ChoiceVariable
JF-Expert Member
- May 23, 2017
- 66,537
- 75,687
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Mimi Huwa naona magofu ya Viwanda vingi tulivyojenga wakati wa Ujamaa vimekufa,ila kwenye zama za umimi Kuna wengine waliuziwa viwanda vya Nyerere wakavibbadilisha kuwa Godowns.Sasa hao uliowataja wewe umeona walisimamia sera za Kijamaa? Hao wote walisimamia ubapari ndio uchumi ulifanya vizuri lakini akina John na Julius ni Bure kabisa
Kwani Bandari za Dubai zinaendeshwa na nani kama siyo serikali!Kuna bandari zaidi ya tatu zinakwenda kupata waendeshaji wapya, na kote huko mikataba ni mibovu?. Profesa Shinji kaingiza chaka watanzania wengi kwa kudai mkataba hauna ukomo wakati ukomo unakuwepo kwenye mikataba ya biashara.
Unakuja wakati wa nchi kufaidika na bandari zetu kwa kuleta waendeshaji wenye uwezo na wenye CV zinazojitosheleza, ule wakati wa kuatamia mali zetu huku tukiendelea kusota kwa umaskini umeshapita.
Kwani Bandari za Dubai zinaendeshwa na nani kama siyo serikali!
Walishajipanga miaka na miaka wakati sisi huku tunapiga siasa na kuendekeza ufisadi wa kila aina.Kwani Bandari za Dubai zinaendeshwa na nani kama siyo serikali!
Ujamaa unapotea kwa kasi sana duniani. Elimu zinazofundishwa mashuleni kwa sasa ni zile zenye kuweka msisitizo kwenye kumuwezesha mwanafunzi kuwa mbunifu na mtundu. Ni elimu inayokwenda na dunia ya uvumbuzi kuliko ile ya kufundisha masuala yale yale ya kijamaa.Mimi Huwa naona magofu ya Viwanda vingi tulivyojenga wakati wa Ujamaa vimekufa,ila kwenye zama za umimi Kuna wengine waliuziwa viwanda vya Nyerere wakavibbadilisha kuwa Godowns.
Wakati wa Mjamaa Magufuli aliamzisha miradi mikubwa ya Umeme na Reli.Mabepari uchwara Huwa ni maneno mengi bila vitendo lakini usisahau pia Katiba inaitambua Tanzania kuwa ni nchi ya Kijamaa;hutaki lamba ndimbu!
Sekta ya nyumba imeanza kurudi Kwenye viwango vyake.Asante SamiaWalishajipanga miaka na miaka wakati sisi huku tunapiga siasa na kuendekeza ufisadi wa kila aina.
Tunapokuja kudai tunaweza kujiendesha inakuwa ni sawa na kukumbuka shuka asubuhi.
Pia ni lazima tuelewe maono ya Rais SSH n kutaka kuifungua sekta yote ya uchukuzi na kufaidika na bandari kwa mapana yake.
Samia anatumia njia ya uendeshaji wa bandari inayoitwa Landlord Port management, kwa maana TPA inakuwa ikiendesha magati na mengine yanachukuliwa na DP World na mengine yanachukuliwa na mwendeshaji mwingine.
Hivyo hivyo kwa bandari ya Mbegani Bagamoyo, anatafutwa mwendeshaji mwingine. Haya ni masuala ambayo tija yake itakuja kuonekana miaka kadhaa ijayo.
Mtaani huku fremu za maduka zinaongezwa ukubwa maana yake wateja wapo, maana yake mzunguko wa pesa umeongezeka.Sekta ya nyumba imeanza kurudi Kwenye viwango vyake.Asante Samia View attachment 2766475View attachment 2766477View attachment 2766478
Hatukuwahi kuingia huko on merit ila kwa sababu ya korona benki ya dunia walishusha ceiling ya viwango vya uchumi ndio tukajikuta tumo kwenye uchumi wa kati kiwango cha chini.kwani uchumi wa kati tuliingia kini siyo awamu ya 5 kweli!
Bahati nzuri ameeleweka vizuri.Mkuu ChoiceVariable naomba nikuulize swali binafsi, do you even know any essence of the so callled Economics? Kwasababu kwenye bandiko lako so far bado sijaona applicabiliy ya neno uchumi kulingana na the way ulivyotafsiri wewe.
Naendelea kuwakumbusha tuu kwamba miaka 6 ya Uongozi wa Awamu ya 5 sekta ya nyumba "Rea estates" ilidorora,Kudoda na kuporomoka kwa kasi ya mwanga hadi kufikia nyumba nyingi huko Dar kuwa empty na matangazo ya benki kupiga bei nyumba yalijaa mitaani na wanunuzi hakuna sababu uchumi iliporomoka na pesa hakuna.
Aidha bei ya ardhi na nyumba ilishuka na biashara hii kiujumla ilivurugika na ikafikia mahala Ukiwa na kiwanja au nyumba kama dhamana banks zikawa zinakataa au unapewa hela kiduchu.
Ni katika awamu ile ndio Posta Mpya ilibakia magofu huku majumba mengi ya ghorofa yakikosa wapangaji nankubakia tupu.
Ujenzi wa miradi mikubwa ya makazi ulisimama mfano Kawe, Morocco Square, Kigamboni ECO Village, magorofa ya mashirika ya pensions nk, Shirika kama NHC, kampuni za ukandarasi wa majengo zilijifia.
Punde si punde Mungu akasikia kilio akamleta Rais Samia Mama wa Uchumi na Mwanamageuzi wa kweli (Reformists) akapiga chini mipango ya Kijima na Kijamaa kwenye uendeshaji wa nchi, akafungua uchumi na kurekesha Imani ya wafanyabiashara na wawekezaji hatimaye uchumi ukaanza kurejea kule kwa enzi ya Jakaya.
Sasa hivi kwa kutumia mfano mmja tuu wa Shirika la Nyumba la Taifa NHC kimeanza tena kupata faida na kufufua miradi yake yote iliyokuwa imekwama.
Hongera sana Rais Samia wewe ndio Mama wa Uchumi unaandika historia na alama ya kudumu kwenye mioyo ya Watanzania maana kila sekta inafurahia uwepo wako.
My Take
Ogopa sana Wajamaa, ujamaa ni umaskini na Utapeli.
=====
View attachment 2707848
Shirika la Kimataifa la Fedha (IMF) limeipongeza serikali ya Tanzania kwa kuimarisha utulivu wa kiuchumi wakati ambapo dunia ilikuwa inapitia changamoto mbalimbali ikiwemo janga la Ugonjwa wa Virusi vya Korona (UVIKO-19), vita vya Urusi na Ukraine na mabadiliko ya tabianchi.
Pongezi hizo zimetolewa na Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa IMF, Bo Li baada ya kumaliza ziara yake nchini ambapo amesema “jitihada za haraka za serikali ya Tanzania zilisaidia kudhibiti mfumuko wa bei na kulinda uchumi dhidi ya athari za vita nchini Ukraine.”
Licha ya mafanikio hiyo, taasisi hiyo imeihimiza Tanzania kuimarisha ukusanyaji wa mapato ya ndani ambayo yatakuza uwezo wa Serikali katika kugharamia huduma za kijamii na kuongeza uwekezaji katika elimu, afya, maji na sekta nyingine muhimu.
Li akizungumza na wawakilishi wa sekta binafsi, asasi za kiraia na wadau wengine wa maendeleo ameeleza kuvutiwa sana na nguvu na uhai wa uchumi wa Tanzania.
Tanzania ni moja ya nchi chache barani Afrika zenye kiwango cha chini zaidi cha mfumuko wa bei ambapo kwa miezi sita mfululizo umekuwa ukishuka kutoka asilimia 4.9 Januari hadi asilimia 3.6 Juni mwaka huu.
=======
Ujenzi wa Nyumba 560 za mradi wa Samia Housing Scheme, unaoendelea Kawe, Dsm, umefikia ghorofa ya nne kwa ujumla.
Kwa mujibu wa mmoja wa wasimamizi wa mradi huo Mhandisi George Shanel, kinachoendelea hivi sasa #SHS kwa ujuma, ni usukaji wa nondo, maboksi ya kushikia zege (form work), umwagaji zege, nguzo, beam na slabs kutoka ghorofa ya tatu kwenda ya nne.
aidha, ameongeza kuwa kingine kinachoendelea ni ujenzi wa kuta za tofali kwaajili ya kutenganisha vyumba ghorofa ya pili kufuatia kukamilika kwa ghorofa ya kwanza.
Kazi nyingine inayoendelea ni Uwekaji wa mifumo ya umeme na maji ghorofa ya chini (Ground floor), upigaji wa plasta kwenye kuta za ndani ghorofa ya chini (finishing).
Mradi ulianza Oktoba 2022 unatarajiwa kuisha mapema mwakani.
View: https://twitter.com/dailynewstz/status/1698608211597684998?t=go0aNjSxAp7fMmfkI2qxww&s=19
Mama yuko kazini
Acha uongo benki ya dunia wenyewe wakikutana na waziri madilu wa fedja walishangaa kwa huu uzushi eti tanzania imeshuka haipo tena kwenye uchimi wa kati.Hatukuwahi kuingia huko on merit ila kwa sababu ya korona benki ya dunia walishusha ceiling ya viwango vya uchumi ndio tukajikuta tumo kwenye uchumi wa kati kiwango cha chini.
Baada korana kupungua sana duniani na chumi nyingi kuanza kukaa sawa duniani ceiling ikapanda. Automatically tumejikuta hatumo.
Hujui tu. Ujamaa nao umebadilika unaenda na wakati. Ona mfano china na urusi. Lengo ni kuhakikisha kila mwananchi anapata fursa na anafaidika na maendeleo ya kiuchumi na sio kuwepo na tabaka la wachache kudhibiti uchumi wa nchi.Ujamaa unapotea kwa kasi sana duniani. Elimu zinazofundishwa mashuleni kwa sasa ni zile zenye kuweka msisitizo kwenye kumuwezesha mwanafunzi kuwa mbunifu na mtundu. Ni elimu inayokwenda na dunia ya uvumbuzi kuliko ile ya kufundisha masuala yale yale ya kijamaa.
Thanks mrangi✊Vigogo wanajinunulia tu majumba
Ova
Acha uongo benki ya dunia wenyewe wakikutana na waziri madilu wa fedja walishangaa kwa huu uzushi eti tanzania imeshuka haipo tena kwenye uchimi wa
Hujakatazwa kuendelea kubaki na ujumaa au kuwarithisha wanao huo ujamaa. Pia hujalazimishwa kuanza kuwa bepari. Ila ninachofahamu I kwa uhakika ni kuwa ulipo amua kununua bando la kutandawika humu jukwaani hujapanga foleni!Utulivu gani kama sio hawa imf na wb wanampamba mtu wao. Mtu anayekopa ovyo kwao na kuliwekwa taifa kwenye utegemezi. Hiyo sekta ya nyumba wanampongeza bure tu. Kuruhusu serikali na mashirika yake kukodi kwa bei mbaya majengo binafsi wakati ya serikali yapo ndio kujenga au kuhujuma fedha za umma?
Eti ogopa sana ujamaa. Hsyo maghorofa yanayojengwa kwa fedha za umma huku hila kibao zikitumika kuonyesha ni za binafsi yanamsaidia nini mtu wa kawaida? Sana itakua ni hujuma kwa maslahi ya umma. Maghorofa kibao ya NHC yamekua bila wapangaji au wanunuzi kutokana na bei zinazochangiwa na gharama za ujenzi kubwa zenye cha juu za vigogo. Saa hizi sera za kutaka kuwauzia wageni wanaosita kununua kwa kua sheria hairusu wao kumiliki ardhi ndio kikwazo. Tumeona sasa wanataka kubadili sheria ili wageni wamiliki ardhi nchini mwetu.
Sisi tunasema ubepari ni unyama twende na ujamaa wetu.
Ndio inavyotakiwa bila vigogo wote tutaishia kuwa choka mbaya kama wewe.Vigogo wanajinunulia tu majumba
Ova
Ni vigumu sana kuizua nafsi ya binadamu isibuni njia mbalimbali za kutafuta maendeleo. Ujamaa wa hao China na Russia ni wa kutafuta fursa zaidi huu wa kwetu ni ushenzi wa kutazamana nani ana miliki prado mpya halafu tunaangalia mshahara wake kama unamuwezesha kuinunua!.Hujui tu. Ujamaa nao umebadilika unaenda na wakati. Ona mfano china na urusi. Lengo ni kuhakikisha kila mwananchi anapata fursa na anafaidika na maendeleo ya kiuchumi na sio kuwepo na tabaka la wachache kudhibiti uchumi wa nchi.
Mchango mujarab!Ni vigumu sana kuizua nafsi ya binadamu isibuni njia mbalimbali za kutafuta maendeleo. Ujamaa wa hao China na Russia ni wa kutafuta fursa zaidi huu wa kwetu ni ushenzi wa kutazamana nani ana miliki prado mpya halafu tunaangalia mshahara wake kama unamuwezesha kuinunua!.
Ni ujinga ulioanza tangu awamu ya Mwalimu Nyerere, umejaa roho mbaya ndani yake zile akili za tukose wote. Stupid mindset.
Sasa hiyo ndio umeona hoja kutetea ubepari?😂😎Hujakatazwa kuendelea kubaki na ujumaa au kuwarithisha wanao huo ujamaa. Pia hujalazimishwa kuanza kuwa bepari. Ila ninachofahamu I kwa uhakika ni kuwa ulipo amua kununua bando la kutandawika humu jukwaani hujapanga foleni!