Sekondari za Vipaji maalum takribani miaka 40 tangu kuanzishwa kwake umaalum wake uko kwenye nini? Hatuoni ubunifu wowote

Mimi nadhani umechangia wazo zuri tu hukuwa na haja ya kutukana watu.

Sasa hao wauza uchi na machawa ndio wanaoonekana. Hao unaodhani wana maana hatuwaoni. Sasa jamii ifanyeje?
Huyo muhandisi mzalendo kapuyanga sana, amedhiirisha kuwa hao wahitimu wa special schools ni wakawaida sana vichwani mwao, hili kuonesha uspecial wake hakutakiwa kabisa hata kuwafikiria hao machawa.

Huyo ilipaswa aje na Idea kwamba tutaweza vipi kufanya desalination kwa haya maji ya bahari ya Hindi hili tuweze kuyatumia majumbani kwetu tuache kutegemea maji ya mto Ruvu... halafu atwambie ni kiasi gani kinahitajika hili mimi nifund hiyo project😅😅
 
Ofcourse wote hawawezi kuwa wagunduzi. Lakini mpaka uzi umefik hapa hakuna hata mfanno mmoja uliotolewa.
Nimeona jamaa muhandisi mzalendo amekutajia PAWA AI aisee hiyo software hasa ya Sartify ni copy ya Chatgpt, alochojitahidi labda ni kugeuza lugha tu, na bado pia haiko effective kwenye data protection...na ndio maana hata bado haijulikani.

Kwa ufupi hakuna unique innovation yoyote hapa kwenye hiyo PAWA.
 
Wengi waliochaguliwa kwenye hizo shule za vipaji maalum walikuwa ni watu wenye uwezo wa kukariri masomo
Ndo sababu uvumbuzi hakuna
 
Atleast kwa kuanzia si mbaya
 
Huko umeenda chini kabisa je umewahi kujiuliza SUA imekusaidia nini licha ya kuwa ni chuo kikubwa na cha muda mrefu hadi sasa? Je umenufaika nacho nini?
Kuna nyakati fulani nilipata bingo la ufadhili wa miradi wa maendeleo la kaka $200k, ile pesa nilitaka nitenge nusu yake kisha nitafute graduates hata 50 kutoka SUA tufanye kilimo cha kisasa kabisa.. ila kuna mtu akaniambia niahairishe huo mpango
 
Walishauwa na sasa tuna tapatapa tu nchi haina think tanks
 
Niliwahi kusikia waligundua Namba ya Panya kugundua Magonjwa ya TB kwenye Sample za Makohozi. Hadi leo sijajua imefikia wapi ile project
Vipi na yule panya aliyekuwa anategua mabomu? Aliishia wapi?
 
Huwezi kukalili Physics,Hesabu na Chemistry. Huwezi kwani swali moja linaweza kuulizwa kwa style zaidi ya tatu. Hayo masomo huwezi kukalili.

Hiyo Chai na ili uweze kukalili lazima ujue sentence inamanisha nini, kama ndio hivyo basi hata kujifunza hizi lugha ingekuwa rahisi.

Hii ni chai unatupanga.
 
Na
Hao ndo wanakuendeshea maisha mkuu,

Wamejaa mawizara yote, wamejaa mataasisi yote makubwa,

Kama haujui Hao ndo muhimili wa watanzania, sio wote ila like 20% wanafanya vzr na wanazibeba saana taasisi wanazozifanyia kazi
Kama hao ndio wanatuendeshea maisha basi hizi shule za vipaji zifutwe, maana hakuna wizara au taasisi yenye ufanisi wa kuridhisha.. yaani zote tu ni ovyo, wanashindana kula rushwa tu na kufanya ufisadi.
 
Hahahhaa
 
Huyu hajasoma physics. HIlo dude linakiuka kanuni za kifizikia. Hilo dude halifai kuwa helicopter bali try cycle, liwekewe injini ya piki piki.
Waafrika wenye hamu ya kubuni hawajui fizikia na wanaojua fizikia hawana hamu ya kubuni kitu.
Na mnaojua fizikia ndio kama wewe hapa ambao haujawahi hata kutengeneza hata piki piki ya makoa.😂

Na hiyo fizikia kwanza mliisoma kuijibia mitihani tu hili mfaulu vizuri, halafu mwisho wa siku mje mle mashavu kwenye serikali ya ccm.
 
Hizo Innovation mnazani zinafanyiwa darasani? Hivi bajeti ya serikali yako kwenye vifaa za maabara za hizi shule ya serikali unaijua? Hivi Tanzania kuna research centers ngapi? Tanzania kuna library ngapi zinazo jitosheleza kwa vitabu?

Juzi tu hapa US Trump pamoja na maendeleo makubwa ya AI waliyo kuwa nayo ,ila kaweka zaidi ya USD bil 500,kwa ajili ya AI peke yako, wewe unazani kibongo bongo USD 500bil sawa na shillingi ngapi? Hapo bado hujaenda kuiona bajeti ya vitengo vingine kama Quantum Computer, Nuclear Physics, Cybersecurity,Maswala ya anga ?

Mnavyo ongelea gunduzi na Innovation mnazani zinakuja na kutokea kama Uyoga, research centers ya IBM ya maswala ya Quantum Computing, kujengwa gharama yake ni USD 5bil ,kama hamvijui hivi vitu bora mnyamaze.Hao madogo wenyewe final year project bajeti wanazopewa ni ndogo ,sometimes wanatumia mpaka hela yao ya bumu,tena unakuta kiproject hakizidi hata Tsh 1m.Youtube kuna story za gunduzi kibao na maswala ya Innovation fuatilieni ndipo mtaona ugumu wake.

Hayo matundu ya vyoo tuu yana tupelekesha,tena yanajengwa kwa msaada wa nchi za nje. Unapoona gunduzi au Innovation ya kitu chochote kaa ukijua billions of USD zimewekwa hapo, tena zaidi ya bajeti ya nchi yako.
 
Kuna nyakati fulani nilipata bingo la ufadhili wa miradi wa maendeleo la kaka $200k, ile pesa nilitaka nitenge nusu yake kisha nitafute graduates hata 50 kutoka SUA tufanye kilimo cha kisasa kabisa.. ila kuna mtu akaniambia niahairishe huo mpango
Huyo jamaa anakupenda sana.Mshukuru mno pale hakuna kitu mkuu Nina USHAHIDI wa kutosha kuhusu wahitimu wa pale.

Yupo niliekezwa na mzee kuwa niwe na mpigia ananipa ushauri wa kilimo maana ndo bwana kilimo wa kata Cha ajabu alipofika akaanza kushangaa Tena ikabidi nianze kumpa darasa
 
Kuna nyakati fulani nilipata bingo la ufadhili wa miradi wa maendeleo la kaka $200k, ile pesa nilitaka nitenge nusu yake kisha nitafute graduates hata 50 kutoka SUA tufanye kilimo cha kisasa kabisa.. ila kuna mtu akaniambia niahairishe huo mpango
Mwenzetu una connection nzito nzito
 
Kuna nyakati fulani nilipata bingo la ufadhili wa miradi wa maendeleo la kaka $200k, ile pesa nilitaka nitenge nusu yake kisha nitafute graduates hata 50 kutoka SUA tufanye kilimo cha kisasa kabisa.. ila kuna mtu akaniambia niahairishe huo mpango
Mkuu tueleze kwa kifupi kwanini uliachana na mpango huo?
 
Sio kwamba aliishangaa bali alikuwa anakupongeza kwa kuwa umefanya vizuri. Sasa wewe ukaanza kujiona una mzidi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…