Sekondari za Vipaji maalum takribani miaka 40 tangu kuanzishwa kwake umaalum wake uko kwenye nini? Hatuoni ubunifu wowote

Mkuu kiufupi hapa kwetu tz tuko kama mnyama mwenye vichwa pande zote mbili(mbele na nyuma:

Yaan hatueleweki hata kidogo hivi tunapo wakejili wasomi wa tz ktk field zao husasan hizi za science huwa tumerukwa na akili?.

Ni wapi sis na serikali yetu tumewahi kuwa na objectives za ugunduz?

Kama ni ndiyo hawa vijana wanaogundua vitu mbalimbali hapa nchini serikali imewandeleza kwa vitu gani au wanao mtaji wa kudevelop hizo ideas?.

Kama ni wataalam je, maghorafa ya hapa yanajengwa na akina nani, tuna tibiwa na akina nani hospatili, hizo matumbo, firigisi, mafuvu, skeleton, vibofu vikizingua vinachokonolewa na akina kama sio wasomi wetu?.

Sasa hii hulka ya kuwadharau wasomi kisa hawajagundua rockets waambieni serikali iweke madolari mezan uone kama vijana hawafanya maajabu, wanafikiri kwenye projects mbalimbali dunian hawamo wabongo?.
 
K
Kiukweli hata mimi sikupenda jamaa kuwatolea mfano wakina Mwijaku sijui Mobeto hao ni wakaa uchi mitandaoni hawapaswi kutolewa mfano kwenye mada yoyote inayohusu mambo ya msingi.
Sasa tukiendelea mbele na mada yetu katika mifano yako uliyoitoa bado hatujaona ugunduzi hapo kuendesha AI means AI tayari ilishagunduliwa na watu wengine wa nchi za mbali yeye anaitumia tu au sivyo hivyo?
 
Kwa mifano yako uliyoitoa hapo mwishoni bila shaka hujaelewa lengo la uzi.
Lecturer wa sayansi anafundisha chuo ujerumani-ana utofauti gani na lecturer wa UDSM?
Mwingine daktari anaishi New castle-ana utofauti gani na daktari wa Muhimbili?
Hapa lengo la uzi ni kujua wamefanya uvumbuzi gani wenye kuletq impact kwa jamii,hatuongelei kupata kazi ya kulipwa mshahara mkubwa au kukimbilia ulaya
 
Wewe unaweza kukariri? Au ukifikiria neno kukariri unachukulia rahisi?
Kila mtu akijiweka bize kwenye kukariri anaweza.
Kinachotofautiana ni mazingatio na kipaumbele katika muda huo husika.
Mwanafunzi mwingine utakuta kipaumbele chake ni michezo,mwingine kipaumbele chake ni kuangalia movies na mwingine kipaumbele chake ni kukesha na notsi kila siku hana muda na mambo mengine na hana muda na stori au kuongea na watu ndio hao mnawaita kipaji maalum.
 
Kwenye dunia ya sasa hakuna kipya utakachogundua bila ku associate na technolojia za awali.

Kutokana na elimu yetu na mitaala tunayopewa ambayo kwa asilimia kubwa tulirithi kutoka wakoloni ambayo inamuandaa mtu kuwa muajiriwa kuliko kuwa mtegemezi tegemea asilimia chache mno watatoka kwenye hiyo minyororo....

Elimu unayopata hapa Tz ni tofauti na waliotengeneza hiyo mitaala ..
 
Well noted.
Hapo kwenye mitaala nakubaliana na wewe.
So ilitakiwa viongozi washtuke waibomoe hiyo mitaala na kutengenezwa upya hii ndio solution.
 
Amesoma fizikia kwa habari niliowahi idoma mahala.
 
Asante kwa mfano mmojawapo hai. Wapo wengi sana wamelowea huko ughaibuni hawataki kurudi. Lakini wapo madaktari wengi bingwa nchini, Wahandisi, Wakufunzi na sector nyingi nchini wamesoma shule hizo. Watu wanaamua kuwachukulia poa tu
Watu wanataka UMAALUMU WAO kama walivyopewa status"SPECIAL". Kama ni utendaji tu wa kawaida hata wasioenda special school wanafanya.
China mwanafunzi akipewa hio status tegemea innovation za ajabu.
Kiujumla wanafanya vitu ambavyo haviwatofaitishi sana na wengine.
Sababu sio kwamba hawawezi kufanya vitu special ila wameathiriwa na mfumo.
Imagine Elon Musk angeamua kubaki SA je angeweza kufanya anayofanya ? Big no, Africa haisapoti ubunifu.
 
Huku kazini wote tunakula skeli moja ya mshahara, mtaala tulisoma wote sawa. Mabanda ya Physics na pure math wote tuliyapiga sana. Sasa umaalum wao uko wapi. Ongeza lingine wote tunatakiwa kwenda veta 🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣
 
Nafikiri aya ya mwisho ndio nilichokuwa nazungumza. Hapewi nafasi ya kufanya wanachoweza na ndio maana wengine wamebebwa ughaibuni na kutokomea huko
 
😅😅😅
 
That was the basis of my Thread
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…