Sekta ya nyumba imeanza kufufuka kwa kasi chini ya Rais Samia Mama wa Uchumi

Sasa hao uliowataja wewe umeona walisimamia sera za Kijamaa? Hao wote walisimamia ubapari ndio uchumi ulifanya vizuri lakini akina John na Julius ni Bure kabisa
Mimi Huwa naona magofu ya Viwanda vingi tulivyojenga wakati wa Ujamaa vimekufa,ila kwenye zama za umimi Kuna wengine waliuziwa viwanda vya Nyerere wakavibbadilisha kuwa Godowns.
Wakati wa Mjamaa Magufuli aliamzisha miradi mikubwa ya Umeme na Reli.Mabepari uchwara Huwa ni maneno mengi bila vitendo lakini usisahau pia Katiba inaitambua Tanzania kuwa ni nchi ya Kijamaa;hutaki lamba ndimbu!
 
Kwani Bandari za Dubai zinaendeshwa na nani kama siyo serikali!
 
Kwani Bandari za Dubai zinaendeshwa na nani kama siyo serikali!

Kwani Bandari za Dubai zinaendeshwa na nani kama siyo serikali!
Walishajipanga miaka na miaka wakati sisi huku tunapiga siasa na kuendekeza ufisadi wa kila aina.

Tunapokuja kudai tunaweza kujiendesha inakuwa ni sawa na kukumbuka shuka asubuhi.

Pia ni lazima tuelewe maono ya Rais SSH n kutaka kuifungua sekta yote ya uchukuzi na kufaidika na bandari kwa mapana yake.

Samia anatumia njia ya uendeshaji wa bandari inayoitwa Landlord Port management, kwa maana TPA inakuwa ikiendesha magati na mengine yanachukuliwa na DP World na mengine yanachukuliwa na mwendeshaji mwingine.

Hivyo hivyo kwa bandari ya Mbegani Bagamoyo, anatafutwa mwendeshaji mwingine. Haya ni masuala ambayo tija yake itakuja kuonekana miaka kadhaa ijayo.
 
Ujamaa unapotea kwa kasi sana duniani. Elimu zinazofundishwa mashuleni kwa sasa ni zile zenye kuweka msisitizo kwenye kumuwezesha mwanafunzi kuwa mbunifu na mtundu. Ni elimu inayokwenda na dunia ya uvumbuzi kuliko ile ya kufundisha masuala yale yale ya kijamaa.
 
Sekta ya nyumba imeanza kurudi Kwenye viwango vyake.Asante Samia
 
Ungeenda Tu kwenye point mabuyu ya asali yanapishashana huko juu. Katembeleeni Bibi na babu Kule kantalamba ndo mlete hizi fukunyunyu
 
kwani uchumi wa kati tuliingia kini siyo awamu ya 5 kweli!
Hatukuwahi kuingia huko on merit ila kwa sababu ya korona benki ya dunia walishusha ceiling ya viwango vya uchumi ndio tukajikuta tumo kwenye uchumi wa kati kiwango cha chini.

Baada korana kupungua sana duniani na chumi nyingi kuanza kukaa sawa duniani ceiling ikapanda. Automatically tumejikuta hatumo.
 
Mkuu ChoiceVariable naomba nikuulize swali binafsi, do you even know any essence of the so callled Economics? Kwasababu kwenye bandiko lako so far bado sijaona applicabiliy ya neno uchumi kulingana na the way ulivyotafsiri wewe.
Bahati nzuri ameeleweka vizuri.
 
Utulivu gani kama sio hawa imf na wb wanampamba mtu wao. Mtu anayekopa ovyo kwao na kuliwekwa taifa kwenye utegemezi. Hiyo sekta ya nyumba wanampongeza bure tu. Kuruhusu serikali na mashirika yake kukodi kwa bei mbaya majengo binafsi wakati ya serikali yapo ndio kujenga au kuhujuma fedha za umma?
Eti ogopa sana ujamaa. Hsyo maghorofa yanayojengwa kwa fedha za umma huku hila kibao zikitumika kuonyesha ni za binafsi yanamsaidia nini mtu wa kawaida? Sana itakua ni hujuma kwa maslahi ya umma. Maghorofa kibao ya NHC yamekua bila wapangaji au wanunuzi kutokana na bei zinazochangiwa na gharama za ujenzi kubwa zenye cha juu za vigogo. Saa hizi sera za kutaka kuwauzia wageni wanaosita kununua kwa kua sheria hairusu wao kumiliki ardhi ndio kikwazo. Tumeona sasa wanataka kubadili sheria ili wageni wamiliki ardhi nchini mwetu.
Sisi tunasema ubepari ni unyama twende na ujamaa wetu.
 
Acha uongo benki ya dunia wenyewe wakikutana na waziri madilu wa fedja walishangaa kwa huu uzushi eti tanzania imeshuka haipo tena kwenye uchimi wa kati.
 
Hujui tu. Ujamaa nao umebadilika unaenda na wakati. Ona mfano china na urusi. Lengo ni kuhakikisha kila mwananchi anapata fursa na anafaidika na maendeleo ya kiuchumi na sio kuwepo na tabaka la wachache kudhibiti uchumi wa nchi.
 
Acha uongo benki ya dunia wenyewe wakikutana na waziri madilu wa fedja walishangaa kwa huu uzushi eti tanzania imeshuka haipo tena kwenye uchimi wa

Hujakatazwa kuendelea kubaki na ujumaa au kuwarithisha wanao huo ujamaa. Pia hujalazimishwa kuanza kuwa bepari. Ila ninachofahamu I kwa uhakika ni kuwa ulipo amua kununua bando la kutandawika humu jukwaani hujapanga foleni!
 
Hujui tu. Ujamaa nao umebadilika unaenda na wakati. Ona mfano china na urusi. Lengo ni kuhakikisha kila mwananchi anapata fursa na anafaidika na maendeleo ya kiuchumi na sio kuwepo na tabaka la wachache kudhibiti uchumi wa nchi.
Ni vigumu sana kuizua nafsi ya binadamu isibuni njia mbalimbali za kutafuta maendeleo. Ujamaa wa hao China na Russia ni wa kutafuta fursa zaidi huu wa kwetu ni ushenzi wa kutazamana nani ana miliki prado mpya halafu tunaangalia mshahara wake kama unamuwezesha kuinunua!.

Ni ujinga ulioanza tangu awamu ya Mwalimu Nyerere, umejaa roho mbaya ndani yake zile akili za tukose wote. Stupid mindset.
 
Mchango mujarab!
 
Hujakatazwa kuendelea kubaki na ujumaa au kuwarithisha wanao huo ujamaa. Pia hujalazimishwa kuanza kuwa bepari. Ila ninachofahamu I kwa uhakika ni kuwa ulipo amua kununua bando la kutandawika humu jukwaani hujapanga foleni!
Sasa hiyo ndio umeona hoja kutetea ubepari?😂😎
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…