Sekretarieti ya Maadili: Siyo kosa kwa kiongozi mwenye dhamana kuteua ndugu, jamaa au marafiki

Sekretarieti ya Maadili: Siyo kosa kwa kiongozi mwenye dhamana kuteua ndugu, jamaa au marafiki

Sawa naona hoja inatetewa kikamilifu..Vip kwa ule uteuzi ambao anapewa ndugu jamaa au rafiki ambeye tayari anawadhifa fulani halafu anaongezewa wadhifa mwingne yaani anakuwa na vyeo wiwili au vitatu huku wengine wakiambiwa ajira hakuna. Bwana sekretarieti hapo sheria inasemaje? mfano, ni mbunge niwazili ni mwenyekiti wa bodi ya kitufani.n.k
 
swali la msingi lilikuwa ni kwanini Tanzania tusifuate kanuni ya conflict of interest ya nchi za Skandvian na Nordic, kama Sweden, Norway, Denmark na Iceland, mtu ukiwa kiongozi wa taasisi yoyote, huruhusiwi kumteua ndugu yako yoyote au rafiki yako yoyote!. Rais hawezi kumteua mwenza, mtoto and ndugu, na ikitokea kuna rafiki ameomba nafasi fulani ya uteuzi, then rais ana delegate powers za uteuzi kwa mtu mwingine, to avoid conflict of interest.
Na jibu lilikuwa ni lipi?
 
Na jibu lilikuwa ni lipi?
Wameupokea ushauri, wataboresha sheria, itakuwa ukiwa rais, huwezi kumteua mwenza, mtoto au ndugu kwenye nafasi zako za uteuzi, na ikitokea mtu aliyepo anayekidhi sifa na vigezo ni mweza wako tuu, au mtoto au ndugu yako, una declare interest, unakasimu mamlaka ya uteuzi, ujapisha kidogo ndipo ateuliwe na wengine na sio wewe!.
P
 
SEKRETARIETI ya Maadili ya Viongozi wa Umma imesema siyo kosa kisheria kwa kiongozi mwenye dhamana kuteua ndugu, jamaa au marafiki kushika nafasi mbalimbali za uongozi.

Uteuzi huo hauwezi kuwa kosa kisheria iwapo utazingatia sifa za mtu anayeteuliwa, wamesema maofisa wa tume hiyo wakati wakizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki iliyopita.

Mkuu wa Kitengo cha Huduma za Sheria ndani ya sekretarieti hiyo, Emma Gerani aliwaambia wahariri kuwa kosa linaweza kuwepo iwapo uteuzi huo utafanywa kwa upendeleo.

MY TAKE

Mifumo ya Nchi ya Tanzania yote imeparalyse tangu 29.10.2025. Hakuna utawala bora wala Utawala wa Sheria.. Ni bora liende ifike 2030 turudi kwetu Oman kutumbua hela za Watanganyika

---
SEKRETARIETI ya Maadili ya Viongozi wa Umma imesema siyo kosa kisheria kwa kiongozi mwenye dhamana kuteua ndugu, jamaa au marafiki kushika nafasi mbalimbali za uongozi.

Uteuzi huo hauwezi kuwa kosa kisheria iwapo utazingatia sifa za mtu anayeteuli wa, wamesema maofisa wa tume hiyo wakati wakizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki iliyopita.

Mkuu wa Kitengo cha Huduma za Sheria ndani ya sekretarieti hiyo, Emma Gerani aliwaambia wahariri kuwa kosa linaweza kuwepo iwapo uteuzi huo utafanywa kwa upendeleo unaozingatia uhusiano kati ya mteuzi na mteuliwa.

Gerani alitoa ufafanuzi huo wakati akijibu swali lililoulizwa na mwandishi wa Pambazuko aliyetaka kujua sheria inasemaje kuhusiana na hatua ya baadhi ya viongozi wenye dhamana kuteua ndugu, jamaa na marafiki katika nafasi mbalimbali za uongozi.

Katika ufafanuzi wake, Gerani alisema kuwa watoto, ndugu, jamaa na marafiki wa viongozi
nao wana haki ya kushika nafasi za uongozi ikiwa wana sifa za kushika nafasi hizo.

Hivyo, alifafanua, iwapo watateuliwa kushika nafasi yoyote ya uongozi huku wakiwa na sifa, hata kama wana uhusiano wa kindugu na anayewateua, uteuzi wao hauna mawaa kisheria.

Mwandishi wa Pambazuko aliuliza swali hilo kufuatia malalamiko mitandaoni kuhusu baadhi ya viongozi wenye dhima kuteua ndugu na jamaa kushika nafasi mbalimbali za uongozi.

Aidha, kumekuwepo na malalamiko kuhusu watoto wa viongozi kupata kazi katika baadhi ya taasisi za umma.

Chanzo: Pambazuko

Pia soma
Nafikiri ufafanuzi huu ni muhimu kwa sababu unasaidia kutenganisha hisia na matakwa ya sheria. Tatizo si kuwa mtu ni ndugu, jamaa au rafiki wa kiongozi, bali ni kama ameteuliwa kwa kuzingatia sifa, uwezo na vigezo vinavyotakiwa. Ikiwa mtu ana sifa stahiki, haipaswi kunyimwa nafasi kwa sababu tu ana uhusiano na mteuzi. Hata hivyo, ili kuondoa mashaka ya upendeleo, ni muhimu uteuzi wowote uwe wa wazi, wenye kuzingatia merit na unaoweza kuwajibika mbele ya umma.
 
wataboresha sheria, itakuwa ukiwa rais, huwezi kumteua mwenza, mtoto au ndugu kwenye nafasi zako za uteuzi
Wanasubiri Samia arudi Kizimkazi. Sema ni vile viongozi wa Tanzania ni mbumbumbu na hawana aibu. Huwezi mpa mwanao kazi kwenye Ofisi za umma kwa kivuli cha cheo chako.

Hii roho ndo inafanya kutoona aibu kuua watoto wa wengine kwa risasi au njaa
 
Unamaanishisha chura ana IQ ndogo au??
Pale marekani,
mzee Donald Trump kumfanya mkwe wake kua muwakilishi wake maalumu huko mashariki ya kati ni kosa kwa sheria ipi kwamfano gentleman? Au kumfanya Trump JR kua miongoni mwa washauri wake kisioasa na kijamii, kosa liko wapi?

Au Rais Museven kumfanya mwanae kua mashauri wake wa masuala ya kiusalama na baadae kumfanya kua mkuu wa majeshi ya Uganda, kosa lipo wapi hapo?

DR.Mussein Ali Mwinyi, kua rais wa Zanzibar kama ilivyokua kwa baba yake hayati Ali Hassan Mwinyi makosa yapo wapi hapo?

Kosa la nafasi ya hayati Fidel Castro kurithiwa na Raul Castro mdogo wake ni lipi hapo kwa mfano?
Au Jorge Bush Sr, Rais mstaafu wa Marekani, na Mwanae Gorge Bush Jr pia kua rais kuna Tatizo hapo gentleman, ukiachilia mbali mambo yalivyo korea kaskazini na kwingineko ulimwenguni?

nadhani kuamini katika dhana iliyo potofu ni kitu mbaya sana :1Head:
 
Kidato cha nne ulipata division ngapi?,mwandiko mbaya na kujenga hoja hujui kwa kweli wafuasi wa CCM wajinga wajinga na nonsense
 
Kazi zingine, ukute wameambiwa wajitokeze kujibu hilo. 😁
 
Asanteni sana kwa mjadala huu muhimu na wa kuvutia! Ni kweli kwamba suala hili lina pande nyingi na linazua hisia tofauti miongoni mwa wananchi, na ni vizuri sana tunalijadili kwa uwazi.

Ni jambo la kufurahisha kuona tunajadili kwa kina masuala ya utawala bora na maadili katika uongozi wetu. Kauli ya Sekretarieti ya Maadili inatupa mwongozo wa kisheria, kwamba uteuzi ukizingatia sifa na uwezo wa mtu, hauwezi kuwa kosa la kisheria. Hii inasisitiza umuhimu wa sifa na uwezo wa mtu anayeteuliwa, bila kujali uhusiano wake.

Lakini pia siwezi kupuuza hoja za wengine, kama alivyosema denoo G, kwamba kuna desturi na matarajio ya jamii ambayo yanaweza kuonekana tofauti na tafsiri ya kisheria pekee. Ni muhimu sana kuendelea kujenga imani ya umma kwa kuonesha uwazi na kuepuka hata chembechembe za migongano ya maslahi. Kujali hisia za umma ni sehemu muhimu ya uongozi.

Kila mchango hapa unatukumbusha umuhimu wa kuendelea kudai uwajibikaji na kuhakikisha nafasi za umma zinawafikia wenye uwezo na sifa stahiki, iwe wana uhusiano na kiongozi au la. Tuendelee kujadili na kushauriana, kwa sababu lengo letu sote ni kuona nchi yetu inasonga mbele kwa misingi imara ya utawala bora na uwajibikaji. Mjadala kama huu unatusaidia sote kukua na kuelewa vizuri zaidi!
JF AI imeshakulemaza dadaake...tunataka mawazo yako sio ya AI
 
Wanasubiri Samia arudi Kizimkazi. Sema ni vile viongozi wa Tanzania ni mbumbumbu na hawana aibu. Huwezi mpa mwanao kazi kwenye Ofisi za umma kwa kivuli cha cheo chako.

Hii roho ndo inafanya kutoona aibu kuua watoto wa wengine kwa risasi au njaa
Tuhuma za nepotism zilipotolewa kwa yule Blaza wangu, nililishauri Bunge letu, Wito kwa Bunge letu tukufu: Mkithibisha hii Nepotism ya ajabu na zile Boeing ni TT, then hatufai!. hiyo niliyoiita nepotism ya ajabu, aliyeteuliwa ni mtoto tuu wa dada yeke na sio mwanae wa kumzaa mwenyewe!, hii ya mwana wa kumzaa mwenyewe kiukweli ni kubwa kuliko!.
Tena hapa issue sio tuu ni mwanae, bali alikuwepo bungeni miaka mitano, hakuchangia mada yoyote kwa miaka yote mitano!, hii tafsiri yake ni...., ni ....

P
 
Back
Top Bottom