Ikiwa ni takriban mwezi mmoja kabla ya sherehe za Krismasi na Mwaka mpya kuanza,Taarifa iliyotolewa na Ilkulu ni kuwa kuanzia sasa ni marufuku kuchapisha kadi za Krismasi na Mwaka mpya,kwa gharama za Serikali na badala yake anayetaka kuchapicha kadi hizo afanye hivyo kwa gharama zake binafsi,na pesa ambazo zingechapisha kadi hizo zitumike kulipia madeni ya wazabuni ,watoa huduma na watumishi wanaodai taasisi husika.
Kauli ya Ikulu imetolewa na KMK Balozi Ombeni Sefue leo tarehe 26/11/2015.