The issue ambayo TLS na Profesa Shivji wamepoint out katika hii arbitration ya nje tena kwa sheria za nje ni kuwa:
IGA yenyewe inazungumza mambo mengi ambayo DP world inapaswa ipewe ambavyo viko governed na sheria za Tanzania kama vile Land rights, Vibali, Haki za wafanyakazi, Mambo ya mazingira and so forth. Kitendo cha kutafuta ar arbitration nje kwa sheria za Uingereza kutapelekea mgongano wa wazi kati ya sheria za Uingereza na Tanzania katika vitu hivyo. Ndiyo maana wanasheria wanasema huu mkataba kwa kiasi kikubwa unataka kumega sovereignity yetu.
Ili mkataba huu uweze kwenda smooth, itabidi tubadili sheria zetu zote zinazogusa ufanyaji kazi wa DP world nchini ziwe za uingereza la sivyo itakuwa ni confusion tupu.
Nimelitaja hilo hapo juu. That is a nuanced argument. This is what we need to focus on. Hizo nuance, si arbitration itafanyika wapi. Na hizo nuance wala hazipo katika arbitration clause. Zina clauses zake.
Kimsingi issue si arbitration kufanyika nje, that is a standard clause.
Issue ni, arbitration inafanyikaje nje? Hapo ndipo conflicts, kwa nfano, za land rights katika sheria ya Uingereza na Tanzania (article 21) zinatakiwa ziangaliwe na zielezewe vizuri kwenye mkataba.
Mfano, issue ya land rights imekuwa covered kwenye article 8 Land Rights, hii wala si issue ya arbitration clause. Ukiiandika hii article 8 vizuri kwamba usuluhushi ukifanyika popote, land rights zitafuata sheria za Tanzania, huna haja ya kuogopa arbitration ya nje kwa sababu ya sheria za land rights za Uingereza, kwa sababu arbitration hata ikifanyika Uingereza, kwenye migogoro ya land, arbitration itaangalia kwenye mkataba mlikubaliana nini? Kama mlikubaliana kuwa kwenye land rights sheria za Tanzania zitumike, arbitration haiwezi kwenda kinyume na mlivyokubaliana kwenye mkataba.
Sehemu nyingine wameandika jambo la kuangalia kwa umakini ni article 21 Governing Law IGA inakuwa governed na English Law, HGAs zinakuwa governed na Tanzanian Laws, hapa kuna potential ya conflict.
Tatizo article 21 iko so brief, vague and prone to argumentative interpretation.
IGA ina govern HGA, na IGA inakuwa governed na English law, lakini HGA inayokuwa governed na IGA (inayokuwa governed na English Law), iko governed na Tanzanian Law.
Unaona tatizo hapo?
Sasa, ukirekebisha hizo articles nyingine, articke 8 kama yenyewe tu arbitration kufanyika nje haina tatizo.
So, tuongelee huku kwingine kwenye matatizo, suala la arbitration kufanyika nje ni standard kabisa katika mikataba hii.