Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 3,984
- 13,760
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma ni Taasisi inayojitegemea chini ya Ofisi ya Rais iliyoanzishwa kwa mujibu wa Ibara ya 132 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 kutekeleza Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma Na. 13 ya mwaka 1995.Jukumu kubwa la Taasisi hii ni kuchunguza tabia na mwenendo wa kiongozi wa umma yeyote kwa madhumuni ya kuhakikisha kwamba masharti ya Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma yanazingatiwa.
Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma imepeleka malalamiko kwenye Baraza la Maadili kuhusu tuhuma za ukiukwaji wa maadili kwa Kiongozi mmoja wa umma (1).
Kiongozi huyo ni Prof. Eliamini M. Sedoyeka ambaye ni Mkuu wa Chuo Taasisi ya Uhasibu Arusha (TAA).
Baraza hilo linatarajia kufanya kikao cha uchunguzi wa kina wa malalamiko hayo kwa mujibu wa kanuni ya 11 ya Kanuni za Maadili ya Viongozi wa Umma (Mwenendo wa Uchunguzi wa Malalamiko katika Baraza la Maadili), 2017.
Kikao hicho cha uchunguzi kitafanyika kuanzia saa 3:00 asubuhi tarehe 16 na 17 Mwezi Octoba, 2024 Jijini Dodoma katika ukumbi wa mikutano wa ofisi za Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma Mtaa wa TAMBUKARELI Makao Makuu DODOMA.
Uchunguzi huu wa wazi unafanyika kwa mujibu wa Kifungu cha 25 (5) na 29 (6) cha Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma.
Aidha, wananchi wote mnaalikwa kuhudhuria katika kikao hicho muhimu.
Jaji (Mst.) Sivangilwa S. Mwangesi
KAMISHNA WA MAADILI
15 Oktoba, 2024
Pia soma:KAMISHNA WA MAADILI
15 Oktoba, 2024
~ Prof. Eliamini Sedoyeka asomewa tuhuma nne kwenye Baraza la Maadili, azikana zote
~ Majibu ya Mkuu wa Chuo cha Uhasibu Arusha (IAA), Prof. Eliamini Sedoyeka mbele ya Baraza la Maadili