Seifee Hospital walichukua namba yangu kunitumia matangazo yao, hii inanikera sana

Seifee Hospital walichukua namba yangu kunitumia matangazo yao, hii inanikera sana

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Joined
Feb 24, 2012
Posts
5,108
Reaction score
10,191
Niliwahi kutibiwa Seifee Hospital iliyoko mjini Dar es Salaam, inayopatikana ile njia kama unaenda Posta. Tangu nitibiwe pale wamekuwa wakinitumia matangazo ya madaktari wanaofika kwao. Hawa jamaa muda si mrefu nitawashtaki maana namba yangu ya simu ni taarifa binafsi na inapochukuliwa inapaswa kuchukuliwa kwa matumizi ninayoyahitaji tu sio kuanza kunitumia matangazo.

Seifee mtambu kuwa unapomtumia mtu ujumbe asiouhitaji mnakiuka haki zangu za kidigitali, lakini pia jumbe zenu hazina namna ya kujitoa ili mtu asipate meseji hizo. Naomba mtambue kuwa tayari Sheria ya Ulinzi wa taarifa binafsi imeshatungiwa kanuni, nitawazingua muda si mrefu.

Someni kifungu cha 35 cha Sheria ya Ulinzi wa Taarifa binafsi. Nimemaliza, endeleeni niwapeleke mnapostahili.

1714389274557.png
1714389287542.png
 
Back
Top Bottom