Sekretarieti ya Bunge: Kuna mapungufu katika Mkataba wa Bandari na DP World; ukomo wake uwekwe wazi

Sekretarieti ya Bunge: Kuna mapungufu katika Mkataba wa Bandari na DP World; ukomo wake uwekwe wazi

Kwa taarifa yako Gas Mtwara ulikuwa ujinga wa Europe na USA, na si unaona baada ya kupiga kelele mkataba haukufanyika ona Ntwara ilivyorudi nyuma. Tuliwaambia, na sasa hili la bandari mmeanza tena ujinga wenu. CCM inapendwa acha kabis.
Kwanini mtwambia na msiweke mambo wazi tuone wenyewe ?

Unaweza kuweka hapa hizo copy za mikataba kuanzia ya Gesi mpaka ya Bagamoyo ?, Au tuendelee tu kuamini sababu mnatwambia Yaliyomo Yamo ?
 
Kwanini mtwambia na msiweke mambo wazi tuone wenyewe ?

Unaweza kuweka hapa hizo copy za mikataba kuanzia ya Gesi mpaka ya Bagamoyo ?, Au tuendelee tu kuamini sababu mnatwambia Yaliyomo Yamo ?
Huyo anayejiita chawa wa Mama ni mpumbavu mmoja tu
 
hahaha huu sasa uchokozi, Faiza alishatoa darsa kuwa huu sio mkataba ni makubaliano tu
Na jerry Silaa alishasema Bungeni kwamba ni makubaliano then akaongea na waandishi wa habari kwamba ni mkataba.
Lakini hakuna makubaliano yanayoridhiwa na bunge, au siyo?
 
Tumelumbana weee, tumeelezana weee, Kuna wale vichwa maji wakajifanya wajuaji kuliko hata wajuaji wenyewe. Haya Sasa huu hapa Waraka wa bunge na kwa kifupi wamekubali kuwa....

1. Huu ni Mkataba, hakuna mahali wameandika Makubaliano kama akina Silaa (Mbunge) alivyowachanganya.

2. Wamekubali kuwa "hakuna ukomo" wa mkataba huo.

3. Wamekubali na kubaini kuwa "mkataba huo hauvunjiki".

4. Kuanza Kwa Early project activities kabla ya BUNGE kuweka baraka.

5. Shughuli za migogoro kufanyika South Africa, yaani mgogoro wowote.

6. Serikali kukosa "haki" ya kuvunja Mkataba, ni mkataba sio Makubaliano.

7. Hakuna muda wa mkataba.

8. Serikali KUZUIWA kuingia Makubaliano na MTU au taasisi yoyote kuhusu Bandari.

9. Serikali ya Dubai "kutokuonyesha" wazi nani Mwenye mamlaka ya kusaini

Hahahaha zile Simbilisi zije hapa Sasa! Mkataba wa kijinga kuwahi kutokea
Too late!! spana zipo pale pale msijisumbue kuleta spinning hapa! majizi wakubwa!
 
Na jerry Silaa alishasema Bungeni kwamba ni makubaliano then akaongea na waandishi wa habari kwamba ni mkataba.
Lakini hakuna makubaliano yanayoridhiwa na bunge, au siyo?
Ukiishi Tanzania ukafa Kwa stress utakua umejiua mwenyewe
 
Tumelumbana weee, tumeelezana weee, Kuna wale vichwa maji wakajifanya wajuaji kuliko hata wajuaji wenyewe. Haya Sasa huu hapa Waraka wa bunge na kwa kifupi wamekubali kuwa....

1. Huu ni Mkataba, hakuna mahali wameandika Makubaliano kama akina Silaa (Mbunge) alivyowachanganya.

2. Wamekubali kuwa "hakuna ukomo" wa mkataba huo.

3. Wamekubali na kubaini kuwa "mkataba huo hauvunjiki".

4. Kuanza Kwa Early project activities kabla ya BUNGE kuweka baraka.

5. Shughuli za migogoro kufanyika South Africa, yaani mgogoro wowote.

6. Serikali kukosa "haki" ya kuvunja Mkataba, ni mkataba sio Makubaliano.

7. Hakuna muda wa mkataba.

8. Serikali KUZUIWA kuingia Makubaliano na MTU au taasisi yoyote kuhusu Bandari.

9. Serikali ya Dubai "kutokuonyesha" wazi nani Mwenye mamlaka ya kusaini

Hahahaha zile Simbilisi zije hapa Sasa! Mkataba wa kijinga kuwahi kutokea
Kama hiki usemacho ni kweli tupu.basi Viongozi wote akiwemo Pm,Sipika ,ministers, and et Al walliodefend Mkataba ule waondoke ofisi za umma, waende wakachunge ng'ombe, kwani wao Nchi ni yao peke yao ??
 
UCHAMBUZI WA VIPENGELE VYA MAKUBALIANO BAINA YA SERIKALI YA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA NA SERIKALI YA DUBAI (INTERGOVERNMENTAL AGREEMENT – IGA) KWA AJILI YA USHIRIKIANO WA KUBORESHA, KUENDESHA NA KUENDELEZA MAENEO YA BANDARI NCHINI – JUNI 2023.

Soma hii Document
 

Attachments

UFAFANUZI WA HOJA ZILIZOJITOKEZA KUHUSU MAKUBALIANO BAINA YA SERIKALI YA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA NA SERIKALI YA DUBAI KWA AJILI YA KUBORESHA, KUENDESHA NA KUENDELEZA MAENEO YA BANDARI

Hizi hoja zote zinajibiwa hapa.
 

Attachments

View attachment 2698264


Kama kanuni zetu za kuingia mikataba zinasema mtu yeyote mwenye mamlaka ya sehemu husika anaweza sign mkataba kwa niaba ya Tanzania; kwanini tudhani ni tofauti upande wa Dubai.

Isitoshe hizo sign hazina nguvu yoyote za kimkataba isipokuwa ridhaa ya bunge tu. Sasa kwanini mtu akadhane na petty issues.

Mengine yote serikali imeshayatolea ufafanuzi wa kutosha; ambae ajaelewa mpaka sasa hataki kuelewa tu including hawa wanaojiita ‘sekretariat ya bunge’.

Hii ni salamu tosha kwa ‘Bi Tozo’ resistance iliyopo huko ndani katika vyombo vya serikali juu ya uongozi wake.

IGA aina shida yoyote, sasa labda inawezekana kuna mambo mengine ya ndani ambayo hatuyajui kuhusu huu mkataba ambao watu wanatumia nguvu sana kupotosha.

Pengine wamechoshwa na ufisadi mkubwa unaoendelea sehemu zingine hii IGA wanaitumia kama fimbo ya kumchapia tu.
Hizi hoja za wadau TLS,LHRC, prof shivv na wananchi ndizo shida kwenye (hivyo IGA ina shida)
 

Attachments

  • Capture+_2023-07-25-15-13-53.png
    Capture+_2023-07-25-15-13-53.png
    12.5 KB · Views: 1
Hizi hoja za wadau TLS,LHRC, prof shivv na wananchi ndizo shida kwenye (hivyo IGA ina shida)
Shida ya mkataba una justify kwa kuonyesha poor terms zilizopo sio porojo za hao watu. Hoja zao zote serikali imeshazijibu.
 
View attachment 2698310

Nakuwekea tena regulations/taratibu Tanzania iliyojiwekea kwenye kuingia Treaty. Sign sio muhimu sana na yeyote mwenye mamlaka anaweza sign.

Sasa ili kusema huko Dubai nani mwenye mamlaka ya kusaini na wenyewe ni kupitia taratibu zao walizojiwekea sio tunavyofikiri sisi kwa sababu kuna sign ya raisi na kwao lazima iwe ivyo.

View attachment 2698312

Kutokana na taratibu zetu kwa umuhimu wa process signatories, halafu baraza la mawaziri then ratification ya bunge.

Kwanini mtu aulize sign ya nani ipo au aipo wakati regulations zinakwambia ratification ndio hatua muhimu zaidi kushinda sign ya ipo kwenye mkataba. Ata Lissu kalielezea hili bunge ndio kila kitu hizo signs ni petty issues kisheria.

Sasa hiyo sekretariet kama sio kutaka kuleta tafrani ni nini na kujaribu ku contradict wanachoeleza serikali.

Hope ni nyaraka ya kutunga sio ya bunge; vinginevyo ‘Bi Tozo’ anatakiwa kutoka na kichwa cha mtu hapo. Kuna mambo mengine kiongozi anatakiwa kuto yavumilia kabisa moja wapo ni hilo la watu ambao anamamlaka ya kuwatumbua kwenda tofauti na agenda zake, ipo hivyo duniani sio Tanzania

Shida ya mkataba una justify kwa kuonyesha poor terms zilizopo sio porojo za hao watu. Hoja zao zote serikali imeshazijibu.
Kwa kusema hivyo mpaka leo ww hujaona poor terms kwenye huo mkataba wa IGA,na ktk muongozo Kipengele 4.6.1 (b) athari za masharti ya mkataba husika kwenye katiba ya nchi (e) athari za kisera na sheria za nchi tulizojiwekea na kupitishwa na bunge ikiwa vyesi kuendeshwa nchini, bado tu ww kwa muda unaochukua kuelewa jambo hujaona poor terms ...
 
Japo sio mwanasheria Nitajaribu kujibu kwa kuchangia Hoja ili tuelewane

Firstly Respond yangu ya swali ilitokana na kile ulichojibu wewe kwenye uzi huu kwa picha comments #256 kwa kusema bunge au kamati ya bunge halina Uwezo wa kurekebisha mkataba...

Naomba kukurekebisha kwa hapo kwa kusema Hiyo dhana sio kweli Kwa mujibu ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 Sura ya 3 ibara ya 63 (3) kifungu kidogo (e) ambayo huweza kusomwa pamoja na sheria Ya madaraka ya Bunge ya mwaka 1984 na 15 ibara ya 12. pamoja na Sheria ya namba 4 ya 1992 ib.17 na Sheria ya 1992 Na.20 ib.11

"Kwa madhumuni ya utekelezaji wa madaraka yake Bunge laweza kujadili na kuridhia mikataba yote inayohusu Jamhuri ya Muungano na ambayo kwa masharti yake inahitaji kuridhiwa".
katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (Sura 3 ib 63 (3e))


so ulichokisema hapo haukuwa sahihi.....

Labda niende kwenye Kanuni au Mwongozo na utaratibu wa kuridhia Mikataba ya Kimataifa ya mwaka 2017 Ambayo ndo ilikuwa hoja yako kuu...

jaribu kupitia Paragraph Ya Tatu ya utangulizi wa Mwongozo huo umeweka wazi kabisa kwamba maridhiano hayo hufanywa na kamati mbalimbali za Bunge...


Huenda kuna Tatizo linaweza kuja kuwa ni La Uelewa Wa hasa Majukumu ya lini hasa Bunge linakuwa Kamati ya Bunge na lini hasa Bunge linaweza kuwa kama Sekretarieti na lini hasa Bunge Huwa kaM bunge, Tujitahidi kizisoma sana sheria haziuzwi ziko Mtandaoni na nyingi ni free.

Ok Nitajaribu kuelezea hivi vitu vitatu,Bunge,Kamati ya Bunge na Sekretarieti Ya bunge...

Majibu yangu yanaweza yakawa marefu lakini Lengo ni kutoa Elimu

Ntaanza na Bunge

Ambapo bunge ni Mhimili au chombo kilichoanzishwa kwa Mujibu wa katiba ya Jamhuri ya Tanzania Ya mwaka 1977 Ibara ya 62 ndiyo inayoweka uwepo wa Bunge la Tanzania. Ibara ya 63 na 64 za Katiba hiyo zinalipa Bunge mamlaka na madaraka lililonalo. Hivyo basi, Muundo wa Bunge pamoja na majukumu yake vimewekwa bayana katika Katiba ya nchi.Ikiwemo hiyo ya kuchambua na Kuridhia mikataba na sheria...

Majukumu ya Bunge yametamkwa katika Ibara ya 63 (2) ya Katiba ya Nchi, Nitaquote

“Sehemu ya pili ya Bunge itakuwa ndicho chombo kikuu cha Jamhuri ya Muungano, ambacho kitakuwa na madaraka, kwa niaba ya Wananchi, ya kusimamia na kuishauri Serikali ya Muungano pamoja na vyombo vyake vyote katika utekelezaji wa majukumu yake “

Kamati Za Bunge..

Ibara ya 96 ya katiba ikisomwa pamoja na Sheria ya 1995 Na.12 Ibara 16 inalipa Bunge uwezo wa kuunda kamati za Bunge za namna mbali mbali kadri litakavyoona inafaa kwa ajili ya utekelezaji bora wa madaraka yake.
Ibara ya 89 inalipa Bunge mamlaka ya kutunga Kanuni za Kudumu kwa ajili ya kuweka utaratibu wa kutekeleza shughuli zake.

Sasa kwa mujibu wa kanuni za Bunge toleo la mwaka 2020 kuna Kamati Aina Tatu za Bunge kuna Kama ya bunge zima ,Kuna Kamati Teule na kuna Kamati za Kudumu...

Kuna kitu nataka ueleee hapa kabla kamati ya bunge zima haijakaa lazma kamati ndogondogo hizi zikae kujadili kwa kina hoja zake kwa mfano kabla halijajadiliwa swala la afya katika kamati ya Bunge zima lazma Kamati ya afya ya Bunge imekaa na imelijadili hilo Swala kabla ya kulipeleka Kamati ya Bunge zima kujadiliwa......

SASA TWENDE KWENYE SEKRETARIETI...

Sektretarieti Maana yake ni kwamba ni Mtu yoyote Au kikundi chchote kilichopewa mamlaka kisheria kuratibu utekelezaji wa shughuli fulani

kwa mujibu wa KANUNI ZA KUDUMU ZA BUNGE, TOLEO LA JUNI, 2020 sehemu ya 6 ibara ya 25

25.-(1) Bila ya kuathiri masharti ya Ibara ya 88 ya Katiba, Sheria ya Uendeshaji Bunge na Kanuni hizi kuhusu uwekaji wa nafasi na ngazi za utumishi, Ofisi ya Bunge itakuwa na Sekretarieti itakayoundwa na Idara, Sehemu na Vitengo mbalimbali kwa namna na idadi ambayo itaiwezesha kutoa huduma bora na kamilifu kwa Bunge, Wabunge na Kamati za Bunge.

(2) Katibu wa Bunge atakuwa Kiongozi wa Sekretarieti ya Bunge kwa mujibu wa Ibara ya 88(3) ya Katiba.
(3) Bila ya kuathiri masharti yaliyotangulia ya Kanuni hii, kutakuwa na Makatibu Wasaidizi wa Bunge, kwa idadi na ngazi mbalimbali kadri itakavyoamuliwa na Tume.

Tafsiri Katibu wa Bunge Akiwa kama Kiongozi wa sekretarieti ya Bunge nadhani tunaweza tukajua kwamba maamuzi ya Katibu wa Bunge hutoka Kw Spika wa Bunge kwani ndye Surbonate wake.....Yaani ndo Taswira yake kwa lugha nyepesi..

Kwahyo kwa kifupi ni kwamba Sekretariet,Bunge na Kamati za bunge ni KITU KIMOJA CHENYE MAJUKUMU TOFAUTI NA YENYE TASWIRA TOFAUTI ILA YENYE LENGO MOJA NA YALIYO NA BODI MOJA YA KIMAAMUZI...

Kwahiyo Sekretarieti ya Bunge haiwi na wabunge?

Elimu tafadhali na Shukrani kwa ufafanuzi huu murua
 
Kwa kusema hivyo mpaka leo ww hujaona poor terms kwenye huo mkataba wa IGA,na ktk muongozo Kipengele 4.6.1 (b) athari za masharti ya mkataba husika kwenye katiba ya nchi (e) athari za kisera na sheria za nchi tulizojiwekea na kupitishwa na bunge ikiwa vyesi kuendeshwa nchini, bado tu ww kwa muda unaochukua kuelewa jambo hujaona poor terms ...
Hakuna mwekezaji kupitia international law trade laws, business efficacy or just common sense atataka mgogoro wa uwekezaji utumie mahakama za nchi husika.

Hilo halipo duniani, hayo mambo watu wameshajifunza toka miaka 1950-60’s walipo nyan’ganywa uwekezaji kwenye mafuta na sera za nationalism.

Kwa hivyo kurudia rudia sheria hiyo sheria ya 2017 ni kupaka pili-pili kwenye kidonda tu; lakini kwa mtu yeyote timamu anajua hilo swala la mahakama za ndani kutatua migogoro halipo popote duniani kwenye uwekezaji wa kimataifa. There is always a neutral venue to settle disputes that’s standard.
 
Back
Top Bottom