Sekondari za Vipaji maalum takribani miaka 40 tangu kuanzishwa kwake umaalum wake uko kwenye nini? Hatuoni ubunifu wowote

Sekondari za Vipaji maalum takribani miaka 40 tangu kuanzishwa kwake umaalum wake uko kwenye nini? Hatuoni ubunifu wowote

Sahihi mkuu lakini bado uwezo wa mtu [kipaji maalumu] sidhani kama unaweza kuathiliwa moja kwa moja na hizo sababu.

Angalia kuna watu wanasomea kayumba pamoja na changamoto zoote za kuyumba lakini wanatoa kuliko wa Ems.

Bado hao hao wanasoma kwenye vyuo kama SUA wanapotoka huko wanaanzisha salon akisubiri ajira Hapa tuseme tatizo ni nini?
Tatizo ni mazingira
 
Unajua Taasisi nyingi za utafiti hapa nchini zinakabiliwa na changamoto lukuki. Mathalani ufinyu wa bajeti kwenye kufanya tafiti, maabara zenye vifaa vya uhakika(vinakidhi vigezo vya kimataifa), mfumo wa elimu ya chuo kikuu, Kujisimamia yenyewe na kujiendesha bila kutegemea fedha za serikali kuu na pressure ya nje(Political Influence), nimejaribu kuorodhesha baadhi.
Mkuu ume highlight mambo muhimu sana kwenye taasisi zetu za vyuo vikuu
 
Mimi o-level nimesoma azania, miaka ile ukisikia azaboy ujue hicho kichwa cha moto, na nina washkaji zangu wamepiga kibaha na mzumbe. Hawa wanafunzi wanaotoka shule za vipaji maalumu wale finest wengi wao huwa wanapata scholarship za kwenda nje, kutokana na uchumi wa bongo wa tia maji tia maji huwa wanaamua kufanya kazi na kuishi uko uko.

Kuna wengine huwa wanachukuliwa na mashirika ya kimataifa ndio maana hapa bongo huwa wanabaki wachache sana kiasi kwamba hatuoni impact yao. Halafu watu waliosoma wana ustaarabu fulani hivi kiasi kwamba hata akiwa anafanya mambo makubwa anakua humble tofauti na ambao hawajasoma wanakuaga na show-offs nyingi sana kwaiyo ni rahisi kuonekana. Ndio maana hawa wanaotoka vipaji maalumu wengi hatujui wako wapi na wanafanya nini.

Lakini wapo na wanafanya vizuri tu nina washkaji zangu nimesoma nao azania kuna mmoja daktari anaishi newcastle, uingereza. Mwingine lecturer wa compyuta sayansi anafundisha chuo ujerumani, mifano ipo mingi wengi wapo nje na kwenye mashirika ya kimataifa
Hizi shule maalum kweli zinapata wanafunzi wenye vipaji lakini hakuna facilities za kuendeleza hivyo vipaji. Pia zinapokea wanafunzi ambao utashangaa wamekujaje hapa kwenye shule maalum. Nimesoma Tabora Girls miaka sita masomo ya Arts, enzi hizo ndio mfumobwa jeshi unaishilia. Ni shule nzuri sana na wanafunzi wanajituma sana, lakini kama nilivyosema hakuna facilities na walimu wazuri wa kutosha.
 
Very Sad
 
Mada nzuri.
Kwa kuwa ume declear kuwa hukubahatika kuchaguliwa shule hizo basi moja kwa moja umekiri wengi huwajui na hujawahi wafuatilia.

BInafsi nawatambua vijana kadhaa waliopita shule hizo na wana mchango mkubwa kwa taifa katika nyanja mbalimbali.

Mfumo wa elimu zetu hazikutuwezesha kufanya gunduzi mbalimbali kwa sababu ya mazingira na vifaa. Lakini pia ugunduzi si mpaka urushe ndege. Matumizi sahii ya akili yako yanaweza kuleta matokeo chanya katika jamii.

Mfano juzi tumeona wanafunzi wa kibaha wakiwekeza mfumo wao wa kupiga kura kidigitali na kufanya uchaguzi.

Vipaji maalumu wengi walivyofika chuo wameendelea katika taaluma mbali mbali na pia wengi wapo na kampuni kadhaa....

Naweza kukutajia mbili tu. Anayeendesha AI ya kiswahili ni kipaji maalumu. Aliyeandika code za kampuni moja ya mawasiliano ni kipaji maalumu.

Nyerere ni kipaji maalumu n.k

Kwa namna ulivyotaja hao influencer wako ni dhahiri wewe ni mtu wa social media unayedanganywa na mafanikio ya picha.
Tatzo la watanzania wengi hudhania mafanikio ni hela nyingi au umaarufu.

Mimi nikuhakikishie tu. Kusanyiko la vilaza sio sawasawa na kusanyiko la vipaji maalumu. Kuna tofauti tu mtaonyesha kwenye kufikiri na kwenye kuamua.

Leo form 1 failure anaweza kutamba kuwa ana hela kuliko aliyesoma chuo. Lakini anasahau kuna watu behind walioweka mifumo imara inayofanya yeye apate hela.

Uvivu wa kufikiri unafanya tunakuwa na jamii isiyo na misingi imara na iliyokosa fikra timamu. Leo mtu mzima ana praise wauza uchi na machawa kuwa ndio wenye mafanikio. Huu ni ugonjwa wa akili.

Kuongezea.

Wengi wa hao Vijana ni Madoctors, Lectures, Engineers na wanamchango mzuri sana kwenye Taasisi na Jamii wanayo ifanyia kazi.

Tukumbuke, "Talents are equally distributed every where but opportunity is not" ndio maana Jami Forums & Twitter zilianzishwa zote 2006, Zikiwa na idea Moja lakini Twitter ikaenea dunia nzima lakini JF imeshindwa kuenea Hata EA, Hata Tanzania kuna watu hawaijui
 
Tatizo sio shule bali waliozianzisha ndio ambao akili zao zinatia mashaka .
Huwezi kuanzisha vipaji maalumu bila kulenga ugunduzi na teknolojia .
Tulitegemea pawe na shule za Vipaji maalumu zenye Maabara na workshop za ufundi na masuala ya ugunduzi na vipaji maalumu katika ubunifu na Computer.

Cha ajabu shule hizi ni za kukariri tu hesabu na sio vipaji vya ugunduzi . Wengi wao hawawezi hata kuchunga mwiko au hata kutengeneza jiko la mkaa achilia mbali Kutengeneza masufuria kama wazee wetu wa zamani .
Hata kufinyanga chungu hawawezi lakini wanauwezo wa kukariri na kupata alama A zote.

Shule za Vipaji maalumu zilitakiwa ziwe ni vipaji vya kuzaliwa na sio kukariri kama Koran tu.
Walitakiwa wapimwe kwa ujuzi usio wa kawaida na uelewa wa kuzaliwa kabla hata ya kuingia kwenye mitihani. Mfano mtoto mwenye uwezo wa kufanya hesabu ngumu kwa kichwa bila kuandika n.k.
Lakini hii ya ufaulu wa A haitatuletea Wagunduzi hata wa baiskeli achilia mbali Cherehani za Kidigitali.
[/QUOTE
Mbegu zote mpya zinatoka kwa Wazungu.
Sio kweli.

SUA wanazalisha mbegu nyingi tu, Shida hawana Marketting strategy kama chuo, Kinachofanyika ni kuuza huo uvumbuvi kwa makampuni ya Mbegu hapa Bongo
 
Hao ndo wanakuendeshea maisha mkuu,

Wamejaa mawizara yote, wamejaa mataasisi yote makubwa,

Kama haujui Hao ndo muhimili wa watanzania, sio wote ila like 20% wanafanya vzr na wanazibeba saana taasisi wanazozifanyia kazi

Hajui kua hata Kama Mke wake anataka kujifungua kwa Operetion, Tayari Anakutana na Mikono ya Hao jamaa.

Kitu kimoja ambacho hakikosekanagi kwa hao watu ni Hard working.
 
Kiufupi hamna kitu kipya ajira sio jambo jipya ,kwamba mna products kubwa zinatumika nchini

Acheni ushamba hamna kipya labda ajira ,mwenzenu Fernandez ana Nala nyie mna nn?

Kwenye utajiri na innovation hampo ,nyie mko wpi? Bado mna makamasi kichwani kuamini matokeo ya darasani.
Dah mtu unajisomea zako shule, Unafauru unapangiwa shule Ambayo walioanzisha waliita Vipaji maalumu bila nyenzo wezeshi, Unafaulu pia na kupata Viajira vyako na kutulia.

Halafa anakuja Mjinga Mmoja, Alie shindwa kufauru kama wewe Kukuhoji juu ya Matumizi Ya Elimu yako, Kama Yeye ndo alikusomesha.

By the way, Facebook iligunduliwa na University drop out What is your excuse boss? Au ndugu yetu hukupewa ubongo ufanye innivations kwa ajili yetu?

Au wewe innovations yako ni kuhoji watu wengine mafanikio yao?

Nyie ndo mkipewa nchi hii mnazani shida ni Wasomi, Kumbe shida ni sera mbovu ya Elimh
 
Hizi shule maalum kweli zinapata wanafunzi wenye vipaji lakini hakuna facilities za kuendeleza hivyo vipaji. Pia zinapokea wanafunzi ambao utashangaa wamekujaje hapa kwenye shule maalum. Nimesoma Tabora Girls miaka sita masomo ya Arts, enzi hizo ndio mfumobwa jeshi unaishilia. Ni shule nzuri sana na wanafunzi wanajituma sana, lakini kama nilivyosema hakuna facilities na walimu wazuri wa kutosha.
ELimu yetu kwenye nyanja za ubunifu na utafiti hatujawekeza vya kutosha, pia hatuna mikakati ya kuwatumia hawa vipanga kwa ajiri ya faida ya nchi. Mbaya zaidi siasa imepewa nguvu kubwa zaidi ya taaluma.
 
Dah mtu unajisomea zako shule, Unafauru unapangiwa shule Ambayo walioanzisha waliita Vipaji maalumu bila nyenzo wezeshi, Unafaulu pia na kupata Viajira vyako na kutulia.

Halafa anakuja Mjinga Mmoja, Alie shindwa kufauru kama wewe Kukuhoji juu ya Matumizi Ya Elimu yako, Kama Yeye ndo alikusomesha.

By the way, Facebook iligunduliwa na University drop out What is your excuse boss? Au ndugu yetu hukupewa ubongo ufanye innivations kwa ajili yetu?

Au wewe innovations yako ni kuhoji watu wengine mafanikio yao?

Nyie ndo mkipewa nchi hii mnazani shida ni Wasomi, Kumbe shida ni sera mbovu ya Elimh
Hauna kipaji ,elewa maana ya kipaji ...Mjinga kwa wwe unaamini kupata ''A'' ni kipaji😅😅.

Kipaji ni asili sio kukaririshwa mshamba wewe ,unataka nyenzo wakati nyenzo kubwa ni akili ....Tesla , Einstein walisoma A masomo gani ?

Wewe unapata A kwenye mifumo ya watu ,akili za Wengine tumia akili kuleta vitu vipya ..
 
Sawa Sisi hatuna kipaji, Tumekariri shule.

Kwani Tesla na Eistein Walisoma shule gani zq Vipaji, Kipi kinakuzuia wewe Kufanya huo uvumbuvi?

Unaambiwa ulete hapa uvumbuzi wako, unaleta story za kukariri za Tesla na Eistein sasa tofauti yako na hao wanao kariri ni ipi.
 
We hauna kipaji wala impact yoyote ile ,hamna kipya kaa kwa kutulia ...Vipaji vipo ila sio wewe na wenzio 😅😅.

We si umesoma kipaji au ushakuwa tapeli ,lete uvumvlbuzi wako ! Ukariri hayo masomo sio kipaji😅
 
Tumejionea wenyewe kule chini na mahala pengine kama ulaya Watoto wadogo wanaandaliwa kiwa Wanasayansi na mainjinia wabobezi. Watoto hao wanasukwa na kufinyangwa kiasi kwamba wanaanza kubuni na kuvumbua Mitambo na teknolojia za kipekee zenye mchango mkubwa ktk maendeleo ya kiuchumi kwenye nchi zao.

Hapa Tanzania mfumo wa Shule za Vipaji maalum umekuwepo kwa miaka mingi sasa.

Binafsi sikuwa na bahati ya Kujiunga na shule hizo hivyo nilitarajia pia kunufaika na Ubunifu/ innovations kutokana na kundi hili kubwa wenye vipaji Maalum/ special inteligence.

Tuna sekondari nyingi kama
1. Ilboru Arusha
2. Msalato Girls Morogoro
3.Mzumbe Boys Morogoro
4.Kibaha Boys Pwani
5. Tabora girls na Tabora Boys.

Ndio kusema Maelfu kwa Maelfu ya Wanafunzi waliopita humo hakuna hata wawili watatu walioonesha Ukipaji wao?

Tuseme basi Mtaji ni Mkubwa ku invest, hata Basi Kuwa Social influencer/ matumizi ya tech zilizopo je?

Tunaona Watu wenye elimu kiasi tu ndio wanaofaidi matumizi ya Technolojia na kunufaika na kuitangaza Tanzania.
Watu kama akina Maulid Kitenge, Kipanya, Zembwela, Diamond, Millard Ayo, Mwijaku, Baba Levo, Mobeto.

Angalau hawa hawakugundua chochote kama walivyo wale wa vipaji maalum ispokuwa wameweza kugundua matumizi sahihi ya teknolojia iliyopo.

Vipaji maalumu katika sekondari hizo ni vya mchongo au tunakwama Wapi?

Bonjour, Je M'apelle Bush Dokta habité à Makerere universite.

Bonvenué de discusio reun̈ion
Mimi nilipata bahati ya kupita kielimu kwenye izo shule.

Kuna watu ni vipaji aisee kwenye kukremisha na ku paste kwenye MITIANI.

True education ni Ile inayo mwezesha mtu/ muhitimu kuyatawala mazingira yake na Maisha yake ki ujumla.

NB.
ELIMU NI KILE KITU KINACHO BAKIA KICHWANI MWA MTU BAADA YA KUHITIMU.
 
We hauna kipaji wala impact yoyote ile ,hamna kipya kaa kwa kutulia ...Vipaji vipo ila sio wewe na wenzio 😅😅.

We si umesoma kipaji au ushakuwa tapeli ,lete uvumvlbuzi wako ! Ukariri hayo masomo sio kipaji😅

We jamaa ghasia sana.

Mfupa umekushinda wewe unauutupia wenzio wautafune, uliona wapi.
 
Hakuna umaalumu wowote wengi tumesoma shule hizo hata ufundishaji wao ni wa kupiga msuli binafsi(kujisomea) vinginevyo utafeli
 
Back
Top Bottom