Sioni sababu ya hoja yako. Kuna maeneo ambayo taasisi za dini zilipewa baada ya kuyaomba zijenge nyumba zao za ibada. Uwanja wa ndege siyo eneo la taasisi za dini kujenga nyumba za ibada. Kwa ndugu zetu Waislamu kuwa na chumba cha sala uwanja wa ndege, ni understandable kutokana na mfumo wao wa kuswali sala 5 kwa siku. Taasisi zingine za dini hazina shida na hitaji hili. Hivyo, hoja kwamba hizi taasisi zipewe vyumba vya kufanyia ibada zao uwanja wa ndege, naona haina mashiko kwa sababu mwisho wa siku uwanja wa ndege utageuka kuwa nyumba za ibada za taasisi za dini mbalimbali zilizoko nchini. Wahindu, Wakristo (ambao mahitaji yao katika nyumba zao za ibada ni tofauti pia), Waislamu, dini za asili, etc.1. Sehemu za Kuabudia Airport iwe takwa la Kisheria na sio hisani kama inavyofanyika sasa au kupendelea upande moja.
2. Laiti airport pangejengwa Kanisa tu sijui hali ingekuaje mpaka sasa.
NB: JNIA Terminal 3 wamejitahidi Ila wamesahau dini nyingine, kwanini? KERO.