Sekta Binafsi ni Nyezo muhimu katika kuibua Mipango mbalimbali ikiwemo fursa za Fedha

Sekta Binafsi ni Nyezo muhimu katika kuibua Mipango mbalimbali ikiwemo fursa za Fedha

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2020
Posts
2,833
Reaction score
1,301

SEKTA BINAFSI NI NYENZO KATIKA KUIBUA MIPANGO NA FURSA ZA KIFEDHA

Waziri wa Uwekezaji, Viwanda na Biashara, Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb.) amesema ushiriki wa sekta binafsi chini ya ubia kati ya serikali ni nyezo muhimu katika kuibua mipango mbalimbali ikiwemo fursa za fedha za kugharamia uwekezaji.

Dkt. Kijaji ameyasema hayo Mei 5, 2023 Bungeni jijini Dodoma wakati wa kuhitimisha hotuba ya makadirio ya mapato na matumizi kwa Wizara ya zaidi ya Sh bilioni 119.018 na kati ya hizo Sh 43.566 zimetengwa kwa ajili ya matumizi ya maendeleo ambapo Sh bilioni 30.347 ni fedha za ndani na Sh bilioni 13.22 ni fedha za nje yaliyopotishwa na Bunge kwa kauli moja

Amesema sekta binafsi ni nyenzo muhimu katika kuibua mipango mbalimbali ikiwamo fursa za fedha za kugharamia uwekezaji, uendelezaji na uanzishwaji wa viwanda. biashara, masoko na viwanda vidogo.

Aidha, Dkt. Kijaji ametoa rai kwa wabunge kuhakikisha wanashiriki katika kuwahahamsiaha watanzania kufahamu sera, mikakati na fursa mbalimbali zilizopo ili wazichangamkie na hivyo kuweze kutoa mchango unaohitajika na kunufaika nao ka maendeleo na ustawi wa kila mmoja na taifa kwa ujumla.

Pia amewashukuru waheshimiwa wabunge kwa hoja na michango yao ambayo inaonesha nia dhabiti ya kuziendeleza sekta ya uwekezaji, viwanda na biashara na kusukuma mbele gurudumu la maendeleo ya taifa.

“Kwa ujumla hoja na michango mingi iliyotolewa na kamati ya Kudumu ya Bunge ya Viwanda, Biashara, Kilimo na Mifugo na waheshimiwa wabunge zimelenga maeneo mbalimbali ambayo yamelenga kupiga hatua katika maeneo ya uwekezaji, viwanda na biashara.
 

Attachments

  • FvZQdwfXwAEWh5_.jpg
    FvZQdwfXwAEWh5_.jpg
    136.8 KB · Views: 3
  • FvZQdwdWAAIodIE.jpg
    FvZQdwdWAAIodIE.jpg
    152.8 KB · Views: 2
Back
Top Bottom