Sekondari za Vipaji maalum takribani miaka 40 tangu kuanzishwa kwake umaalum wake uko kwenye nini? Hatuoni ubunifu wowote

Tatizo ni mazingira
 
Mkuu ume highlight mambo muhimu sana kwenye taasisi zetu za vyuo vikuu
 
Hizi shule maalum kweli zinapata wanafunzi wenye vipaji lakini hakuna facilities za kuendeleza hivyo vipaji. Pia zinapokea wanafunzi ambao utashangaa wamekujaje hapa kwenye shule maalum. Nimesoma Tabora Girls miaka sita masomo ya Arts, enzi hizo ndio mfumobwa jeshi unaishilia. Ni shule nzuri sana na wanafunzi wanajituma sana, lakini kama nilivyosema hakuna facilities na walimu wazuri wa kutosha.
 
Very Sad
 

Kuongezea.

Wengi wa hao Vijana ni Madoctors, Lectures, Engineers na wanamchango mzuri sana kwenye Taasisi na Jamii wanayo ifanyia kazi.

Tukumbuke, "Talents are equally distributed every where but opportunity is not" ndio maana Jami Forums & Twitter zilianzishwa zote 2006, Zikiwa na idea Moja lakini Twitter ikaenea dunia nzima lakini JF imeshindwa kuenea Hata EA, Hata Tanzania kuna watu hawaijui
 
 
Hao ndo wanakuendeshea maisha mkuu,

Wamejaa mawizara yote, wamejaa mataasisi yote makubwa,

Kama haujui Hao ndo muhimili wa watanzania, sio wote ila like 20% wanafanya vzr na wanazibeba saana taasisi wanazozifanyia kazi

Hajui kua hata Kama Mke wake anataka kujifungua kwa Operetion, Tayari Anakutana na Mikono ya Hao jamaa.

Kitu kimoja ambacho hakikosekanagi kwa hao watu ni Hard working.
 
Dah mtu unajisomea zako shule, Unafauru unapangiwa shule Ambayo walioanzisha waliita Vipaji maalumu bila nyenzo wezeshi, Unafaulu pia na kupata Viajira vyako na kutulia.

Halafa anakuja Mjinga Mmoja, Alie shindwa kufauru kama wewe Kukuhoji juu ya Matumizi Ya Elimu yako, Kama Yeye ndo alikusomesha.

By the way, Facebook iligunduliwa na University drop out What is your excuse boss? Au ndugu yetu hukupewa ubongo ufanye innivations kwa ajili yetu?

Au wewe innovations yako ni kuhoji watu wengine mafanikio yao?

Nyie ndo mkipewa nchi hii mnazani shida ni Wasomi, Kumbe shida ni sera mbovu ya Elimh
 
ELimu yetu kwenye nyanja za ubunifu na utafiti hatujawekeza vya kutosha, pia hatuna mikakati ya kuwatumia hawa vipanga kwa ajiri ya faida ya nchi. Mbaya zaidi siasa imepewa nguvu kubwa zaidi ya taaluma.
 
Hauna kipaji ,elewa maana ya kipaji ...Mjinga kwa wwe unaamini kupata ''A'' ni kipaji😅😅.

Kipaji ni asili sio kukaririshwa mshamba wewe ,unataka nyenzo wakati nyenzo kubwa ni akili ....Tesla , Einstein walisoma A masomo gani ?


Wewe unapata A kwenye mifumo ya watu ,akili za Wengine tumia akili kuleta vitu vipya ..
 

Sawa Sisi hatuna kipaji, Tumekariri shule.

Kwani Tesla na Eistein Walisoma shule gani zq Vipaji, Kipi kinakuzuia wewe Kufanya huo uvumbuvi?

Unaambiwa ulete hapa uvumbuzi wako, unaleta story za kukariri za Tesla na Eistein sasa tofauti yako na hao wanao kariri ni ipi.
 
We hauna kipaji wala impact yoyote ile ,hamna kipya kaa kwa kutulia ...Vipaji vipo ila sio wewe na wenzio 😅😅.

We si umesoma kipaji au ushakuwa tapeli ,lete uvumvlbuzi wako ! Ukariri hayo masomo sio kipaji😅
 
Mimi nilipata bahati ya kupita kielimu kwenye izo shule.

Kuna watu ni vipaji aisee kwenye kukremisha na ku paste kwenye MITIANI.

True education ni Ile inayo mwezesha mtu/ muhitimu kuyatawala mazingira yake na Maisha yake ki ujumla.

NB.
ELIMU NI KILE KITU KINACHO BAKIA KICHWANI MWA MTU BAADA YA KUHITIMU.
 
We hauna kipaji wala impact yoyote ile ,hamna kipya kaa kwa kutulia ...Vipaji vipo ila sio wewe na wenzio 😅😅.

We si umesoma kipaji au ushakuwa tapeli ,lete uvumvlbuzi wako ! Ukariri hayo masomo sio kipaji😅

We jamaa ghasia sana.

Mfupa umekushinda wewe unauutupia wenzio wautafune, uliona wapi.
 
Hakuna umaalumu wowote wengi tumesoma shule hizo hata ufundishaji wao ni wa kupiga msuli binafsi(kujisomea) vinginevyo utafeli
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…