Security alert kwa Serikali yetu: Tuwe makini sana na Marekani, kuna kitu kinapangwa halafu wajifanye walionya kabla. Je, wanapanga kutu-Libya?

Wapi walikopiga kura tuoneshe? Wapi watanzania walipiga hizo kura CCM ikapata kura 99.9%?
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Paschal nilikuwa nakuheshimu Sana ukiwa ITV. Ila kwa hizi Pumba unazoziandikaga humu kujifanya Politics and Security Expert Yani nakuona Zero brain. Eti uchaguzi wa serikali za mitaa ulikuwa wa kidemokrasia na CCM ikashinda 99.9%. Jamani hata Kama ndo njaa inakusumbua na kutafuta utezui at least reason kama a professional Journalist unajitia aibu na mabandiko yako yanayoonyesha wazi uko biase.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu Pasko,andiko lako ni refu sana ila nafikiri baadhi ya source zako pia nilishazisoma na nafikiri baadhi ya source ni waandishi wa habari,watafiti na wapelelezi.Kuhusu ukweli wa hoja zilizowekwa sidhani kama kuna mjadala hapo kwamba mambo waliyosema yanaendelea nchini ni kweli kwamba yapo au yametokea kuhusu ukweli wa mambo yatakayotukia nafikiri hilo linahitaji akili kubwa sana ili kuweza kutambua kama kuna ukweli ni pia muda utatuambia.

Ni kweli vijana wa kitanzania wengi sana wamejiunga na makundi ya kigaidi-militants na pia unaona kabisa kumbwa tuna wimbi kubwa la digital activists ambao kwa hakika kuna hatua itafia wataweza kutumika kutimiza kile unachohofia.

Binafsi sikubaliana na wewe kusema kwamba hili ni security issue,hapana hili in operational issue,ni suala tu la serikali kurekebisha mambo,kutenda haki na kuonesha nia kabisa ya kutaka kujenga umoja wa kitaifa.Usitake kuwasingiza wamarekani wakati ukweli ni kwamba wao hata kama wakitu-Libya kama unavyosema watatumia internal weakness zetu kuwezesha hilo.

najua bado Msemaji wa serikali hajateuliwa ila usijali.KAMA IPO,IPO TUUUU
 
Mbona uhoji wapi walipata silaha wale walimshambulia Mh Lissu ndani ya eneo ya eneo la bunge?.

Aiseeee... bora taifa lisambalatike tu.. watakao baki uenda wakazaa kizazi chenye haki.

Nope:
Naunga mkono marekani na washirika wake.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
True taifa lolote lenye umoja ni ngumu kulisambaratisha kosa kubwa alilofanya Gadaffi na saddam ni kutowaunganisha watu wao.Jiulize mbona Iran imeshindikana kuisambaratisha sababu ni moja.Taifa lolote lisilo na umoja haiitaji dakika kulisambaratisha je ni nani chanzo cha kuvunja umoja wetu?
 
ona ili nalo..
madini yamekuwaje?.
wakati wa tawala zingine Tanzania haikuwa na madini? kwanini hali hii iwe utawala huu tu?.

ebu nitajie kampuni hata moja tu ya Marekani inayojihusisha na madini Tanzania..

Mameee...
nipo tayali kuuza hata kuku wangu kumsapoti marekani.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Marekani inapaswa kuwachukulia hatua mapema wote wanaoashiria uvunjifu wa amani hii itaipunguzia dunia kuingia gharama za kuhudumia wakimbizi ni heri wachache waliokosa malezi bora wakaangamizwa ili ibaki salama.Kuna watu walitakiwa wabakie kuzimu wamsaidie ibilisi kazi na sio kuwaleta duniani kuwaumiza wengine Mungu alikosea sana
 
Elimu, Ujuaji kupitiliza tena kwa maslahi ya watu wachache hili ni tatizo kwa Taifa, Niwapongeze tu wale wote wanaoikosoa serikali hii ya awamu ya 5 maana wanatia chachu ya kile kinachoonekana kukosewa kiweze kurekebishwa na ili uwe sahihi lazima ukubali kukosolewa. Ni jukumu letu kwa pamoja kuweza kuilinda amani hii, Mungu atunusuru tusije ingia katika machafuko maana itakua ni anguko letu la amani ya kudumu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…