Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma yawasilisha malalamiko kuhusu Prof. Eliamini M. Sedoyeka

SEKRETARIETI YA MAADILI YA VIONGOZI WA UMMA

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma ni Taasisi inayojitegemea chini ya Ofisi ya Rais iliyoanzishwa kwa mujibu wa Ibara ya 132 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 kutekeleza Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma Na. 13 ya mwaka 1995.

Jukumu kubwa la Taasisi hii ni kuchunguza tabia na mwenendo wa kiongozi wa umma yeyote kwa madhumuni ya kuhakikisha kwamba masharti ya Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma yanazingatiwa.

Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma imepeleka malalamiko kwenye Baraza la Maadili kuhusu tuhuma za ukiukwaji wa maadili kwa Kiongozi mmoja wa umma (1).

Kiongozi huyo ni Prof. Eliamini M. Sedoyeka ambaye ni Mkuu wa Chuo Taasisi ya Uhasibu Arusha (TAA).

Baraza hilo linatarajia kufanya kikao cha uchunguzi wa kina wa malalamiko hayo kwa mujibu wa kanuni ya 11 ya Kanuni za Maadili ya Viongozi wa Umma (Mwenendo wa Uchunguzi wa Malalamiko katika Baraza la Maadili), 2017.

Kikao hicho cha uchunguzi kitafanyika kuanzia saa 3:00 asubuhi tarehe 16 na 17 Mwezi Octoba, 2024 Jijini Dodoma katika ukumbi wa mikutano wa ofisi za Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma Mtaa wa TAMBUKARELI Makao Makuu DODOMA.

Uchunguzi huu wa wazi unafanyika kwa mujibu wa Kifungu cha 25 (5) na 29 (6) cha Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma.

Aidha, wananchi wote mnaalikwa kuhudhuria katika kikao hicho muhimu.

Jaji (Mst.) Sivangilwa S. Mwangesi
KAMISHNA WA MAADILI
15 Oktoba, 2024​
Yule mwangalizi wa kibuyu chetu cha asali vipi au anaogopwa kwasababu ya zile tai anazovaa
 
15 Oktoba, 2024
Pia soma:
~
Prof. Eliamini Sedoyeka asomewa tuhuma nne kwenye Baraza la Maadili, azikana zote
~ Majibu ya Mkuu wa Chuo cha Uhasibu Arusha (IAA), Prof. Eliamini Sedoyeka mbele ya Baraza la Maadili
Wangeweka na tuhuma , hii habari imekaa kuunoko unoko
Tuhuma zake tayari amesomewa na mwenyewe amepata nafasi ya kujitetea.

Ingawaje kwa kiasi fulani amejitahidi kujibu baadhi ya hoja kwa usahihi, lakini bado kuna baadhi ya hoja ambazo anapaswa azitolee ufafanuzi wa kina zaidi, hususani kuhusu suala hili la Uhamisho wa Ndani wa huyo Mtumishi mwenye taaluma ya manunuzi kwenda Idara ya Maktaba.
1. Kama lengo lilikuwa ni kuongeza ufanisi kwenye Idara hiyo ya Maktaba, Je, ni kwa nini Mtumishi huyo aliyehamishwa hakupewa na Maainisho ya Majukumu yake Mapya (Job Descriptions mpya) wakati alipohamishiwa huko Maktaba??
2. Kwa kuwa Mtumishi huyo hakupewa New Job Descriptions, maana yake ni kwamba Majukumu yake yale yale ya awali aliyopangiwa na Mwajiri wake ndiyo anapaswa kuendelea nayo akiwa huko kwenye Idara mpya ya Maktaba alikohamishiwa. Sasa; Je, kwa nini Mtumishi huyo apangiwe majukumu mengine Mapya kabisa kinyume na taaluma yake aliyosomea na kinyume kabisa na majukumu yake ya awali ambayo alipangiwa na ambayo pia ndio sababu za Msingi zilizopelekea Mtumishi huyo kuajiriwa na hiyo taasisi? So Where is the purpose of Professionalism and Job Specialization for the Job-seekers or Employees?? Je, kulikuwa na sababu gani ya kumuajiri Mtumishi mwenye sifa hizo za taaluma ya Manunuzi wakati kazi zake au majukumu yake atakayopangiwa hayaendani na uhitaji wa taaluma hiyo?? Jambo hili ni kitendo cha hatari Sana endapo kama utalifanyia tathmini ya kina Sana.
Yaani Kama vile Utawala wa Hospitali ya Muhimbili Leo hii kwa kutumia njia za holela waamue kuwabadilishia majukumu ya kazi baadhi ya Madereva na kuwapangia Majukumu Mapya ya kazi za Udaktari wa Tiba ya Binadamu na kisha kuwaruhusu Madereva hao waanze kuingia kwenye Vyumba vya Upasuaji Wagonjwa ili waweze kuwafanyia Upasuaji (Surgery) wagonjwa wenye uhitaji wa huduma hiyo!
Ridiculous!
 
Back
Top Bottom