Sehemu salama ya mwanaume ni wapi?

Sehemu salama ya mwanaume ni wapi?

Yakiwa mambo magumu ni bora kufa siwezi kulazimisha mambo kwa vile nimezaliwa kwa manufaa ya watu wengine sio maamuzi yangu.
Daah 🥹 basi tuombe mambo yasije kuwa magumu ukafikia huko.
Sad Feelings GIF.gif
 
Hakuna anaejali shida za mwanaume.. Wengi watasema ongea au tuelezee lakini mwisho wa siku utapewa pole na kutangazwa kuwa hujikazi kiume.

Huwa nawaambia watu, katika tembea tembea yako lazma utakutana na mtu msiri, mwenye hekima na sio judgemental. Watu wengi hatuwazingatii kwa sababu sio watu social lakini kama kuna watu wa kuwaamini ni wao hususani kama mkiwa marafiki mlioivana.

Zaidi ya hapo bora uje anonymously humu jf useme au la kama una mtu wa karibu ama baba share nae kuomba solution. Kuwaambia kina mama mara nyingi huwa wanateseka mara mbili, so huwa naepuka hilo
 
Hakuna anaejali shida za mwanaume.. Wengi watasema ongea au tuelezee lakini mwisho wa siku utapewa pole na kutangazwa kuwa hujikazi kiume.

Huwa nawaambia watu, katika tembea tembea yako lazma utakutana na mtu msiri, mwenye hekima na sio judgemental. Watu wengu hatuwazingatii kwa sababu sio watu social lakini kama kuna watu wa kuwaamini ni wao hususani kama mkiwa marafiki mlioivana.

Zaidi ya hapo bora uje anonymously humu jf useme au la kama una mtu wa karibu ama baba share nae kuomba solution. Kuwaambia kina mama mara nyingi huwa wanateseka mara mbili, so huwa naepuka hilo
Ukweli mchungu huu, Kuhusu kuto mwambia Maza hata mimi nakaaga kimya.

Maana ana weza Anza kuwaza au kuni uliza maswali like ime kuwaje kila saa.

Hata niki umwa huwa namwambia mie mzima, Kuna kipindi nili pelekwa hospital kwa lazima coz ali ona namdanganya.
 
Hiyo sentensi yako ya mwisho inabeba majibu yote unayoyataka, kwa namna hizi;

1. Unamwonaje baba wa watoto wako..??

2. Baba wa watoto wako, anazungumza na wewe kuhusu matatizo au changamoto alizonazo?

3. Akikwama kikazi, kibiashara, kimahusiano n.k, baba wa watoto wako, msaada huwa anapata kwako?

4. Baba wa watoto wako, ana mtu maishani ambaye anaweza kumwambia mambo yake ya ndani kwa uhuru bila kuogopa kuwa judged (kuhukumiwa au kuonekana ndivyo sivyo)? huyo mtu ni wewe?

5. Baba wa watoto wako, ana mambo au vitu anavyopenda kufanya yeye mwenyewe ambavyo vinampa furaha?

6. Baba watoto wako anaamini kwenye kutafuta msaada wa kisaikolojia au kitabibu (therapy / couseling) pale atakapoelemewa au watu wakimshauri kufanya hivyo?
Kiuhalisia wanawake wakikutwa na vitu hufikiria kwanza kubembelezwa kihisia "attention na maneno matamu" Ili kupoa. Wanaume kwa kiasi kikubwa hutafuta solution kwanza maana huwezi tafuta kubembelezwa na kuna watu wanakuyegemea hivyo wengi huifadhi mambo kifuani ama hukimbilia addiction kama pombe na sex. Pia kwa kiwango kiasi ni kuongea kwa sababu kiuhalisia hakuna anaemjali boy child

Ila huwa nawaambia watu, rafiki wa kumuamini hatafutwi Ila huwa anakuja katika mazingira flani. So ukimpata hata mmoja sio mbaya kumfungukia kiasi. Ila ukitegemea msaada wa kihisia kwa sehemu zingine. Bhasi uwe umebahatika sana
 
Ukweli mchungu huu, Kuhusu kuto mwambia Maza hata mimi nakaaga kimya.

Maana ana weza Anza kuwaza au kuni uliza maswali like ime kuwaje kila saa.

Hata niki umwa huwa namwambia mie mzima, Kuna kipindi nili pelekwa hospital kwa lazima coz ali ona namdanganya.
Yeah wamama huwa wanateseka mara mbili japo nao huwa wanaweza kujua kama haupo sawa kirahisi. Kwa hiyo unaweza muambia akuombee labda kuna jambo halipo sawa au la ukadogosha hilo jambo kiasi maana ukimpa ukweli wote. Utamtesa

Wamama huwa sensitive sana na kwa baadhi pia huwa hawakai na vitu. Unaweza muelezea, na yeye akawaelezea ndugu zako. Sometimes sio kwa umbeya au kwa ubaya Ila tu ni katika kukusaidia. Mwisho wa siku jambo linakuzwa kuliko uhalisia ama la unahisi kama umesalitiwa katika faragha yako
 
Kuna kipindi nili Anza kumpa ka kitengo fulani ka issue zangu, Sasa yeye aki ona vile zina enda ana ona I'm big as hell.

Si aka Anza kusema kwa ndugu na marafiki, kwamba huyu dogo ni 🔥 🔥 kilicho fata naki jua.
 
Sijafikia hatua hiyo, ila kuna wana mna share vitu vingi si mbaya kuongea nae, na kama vipi muhusishe mdingi wako, ama viongozi wa kidini.
Viongozi wa kidini wamekua wambea sana, stor yako ukiwapa inakuja kua shuhuda ama kifundishio kwenye ibada,
Na kama kuna anaewafahamu aibu unayo
Baba/mama baas ndo wanaoweza kuficha siri ama magumu ya mwanaume(mwanaye)
 
Kufanya mazoezi nayo ni namna mojawapo ya kurelease.

Mshauri hata akiwa mwanamke siyo shida, pale yupo kazini kwa kitu alichokisomea au kupata taaluma nacho so ana uwezo wa kukusaidia pia.
Mwanaume unakalisha kende 2 unamsikiliza mwanamke anakushairi wewe na mkeo, pipo tuwe siriaz
 
Mimi nimepitia majanga sana kiasi kwamba naonaga kila kitu ni Sawa tu.Nimekuwa kama gaidi au shehe au padri au katili ila kwa kadiri itakavyonijia.Nashukuru siwazi Wala kufikiria kujiua.NIMEKUWA SUGU.
 
Kuna hatari kubwa sana huko mbeleni, jinsia ya kiume imewekwa pembeni kwa kuona kwamba ilikuwa ni tatizo kwa jinsia ya kike nafikiri ni upotoshaji wa makusudi ulifanyika:

1. Mazingira yaliyotengenezwa hayamfanyi mwanaume kusema(wanakufa na tai shingoni)

2. Mwanamke katengenezewa mazingira ya kusikilizwa maeneo yote, na maeneo hayo hayo ndio mwanaume anakandamizwa

Hebu fikiri mwanaume anayepigwa na mke wake anaenda kusema wapi? mwanamke anatembea na mume wa mtu huwa anafanywaje, vipi kwa mwanaume anayetembea na mke wa mtu mazingira yako sawa?
 
Ukiwaeleza viongozi wa Dini jiandae matatizo yako kuja kusemwa madhabahuni kama mfano... Wale ndiyo Sina Imani nao kabisa..
Sidhani, sujawahi ona, labda kwakuwa mie sijawahi kumfata kiongozi wa dini.
 
Back
Top Bottom