Sehemu salama ya mwanaume ni wapi?

Sehemu salama ya mwanaume ni wapi?

Asante, ngoja nikujibu mkuu
Hiyo sentensi yako ya mwisho inabeba majibu yote unayoyataka, kwa namna hizi;

1. Unamwonaje baba wa watoto wako..??

Namwona kama mtu muhimu sana na ambaye ni nguzo ya familia hasa kwa watoto wake.
2.Baba wa watoto wako, anazungumza na wewe kuhusu matatizo au changamoto alizonazo?
Ndiyo anazungumza na mimi, na tuna utaratibu wa kushirikishana na kuzungumza kuhusu yanayojiri.
3. Akikwama kikazi, kibiashara, kimahusiano n.k, baba wa watoto wako, msaada huwa anapata kwako?
Kwangu, kwa rafiki zake, kwa wazazi, kwa ndugu na kwa mwanasaikolojia wake.
4. Baba wa watoto wako, ana mtu maishani ambaye anaweza kumwambia mambo yake ya ndani kwa uhuru bila kuogopa kuwa judged (kuhukumiwa au kuonekana ndivyo sivyo)? AU huyo mtu ni wewe?
Ana marafiki wa karibu, ana dada na kaka zake pia yuko karibu na wazazi wake.
5. Baba wa watoto wako, ana mambo au vitu anavyopenda kufanya yeye mwenyewe ambavyo vinampa furaha?
Anapenda michezo, shughuli za kujitolea na kusafiri. Huwa anafanya peke yake na akijisikia kunialika basi ninafanya naye.
6. Baba watoto wako anaamini kwenye kutafuta msaada wa kisaikolojia au kitabibu (therapy / couseling) pale atakapoelemewa au watu wakimshauri kufanya hivyo?
Yuko kwenye therapy tayari anadeal na trauma za ujana wake jeshini.
 
Mwanamme anapata stress nyingi kama mfereji wa pesa ukikata....Ukiona Mwanamme analilia kisa kuchwa jua hana "MZIGO' na mwanamme mwenye mzigo aachwi.

KWINI MASANJA alimuacha TABIBU YEAR coz tayari alishajipata hana anachomtegemea tena.
Hakika
 
  1. Huwa unazungumza na nani kuhusu matatizo au changamoto binafsi ulizonazo?
  2. Je ukikwama kikazi, kibiashara, kimahusiano n.k, msaada huwa unapata wapi?
Yupo jamaa yangu mmoja ni binamu yangu amenizidi miaka mitano. Yeye ndio huwa namshirikisha mbanga kama hizi za biashara na mahusiano
Una mtu maishani ambaye unaweza kumwambia mambo yako ya ndani kwa uhuru bila kuogopa kuwa judged (kuhukumiwa au kuonekana ndivyo sivyo)?

Una mambo au vitu unavyopenda kufanya wewe mwenyewe ambavyo vinakupa furaha?
Nikiwa na mambo au vitu napenda kuzungumza na baba yangu mzazi. Yuko poa sana. Lakini pia napenda sana mazoezi binafsi na kucheza mpira inanifanya nijione bado niko alive.
Unaamini kwenye kutafuta msaada wa kisaikolojia au kitabibu (therapy / couseling) pale utakapoelemewa au watu wakikishauri kufanya hivyo?
Kuna kipindi nilipitia changamoto za kimahusiano nikatafuta mwana saikolojia tukashauriana mambo kadhaa maana nilikua naelekea kubaya.
 
Back
Top Bottom