Sekta binafsi kufaidika na cheap skilled labour force kwa sababu ya ukosefu wa ajira nchini

Sekta binafsi kufaidika na cheap skilled labour force kwa sababu ya ukosefu wa ajira nchini

Hiyo pesa mi namlipa fundi ujenzi na kibarua wake kwa siku kwa tofali za kuuziana…, daah..

Vijana someeni taaluma kwanza za ufunddi stadi kisha ndio mkasomee rubber stamp jobs.., ili muwe na mbadala..
We jamaa we ni tajiri kwa standard za Tanzania, kulipa 90k kwa siku wewe ni trump hapa bongo, mtu ana degree mbili anapokea 15k kwa siku.
 
1. Kufungua Kikundi cha Waigizaji hapo mtaani. Chukua simu, download app za Camera zenye HD inayoonyesha picha quality, andaa vipindi, fungua akaunti tiktok, YouTube, Facebook. Anza Kazi.

2. Fungua Kikundi cha vipaji na entrainment hapo mtaani. Kuimba, kuchora, kupigana au Mpira. Fanya yako

3. Fungua OFISI ya usimamizi wa Wasanii au Wana masumbwi. Weka Sheria, simamia. Nenda kwenye Bar, Club, Fukwe, matukio ya harusi, siasa n.k. piga hela.

4. Fungua OFISI ya Usafi. Fanya Usafi, UDOBI, kwenye nyumba za watu

5. Fungua Kikundi cha Wedding Maids ambao watacheza au kuhusika na mambo ya harusi, birthday, sherehe au shughuli za mazishi. Piga pesa.

6. Fungua OFISI ya Mapambo kwenye harusi, SHEREHE au birthday
Tafuta vijana wakukusaidia. Jipromoti.
Kuna sehemu wanakodisha Mapambo hivyo huna haja ya kuwaza mtaji.
Mtaji utaupata ukipata Advance kwenye SHEREHE.
Shughuli zote ziwe digitalised

7. Fungua OFISI ya kutia Sauti simulizi zilizoandikwa, kwenye vitabu. Ongea na Waandishi kama kina Taikon Wana Kazi, zitie Sauti.
Unahitaji uwe na simu, Maiki, na Mitandao ya kijamii kama YouTube.
Piga Kazi.
Shughuli hizi mtaji wake ni juhudi, ubunifu, na ustahimilivu wako.

8. Jifunze Kuogelea, nenda Coco Beach, tafuta kijana akufundishe.
Kisha jifue, ukipata pesa nenda, kule Mikocheni au pale Udsm wanafudisha sio gharama nyingi. Haizidi Laki Tatu.
Ukishajua, fungua akaunti mtandaoni, Instagram, tiktok, Facebook na YouTube.
Anza kupiga Kazi.
Jiite The Swimmer, au Swimming Trainer, au MkataMaji.
Nunua vifaa vya Kuogelea, na nguo Rasmi za kukutambulisha.

Huduma yako ilenge watu wa daraja la juu na Kati. Malipo yawe kwa mfumo wa Dollar.

9. Jifunze kulenga Shabaha, Fanya kwa miezi sita mfululizo. Hakikisha umemaster na ufanye kwa mitindo mingi na uwe na Shabaha kwa kiwango cha ajabu.
Nenda Mikocheni, kuna maeneo ya kujifunzia kulenga Shabaha.
Kwa sasa unaweza Anza na kupiga manati, upinde, mkuki, kisha bastola na bunduki
Haitazidi miezi sita utakuwa ushafuzu.

Kisha ingia mtandaoni jitangaze, nenda kwenye majeshi watakupa Nafasi ya kufundisha.
Watu binafsi ndani na nje ya nchi watakutafuta. Piga hela.

10. Jifunze Lugha za Alama. Jitangaze na andaa program za kibunifu piga hela.

Mambo yote haya hayaji kwa siku Moja. Inahitaji Nia, subira, Muda, Nidhamu, na commitment.
Fafanua vizuri lugha ya alama
 
We jamaa we ni tajiri kwa standard za Tanzania, kulipa 90k kwa siku wewe ni trump hapa bongo, mtu ana degree mbili anapokea 15k kwa siku.
Sasa kama anajenga tofali nyingi kama roboti utaachaje kumlipa na mmeshakubaliana kwamba utamlipa kwa tofali alizojenga…
 
Ila kazi za wenye ujuzi wa veta ajira zinapatikana au ni yale yale tu.
Hali sio mbaya kama Hizi za vyuo vikuu, Ukienda leo Metl pale utakuta Anaeendesha Konecrane, Forklift, Fundi umeme magari etc analipwa Mshahara mara 2 ama 3 zaidi ya mhasibu ama HR.

Kuna kazi ukiwa vizuri Automatic watu wana kutafuta tu, ila kuna kazi kila mtu anafanya, interview mpaka zifanyike Uwanja wa Taifa ama Diamond Jubilee na mlivyo wengi mnavunja milango
 
Kulipa ada sio issue ila unalipia hiyo ada kwa kusoma kozi gani? Mtoto anasoma HKL Advance unalipia ada yake 3m anaenda chuo anasoma B.A tourism, huo ni ignorance na utumiaji vibaya pesa yako utakuja kujutia bure.
Mbona tourism....sio siri hii course graduates wake ni mayatima wa ajira..nafsi zake wakitangaza zikizidi sana 8 ..huko Tanapa na Game reserve wamejaa wildlife na ndugu zao ..sielewi walifikiria nn kuanzisha course hii wakati hawaajiri na most of them wanaochakarika na kufanikiwa na corse hii ni wa kutoka kanda ya kaskazini ambao wana konekshen huko huko ... degree graduate wa SUA na certifacate ya Musoma utalii hawana tofauti kwenye soko la ajira vinginevyo utaishia online seller.. content creator muuza vyombo na nguo,winga kariakoo... kwa wanawake ukiolewa ubaki nyumbani kulea watoto maana huna ramani..Hii course nyoko kabisa
 
Hata serikali ni wanufaika wa hizo cheap labour. Mfano walimu wanaoitwa "wa kujitolea" haswa wa masomo ya sayansi ni sababu ya serikali kutokuona umuhimu wa kuwaajiri walimu wa kutosha.
 
Hata serikali ni wanufaika wa hizo cheap labour. Mfano walimu wanaoitwa "wa kujitolea" haswa wa masomo ya sayansi ni sababu ya serikali kutokuona umuhimu wa kuwaajiri walimu wa kutosha.
Hiyo policy sio rasmi inafanywa tu na walimu wakuu wajanjawajanja hamna kitu kama kujitolea katika sera za serikali za elimu.
 
U
Hali sio mbaya kama Hizi za vyuo vikuu, Ukienda leo Metl pale utakuta Anaeendesha Konecrane, Forklift, Fundi umeme magari etc analipwa Mshahara mara 2 ama 3 zaidi ya mhasibu ama HR.

Kuna kazi ukiwa vizuri Automatic watu wana kutafuta tu, ila kuna kazi kila mtu anafanya, interview mpaka zifanyike Uwanja wa Taifa ama Diamond Jubilee na mlivyo wengi mnavunja milango
Umesema kweli, TIJA ni muhimu sanaa katika kila kazi. Si Cheti tuu. Nadhani hata ile standard ya kufundisha vyuo vikuuu lazima uwe na 3.8 GPA itakuja kufutika kwa sababu kuna watu wapo kitaa wanauwezo wa kufanya mambo makubwa sanaa na wana ufaulu wa kawaida
 
Sasa huo ni unyoonyaji kwa upande wa serikali, wananyima watu ajira kwa malengo ya kuwapa hizo temporary permite za ufundishaji.
Waraka wa elimu namba 3 wa mwaka 2016 unawatambua vizuri tu. Na wanalipwa ujira mdogo kwa michango ya wazazi. Hivyo sio propaganda za wakuu wa shule.
 
Law of Supply and Demand, huwezi kumpangia muajiri akulipe ngapi wakati wako wenzio kama wewe wapo tayari kwa chochote
 
Back
Top Bottom