Hiyo sentensi yako ya mwisho inabeba majibu yote unayoyataka, kwa namna hizi;
1. Unamwonaje baba wa watoto wako..??
2. Baba wa watoto wako, anazungumza na wewe kuhusu matatizo au changamoto alizonazo?
3. Akikwama kikazi, kibiashara, kimahusiano n.k, baba wa watoto wako, msaada huwa anapata kwako?
4. Baba wa watoto wako, ana mtu maishani ambaye anaweza kumwambia mambo yake ya ndani kwa uhuru bila kuogopa kuwa judged (kuhukumiwa au kuonekana ndivyo sivyo)? huyo mtu ni wewe?
5. Baba wa watoto wako, ana mambo au vitu anavyopenda kufanya yeye mwenyewe ambavyo vinampa furaha?
6. Baba watoto wako anaamini kwenye kutafuta msaada wa kisaikolojia au kitabibu (therapy / couseling) pale atakapoelemewa au watu wakimshauri kufanya hivyo?