Sawa zipo ila zinahitaji mtaji fulani au connection fulani, naomba utatajie aina mbili ya hizo kazi ambazo haxihitaji hata shilling moja, ondoa ya kilimo kwasbb ni gharama kuanzisha kilimo kwa namna yoyote.
1. Kufungua Kikundi cha Waigizaji hapo mtaani. Chukua simu, download app za Camera zenye HD inayoonyesha picha quality, andaa vipindi, fungua akaunti tiktok, YouTube, Facebook. Anza Kazi.
2. Fungua Kikundi cha vipaji na entrainment hapo mtaani. Kuimba, kuchora, kupigana au Mpira. Fanya yako
3. Fungua OFISI ya usimamizi wa Wasanii au Wana masumbwi. Weka Sheria, simamia. Nenda kwenye Bar, Club, Fukwe, matukio ya harusi, siasa n.k. piga hela.
4. Fungua OFISI ya Usafi. Fanya Usafi, UDOBI, kwenye nyumba za watu
5. Fungua Kikundi cha Wedding Maids ambao watacheza au kuhusika na mambo ya harusi, birthday, sherehe au shughuli za mazishi. Piga pesa.
6. Fungua OFISI ya Mapambo kwenye harusi, SHEREHE au birthday
Tafuta vijana wakukusaidia. Jipromoti.
Kuna sehemu wanakodisha Mapambo hivyo huna haja ya kuwaza mtaji.
Mtaji utaupata ukipata Advance kwenye SHEREHE.
Shughuli zote ziwe digitalised
7. Fungua OFISI ya kutia Sauti simulizi zilizoandikwa, kwenye vitabu. Ongea na Waandishi kama kina Taikon Wana Kazi, zitie Sauti.
Unahitaji uwe na simu, Maiki, na Mitandao ya kijamii kama YouTube.
Piga Kazi.
Shughuli hizi mtaji wake ni juhudi, ubunifu, na ustahimilivu wako.
8. Jifunze Kuogelea, nenda Coco Beach, tafuta kijana akufundishe.
Kisha jifue, ukipata pesa nenda, kule Mikocheni au pale Udsm wanafudisha sio gharama nyingi. Haizidi Laki Tatu.
Ukishajua, fungua akaunti mtandaoni, Instagram, tiktok, Facebook na YouTube.
Anza kupiga Kazi.
Jiite The Swimmer, au Swimming Trainer, au MkataMaji.
Nunua vifaa vya Kuogelea, na nguo Rasmi za kukutambulisha.
Huduma yako ilenge watu wa daraja la juu na Kati. Malipo yawe kwa mfumo wa Dollar.
9. Jifunze kulenga Shabaha, Fanya kwa miezi sita mfululizo. Hakikisha umemaster na ufanye kwa mitindo mingi na uwe na Shabaha kwa kiwango cha ajabu.
Nenda Mikocheni, kuna maeneo ya kujifunzia kulenga Shabaha.
Kwa sasa unaweza Anza na kupiga manati, upinde, mkuki, kisha bastola na bunduki
Haitazidi miezi sita utakuwa ushafuzu.
Kisha ingia mtandaoni jitangaze, nenda kwenye majeshi watakupa Nafasi ya kufundisha.
Watu binafsi ndani na nje ya nchi watakutafuta. Piga hela.
10. Jifunze Lugha za Alama. Jitangaze na andaa program za kibunifu piga hela.
Mambo yote haya hayaji kwa siku Moja. Inahitaji Nia, subira, Muda, Nidhamu, na commitment.