Sekretarieti ya Ajira, kwanini mruhusu TRA kutangaza ajira zao? Naiona ile TRA ya makabila ikirudi kwa kasi

Sekretarieti ya Ajira, kwanini mruhusu TRA kutangaza ajira zao? Naiona ile TRA ya makabila ikirudi kwa kasi

Hapo watajazana watu wale wa chini ya kichuguu kilichochangamka kama ilivyo desturi yao.
Ni kihoro cha hovyo, siku hizi makabila yote yamesoma ingawa ukabila ni tofauti na mtu kuwa na kabila lake. Kuna makabila yana ukabila mengine hayana.
 
We ni dogo wa 2000s, hizi taasisi ambazo ni autonomous na semi-autonomous zimekuwa zikiajiri na hakuna hayo mnayoyawaza.
Wewe ambaye ni mkubwa, tuambie kwanini Serikali iliamua ku Centralize ajira zote zipitie Utumishi!?
 
Kwanini unafikiri ukabila tu, udini vipi. Kwani kamishna mkuu kabila gani. TRA yote ni kabila moja? Mambo mengine ni hisia tu.
Nadhani huelewi sababu za kwanini serikali iliamua ku centralize ajira PSRS.

Wewe unaye jiona mkubwa unafahamu nini kilitokea kipindi hizi Taasia zina ajiri zenyewe!?

Kama wewe ni wa juzi, fuatilia ukabila uluvyokuwa katika taasis hizi.

TPA
BIMA
TRA
BOT
......
 
SABABU KUU ZILIZOFANYA AJIRA ZA TRA KUSIMAMIWA NA WENYEWE
✅ Utumishi huzingatia tu ufaulu wa Written & Oral Interview. Mwenye Ufaulu mkubwa kapata kazi regadless his/her lack of taxation professional background
  • Inasemekana kuna malalamiko kuwa watu hawana taaluma za kodi au zinazohusiana na kodi kiasi cha kuwapelekea kufanya vibaya kazini. Kwa ufaulu wao wa interview hausababishi wao kuwa wataalamu wa sheria za kodi na kuwahudumia walipa kodi ipasavyo. Hii huleta utendaji kazi m-baya na makosa mengi kazini wakati unakuta waliosomea sheria za kodi wanaachwa kisa tu walifaulu kidogo. Anachukuliwa mwenye Bachelor of agricultural business anaachwa mwenye bachelor ya taxation.
  • Inasemekana wakufunzi wa hawa waajiriwa wa TRA wanapowapa Training waajiriwa wapya wanagundua wengi ni vilaza wa kodi kiasi cha wao kutumia nguvu kubwa ya kuanza kuwafundisha tena upya “What is taxation, How to compute tax, How many Tax acts & their implication”. Baada ya training huwa wanawapa mtihani kuwapima walichojifunza, kwa kiasi kikubwa hufeli huo mtihani sababu tu hawana good background za kodi.

✅ INASEMEKANA LAKINI Msiseme nimesema
Sio kweli.

UBINAFSI wa kutaka kubebana ndio kilichofanya TRA wajitoe PSRS.
 
Una hoja Mkuu.. Ila kama nakumbuka Mhe. Namba 1 aliwapa Kibali kwa madai kuwa walilalamika kucheleweshwa kwa mchakato wa kuwapata watumishi wapya
Suala sio uharaka walio nao hao wenyewe utashangaa inachukua mapaka miezi 4 watu hawajaitwa
 
Kwanza mfumo wao wa ajira TRA haupo sawa bado una mapungufu maana hata ukiangalia kuna baadhi ya kozi hazipo kwenye mfumo wao.
 
Kwanza mfumo wao wa ajira TRA haupo sawa bado una mapungufu maana hata ukiangalia kuna baadhi ya kozi hazipo kwenye mfumo wao.
Vijana wako strannded, mfumo unawasumbua sana, uko slow na sometime attachment zinagoma
 
Zamani nadra sana kumuona mwarabu au msomali katika utumishi lakini siku hizi wapo wengi
 
Una hoja Mkuu.. Ila kama nakumbuka Mhe. Namba 1 aliwapa Kibali kwa madai kuwa walilalamika kucheleweshwa kwa mchakato wa kuwapata watumishi wapya
Ila hii nahisi inaweza kuwa sababu..Mfano kuna kazi zilitangazwa na eGA tokea August 2024 ila hadi leo hawajaita interview ni miezi 6 sasa mchakato wa Ajira haujaisha. na kuna nyingi ambazo zinasubiri..kwa hili la TRA wangesimamia PSRS interview wangeita mwakan 2026 maana wako busy na Ajira za walimu
 
Back
Top Bottom