Mshangazi dot com
JF-Expert Member
- Nov 19, 2011
- 1,345
- 3,503
Afya ya akili kwa wanaume imekua tatizo linalokua kwa kasi sana na kusababisha matatizo na majanga ambayo tumekua tukiyasikia kila siku.
Naomba kuuliza wanaume mliopo JF:
Nauliza genuinely kwa sababu nataka kujifunza kama mama wa watoto wa kiume ambao watakuja kuishi kama wanaume kwenye jamii zetu siku za usoni.
Naomba kuuliza wanaume mliopo JF:
- Huwa unazungumza na nani kuhusu matatizo au changamoto binafsi ulizonazo?
- Je ukikwama kikazi, kibiashara, kimahusiano n.k, msaada huwa unapata wapi?
- Una mtu maishani ambaye unaweza kumwambia mambo yako ya ndani kwa uhuru bila kuogopa kuwa judged (kuhukumiwa au kuonekana ndivyo sivyo)?
- Una mambo au vitu unavyopenda kufanya wewe mwenyewe ambavyo vinakupa furaha?
- Unaamini kwenye kutafuta msaada wa kisaikolojia au kitabibu (therapy / couseling) pale utakapoelemewa au watu wakikishauri kufanya hivyo?
Nauliza genuinely kwa sababu nataka kujifunza kama mama wa watoto wa kiume ambao watakuja kuishi kama wanaume kwenye jamii zetu siku za usoni.