu al maaruf kwa jina la Faiza Foxy USA yaendelea kuichimba Tanzania
  11. Hoja hizi 54, zenye maswali 33 ni maswali ya msingi sana, japo kuna hoja za urongo humu sio za kuzizingatia, lakini pia kuna hoja za ukweli, sio za kuzipuuzia
Jumatatu njema

Paskali
Acha lolote litokee .tutaanza moja kujenga taifa letu .tupigane tuuwane kisha tujirekebishe .nchi nyingi zenye viongozi wapumbavu zilipita huko na sisi lazima tupite
 
Zingatia kwamba,Mtanzania anao uhuru wa kuishi popote na kufanya chchote mradi havunji sheria za nchi.Sasa unaposema Eneo lake lazima uweke sawa eneo lake ni lipi?Huwezi kuchanganya Mikutano ya Wabunge na mikutano ya wanasiasa.Wanasiasa sio lazima wawe wabunge/madiwani.

Huwezi kuzuia Mwanasiasa ambaye pia ni Mbunge kushiriki katika shughuli kisiasa popte Tanzania kwa sababu tu yeye sio wa eneo hilo hio ni kinyume na katiba.Kwa ufupi Kauli hio ilitafsiriwa kama uminyaji wa uhuru wa watu ambao huo ndio ukweli wenyewe.
Hawa hawa na Magufuli wao wanakwambia serikali za majimbo zitaleta ubaguzi wakati wao wenyewe kabla hata ya uwepo wa hizo serikali za majimbo wameanza kutugawa kwa lazima tena.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Awamu ya tano kwa maamuzi ya JPM kutotoka nje ya Afrika ni sababu tosha ya wao kutomchukulia kama ni “rafiki” yao.

Awamu hii imefufua shirika la ndege na inataka liwe na ushawishi katika dunia, Marekani hawezi kuipenda hali hiyo kwani anahisi sehemu ya ushawishi wake itapungua.

Awamu hii inaufanyia kazi kwa vitendo ushauri wa Obama juu ya ushirikiano wa kikanda kiuchumi kuelekea ushirikiano wa Africa nzima, ushauri ni wa aliyekuwa rais wa Marekani lakini wale wazungu wenyewe hawapendi jambo hilo lifanikiwe.

Awamu hii inalinda rasilimali tulizonazo kwa vitendo, wazungu wanapenda wawe na maamuzi ya mwisho linapokuja suala la rasilimali za dunia nzima.

Wazungu wanapenda kunyenyekewa wakijidanganya kwamba wao kwa asili ni bora, JPM anayo natural pride ambayo hawawezi kuipenda.

Muhimu kwa Tanzania ni kwamba kabla ya uhuru hii nchi ilikabidhiwa kwa Mungu, hatukukurupuka tu kutaka kuwa nchi huru, Mungu alitangulizwa na Waislam pamoja na Wakristo.
 
Mkuu nimejaribu kusoma thread yako lakini nilipofika mstari namba 2, ambapo umeuita uchaguzi wa serikali za mitaa ambao ccm ilishinda kwa asilimia 99.9% ,kwamba ulikuwa Huru na Wa Haki! Ikabidi niishie hapo maana mauzauza yaliyofanyika kwenye ule uchaguzi hata wenyeviti wa ccm waliopitishwa bila kupingwa wanakiri walibebwa na dola, hivyo haingii akilini leo ukauita ni huru na wa haki!

Naipenda sana nchi yangu ya Tanzania, napenda sana kuona tunakuwa huru tena si uhuru tu wa bendera na mamlaka bali pia uhuru wa fikra!

Lakini tunapolazimishana kutawaliwa au kuongozwa na viongozi ambao hatukuwachagua, hapa pia uhuru wetu haupo, ni ukoloni chini ya wafrika na zaidi watanzania wenzetu walioshika dola!
Kitendo hiki ndicho kinavunja umoja wetu kama taifa, pia ndicho kinafanya mataifa mengine yaanze kutujadili na katika namna hii utengano wetu ndio unaoweza kutoa mwanya wa kuingiliwa kupitia ule upande ambao unakandamizwa!

Imagine kama katika kila chaguzi zetu kila chama kingeheshimu demokrasia na haki za wengine, kila mshindi akapatikana kihalali bila hujuma wala figisu, Ofcourse tungekuwa na umoja wa kihistoria! Tungekuwa mbali sana hata kimaendeleo, sababu pesa nyingi sasa hivi inatumika na chama tawala kuhakikisha tu kinasalia madarakani badala ya kupelekwa kwenye miradi ya maendeleo!

Kuna ushetani wa kila aina ndio maana mataifa makubwa kama Marekani wakijaribu kufumbua mdomo kidogo tu, tunaanza kuwa hofu, siku zote mtu asiyeishi katika haki, ukizungumzia haki ni kama unazungumzia mwisho wa maisha yake!

Hivyo basi wenye hofu na hizi kauli za wito wa Marekani lazima ni waovu na hawataki kujirudi!
 
Mkuu andoza , ama kweli tuna watu wana macho lakini hawaoni, na masikio lakini hawasikii!, hivi maendeleo yote haya yanayofanyika na yaliyofikiwa hadi Tanzania kuingia nchi ya uchumi wa kati hautaoni?!.
Hebu panda gari pita Ubungo uone mambo!.
Uchaguzi 2020 - Je, Unaweza kupita Ubungo Interchange usiseme asante Magufuli? Mtakubaliana na mimi, asante stahiki ni kura zote kwa Magufuli
midege ile hujaona?
SGR?, Stigler?, etc, etc
P
Mbona ni Wasukuma tu tena wale wenye Njaa ndo wanaona mafanikio ya Msukuma mwenzao yaliyopatikana ndani ya miaka 5? Ni wao tu na maCCM ndo wamepewa macho ya paka ya kuona SGR imefika Morogoro kwetu tangu Novemba, 2019 na umeme wa Stiegler's wananchi wa Kibiti wanafaidi na Wasukuma wa Chato sasa wanasafiri kwa madege badala ya Musukuma Bus Service?

Sisi wa pembezoni tuna macho lakini mnayoyaona hatuyaoni hata kwa darubini tunayasikia tu toka kwenu, Njaa tunazo na teuzi tunatafuta lakini hatuteuliwi mnateuana hukohuko, tunaunga mkono juhudi miradi hatupati mnapata hukohuko ingawa kodi tunalipa, viwanda 4000 vya cherehani 4 vya Mwijage mnavyo hukohuko sisi bado tunavaa mitumba, mnaishi kama malaika sisi tunaendelea kuishi kama mashetani. Ahsante mpeni na kura mpeni sisi hatumpi ng'oo tunataka mabadiliko!
 
Back
Top Bottom