Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma yawasilisha malalamiko kuhusu Prof. Eliamini M. Sedoyeka

Yule mwangalizi wa kibuyu chetu cha asali vipi au anaogopwa kwasababu ya zile tai anazovaa
 
Wangeweka na tuhuma , hii habari imekaa kuunoko unoko
Tuhuma zake tayari amesomewa na mwenyewe amepata nafasi ya kujitetea.

Ingawaje kwa kiasi fulani amejitahidi kujibu baadhi ya hoja kwa usahihi, lakini bado kuna baadhi ya hoja ambazo anapaswa azitolee ufafanuzi wa kina zaidi, hususani kuhusu suala hili la Uhamisho wa Ndani wa huyo Mtumishi mwenye taaluma ya manunuzi kwenda Idara ya Maktaba.
1. Kama lengo lilikuwa ni kuongeza ufanisi kwenye Idara hiyo ya Maktaba, Je, ni kwa nini Mtumishi huyo aliyehamishwa hakupewa na Maainisho ya Majukumu yake Mapya (Job Descriptions mpya) wakati alipohamishiwa huko Maktaba??
2. Kwa kuwa Mtumishi huyo hakupewa New Job Descriptions, maana yake ni kwamba Majukumu yake yale yale ya awali aliyopangiwa na Mwajiri wake ndiyo anapaswa kuendelea nayo akiwa huko kwenye Idara mpya ya Maktaba alikohamishiwa. Sasa; Je, kwa nini Mtumishi huyo apangiwe majukumu mengine Mapya kabisa kinyume na taaluma yake aliyosomea na kinyume kabisa na majukumu yake ya awali ambayo alipangiwa na ambayo pia ndio sababu za Msingi zilizopelekea Mtumishi huyo kuajiriwa na hiyo taasisi? So Where is the purpose of Professionalism and Job Specialization for the Job-seekers or Employees?? Je, kulikuwa na sababu gani ya kumuajiri Mtumishi mwenye sifa hizo za taaluma ya Manunuzi wakati kazi zake au majukumu yake atakayopangiwa hayaendani na uhitaji wa taaluma hiyo?? Jambo hili ni kitendo cha hatari Sana endapo kama utalifanyia tathmini ya kina Sana.
Yaani Kama vile Utawala wa Hospitali ya Muhimbili Leo hii kwa kutumia njia za holela waamue kuwabadilishia majukumu ya kazi baadhi ya Madereva na kuwapangia Majukumu Mapya ya kazi za Udaktari wa Tiba ya Binadamu na kisha kuwaruhusu Madereva hao waanze kuingia kwenye Vyumba vya Upasuaji Wagonjwa ili waweze kuwafanyia Upasuaji (Surgery) wagonjwa wenye uhitaji wa huduma hiyo!
Ridiculous!
 
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…