Kwani Mama anasemaje? Tutaondokanaje na huu mkataba wakati tumeishasaini na bunge limeishauridhia?Tumelumbana weee, tumeelezana weee, Kuna wale vichwa maji wakajifanya wajuaji kuliko hata wajuaji wenyewe. Haya Sasa huu hapa Waraka wa bunge na kwa kifupi wamekubali kuwa....
1. Huu ni Mkataba, hakuna mahali wameandika Makubaliano kama akina Silaa (Mbunge) alivyowachanganya
2. Wamekubali kuwa "hakuna ukomo" wa mkataba huo
3. Wamekubali na kubaini kuwa "mkataba huo hauvunjiki"
4. Kuanza Kwa Early project activities kabla ya BUNGE kuweka baraka
5. Shughuli za migogoro kufanyika South Africa, yaani mgogoro wowote
6. Serikali kukosa "haki" ya kuvunja Mkataba, ni mkataba sio Makubaliano
7. Hakuna muda wa mkataba
8. Serikali KUZUIWA kuingia Makubaliano na MTU au taasisi yoyote kuhusu Bandari
9. Serikali ya Dubai "kutokuonyesha" wazi nani Mwenye mamlaka ya kusaini
Hahahaha zile Simbilisi zije hapa Sasa! Mkataba wa kijinga kuwahi kutokea
Tukiuvunja itabidi tuwalipe $$$$ wakati hazina yetu imekauka.
Ok. Nimepata mwanga: tutawapa ngorongoro na longido yote.
Wale wamasai waliokaidi kuhamia msomera, sasa hivi watahama kwa lazima na viboko juu.
Hakuna kuwapakia kwenye mabasi wala nini. Watapiga lapa na mifugo yao hadi msomera.