Sekondari za Vipaji maalum takribani miaka 40 tangu kuanzishwa kwake umaalum wake uko kwenye nini? Hatuoni ubunifu wowote

Hii trend ya wakina dotto magari na musukuma kudhalilisha wasomi ndio tumefika hapa. Mtu national exams std 7 kafeli, olevel kasoma makongo, 4 kapita kijanja tu kwa chabo, alevel kaenda kambangwa uko comb H nini nini sijui, halafu anataka kujiweka kwenye mzani sawa na kichwa cha PCM kutoka kibaha.
 
Hahah umenikumbusha Kambangwa ya pale Mwananyamala
 
Msalato Morogoro au ziko mbili
 
Nimependa hiyo sentensi watu wengi walioelimika wana ka-ustaarabu fulani....
 
Huko umeenda chini kabisa je umewahi kujiuliza SUA imekusaidia nini licha ya kuwa ni chuo kikubwa na cha muda mrefu hadi sasa? Je umenufaika nacho nini?
Unajua Taasisi nyingi za utafiti hapa nchini zinakabiliwa na changamoto lukuki. Mathalani ufinyu wa bajeti kwenye kufanya tafiti, maabara zenye vifaa vya uhakika(vinakidhi vigezo vya kimataifa), mfumo wa elimu ya chuo kikuu, Kujisimamia yenyewe na kujiendesha bila kutegemea fedha za serikali kuu na pressure ya nje(Political Influence), nimejaribu kuorodhesha baadhi.
 
Hao hawakuwa vipaji maalum bali wenye uwezo mkubwa wa Kukariri
 
Very Disappointing!
 
Sahihi mkuu lakini bado uwezo wa mtu [kipaji maalumu] sidhani kama unaweza kuathiliwa moja kwa moja na hizo sababu.

Angalia kuna watu wanasomea kayumba pamoja na changamoto zoote za kuyumba lakini wanatoa kuliko wa Ems.


Bado hao hao wanasoma kwenye vyuo kama SUA wanapotoka huko wanaanzisha salon akisubiri ajira Hapa tuseme tatizo ni nini?
 
Ni sahihi, lakini bado tunarudi pale pale Mtoto wa Simba akilelewa kama mbuzi, kuna namna tuu atakosa uwezo kama wale simba wa porini. Ni kwasababu amefugwa kwa mfumo tofauti. Ndicho kilichopo huku Tanzania. Unakuta mtu anapotential lakini mazingira yanambinya anashindwa ku-explore kile kilichopo ndani yake.
 
Nakubali mkuu
 
Huo ulikuwa usanii wa kaiwada. Uliza tuosoma nao vyuo vikuu tukwambie tulivyowapiga. Wengine, ukiwaona, unajiuliza vipaji vilikwenda wapi.
 
Wewe hutaki tu kukubali..
Wengi wao wako usalama wa taifa, wakiteka raia na kuwalinda viongozi..
Wengine wako mtandaoni kubishana na vizabizabina wanaoikashifu chukuwachakomapema...
Wengine wamesambazwa kwenye mashirika, taasisi muhimu za dola kuwasoma vizuri viongozi walafi na wasio wazalendo, watajifunza jinsi vigogo wanavyotafuna maliasili na rasilimali na kuandika ripoti wanavyokula kwa urefu wa kamba zao!
Waliobaki wameingizwa bongo flava, Sanaa, utalii, uchawa nk nk!
 
Kuna dogo m1 anamaliza A level mwaka huu. Hajapita huko vipaji. Alisoma hizi shule za English medium. O level alisoma pale st Joseph mwanga .
Huyu dogo unaambiwa hesabu anapataga alama 100.

Namtabiria makubwa mbeleni.
 
Hahhaah....we jamaa
 
Kuna dogo m1 anamaliza A level mwaka huu. Hajapita huko vipaji. Alisoma hizi shule za English medium. O level alisoma pale st Joseph mwanga .
Huyu dogo unaambiwa hesabu anapataga alama 100.

Namtabiria makubwa mbeleni.
Yuko vizuri anahitaji support atafika mbali
 
Huo ulikuwa usanii wa kaiwada. Uliza tuosoma nao vyuo vikuu tukwambie tulivyowapiga. Wengine, ukiwaona, unajiuliza vipaji vilikwenda wapi.
Hehehehe.....walikosa support kuunga mkono vipaji vyao. Kama Nchi tujitafakari
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…