SABABU KUU ZILIZOFANYA AJIRA ZA TRA KUSIMAMIWA NA WENYEWE
✅ Utumishi huzingatia tu ufaulu wa Written & Oral Interview. Mwenye Ufaulu mkubwa kapata kazi regadless his/her lack of taxation professional background
- Inasemekana kuna malalamiko kuwa watu hawana taaluma za kodi au zinazohusiana na kodi kiasi cha kuwapelekea kufanya vibaya kazini. Kwa ufaulu wao wa interview hausababishi wao kuwa wataalamu wa sheria za kodi na kuwahudumia walipa kodi ipasavyo. Hii huleta utendaji kazi m-baya na makosa mengi kazini wakati unakuta waliosomea sheria za kodi wanaachwa kisa tu walifaulu kidogo. Anachukuliwa mwenye Bachelor of agricultural business anaachwa mwenye bachelor ya taxation.
- Inasemekana wakufunzi wa hawa waajiriwa wa TRA wanapowapa Training waajiriwa wapya wanagundua wengi ni vilaza wa kodi kiasi cha wao kutumia nguvu kubwa ya kuanza kuwafundisha tena upya “What is taxation, How to compute tax, How many Tax acts & their implication”. Baada ya training huwa wanawapa mtihani kuwapima walichojifunza, kwa kiasi kikubwa hufeli huo mtihani sababu tu hawana good background za kodi.
✅ INASEMEKANA LAKINI Msiseme nimesema