Sefue: Marufuku kutengeneza kadi za Christmas/Mwaka Mpya kwa gharama ya Serikali

Sefue: Marufuku kutengeneza kadi za Christmas/Mwaka Mpya kwa gharama ya Serikali

figganigga

JF-Expert Member
Joined
Oct 17, 2010
Posts
25,724
Reaction score
55,906
attachment.php
IMG-20151126-WA0013(1).jpg
 
Ni agizo lililotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi. Marufuku shirika, taasisi au Idara ya Serikali kuchapisha hizo kadi. Fedha zilizotengwa zitumike kupunguza madeni ya wizara, taasisi na idara. Anayetaka kuchapisha, ametakiwa afanye hivyo kwa gharama zake mwenyewe.
Chanzo: Taarifa ya Ikulu.
 
Katibu Mkuu Kiongozi , OMBENI SEFUE amepiga marufuku uchapishaji wa kadi za Krismasi na Mwaka Mpya kwa gharama za Serikali katika taasisi na idara za serikali.
Kadi hizo zilitumika kutakiana heri ya Krismasi na mwaka mpya kwa viongozi, taasisi na Idara za Serikali. SEFUE amesema atakaeona kuna umuhimu wa kuchapisha kadi hizo, basi achapishe kwa gharama zake mwenyewe.
Katibu Mkuu Kiongozi ameelekeza pesa za serikali zilizotengwa kwa ajili hiyo zitumike kupunguza madeni ambayo taasisi na Idara za serikali zinadaiwa au zifanye kazi nyingine.
 
Ikiwa ni takriban mwezi mmoja kabla ya sherehe za Krismasi na Mwaka mpya kuanza,Taarifa iliyotolewa na Ilkulu ni kuwa kuanzia sasa ni marufuku kuchapisha kadi za Krismasi na Mwaka mpya,kwa gharama za Serikali na badala yake anayetaka kuchapicha kadi hizo afanye hivyo kwa gharama zake binafsi,na pesa ambazo zingechapisha kadi hizo zitumike kulipia madeni ya wazabuni ,watoa huduma na watumishi wanaodai taasisi husika.
Kauli ya Ikulu imetolewa na KMK Balozi Ombeni Sefue leo tarehe 26/11/2015.
 
Siku tukikuta hizo hela mnazosema kuwa zilielekezwa
kwenye kazi nyingine zimepigwa na wajanja ndipo mtapojua
kiwango cha munkari wetu....
 
Siku tukikuta hizo hela mnazosema kuwa zilielekezwa
kwenye kazi nyingine zimepigwa na wajanja ndipo mtapojua
kiwango cha munkari wetu....

Mkuu fact ni moja, serikali haina hela za kugharamia hivyo vitu na haitaki kuingia madeni zaidi kwa ajili ya hivyo vitu. Miaka ya nyuma hela ingetafutwa hata kwa kukopa ili kadi zitengenezwe, ila kwa sasa hakuna kukopa kwa ajili ya vitu visivyokuwa natija kwa maendeleo ya taifa.

Na kama unavyojua tenda za serikali, kadi ya sh 2,000/- itachajiwa kwa sh 20,000/-, mi naona bora sana, tunakumbushana uwajibikaji.
 
Santeeee! Futeni kabisa Na hizi dini za watu weupe uislam/ukristo,Na serikali ianzishe dini mpya itakayoaminiwa Na watanzania wote.
Nalog off
 
Back
Top Bottom