Selasini aishauri CHADEMA kuhusu maridhiano, asema CHADEMA lazima imshirikishe Rais Samia

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
5,383
Reaction score
18,776
Mwanachama wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Joseph Selasini, amesema haiwezekani kukataa maridhiano bila kwanza kuwepo mchakato wa kuyafikia.

Amesema mchakato huo unapaswa kuwa na wajumbe, mwenyekiti na ajenda za kujadiliwa, ambapo pande zinazohusika zinaweza kukubaliana au kupendekeza mabadiliko kabla ya kufikia uamuzi wa mwisho.

Soma pia: Baada ya Miezi Miwili kurejea CHADEMA, Selasini ataka Heche achunguzwe na Selasini arudi CHADEMA baada ya kukihama NCCR

Selasini amesema Watanzania wanahitaji kuzungumza ili kufikia maridhiano, akisisitiza kuwa maridhiano ni matokeo ya mchakato wa majadiliano na si jambo linaloweza kukataliwa kabla ya mchakato huo kuanza.

Your browser is not able to display this video.
 
Nilijua tu hawa watu wanafanya kazi za kutumwa na CCM, na wamepewa mission kuja kuwavuruga Chadema.

Chadema mnapaswa kuwa makini sana na watu walioondoka na kisha wanaomba kurudi. Wengi huwa ni mamluki wametumwa na wanalipwa kuja kuwavuruga.

The most effective person CCM watataka kumpanda ndani ya Chadema ni yule anaejifanya ametubia makosa yake anaomba kurudi Chadema. Be very careful na watu hao.

Selasini akiwa ndani ya Chadema hana mamlaka ya kutoa maoni kwa jambo ambalo linapaswa kutolewa msimamo wa chama. Kama ana maoni kama haya anapaswa kuyatoa ndani ya vikao vya chama. In fact hili ni jambo hata Heche au Lisu hapaswi kulisemea as an individual, sembuse Selasini? Kwa jambo kama hili Selasini anapaswa kufukuzwa toka Chadea kwa sababu anapandikiza mbegu za kukigawa chama.
 
Huyu jamaa nae
 
Kila siku tunawaambia chadema ni washamba, hawana jinsi watafya nn
 
Hiyo ni strategy ya baadhi ya wanasiasa kutafuta relevance na nafasi za kuteuliwa na serikali.
Basi ni very poor strategy ya mtu ambae hana busara wala hekima. Ni sawa na wewe ukiwa umeajiriwa mahali uamue kuongea na waandishi wa habari kuhusu msimamo wa kampuni ambao unapaswa kuchukuliwa.

Hata katika timu za mpira. Cuculela alipobwabwaja kuhusu namna ambavyo Chelsie wanapaswa kuiunda timu, alionywa na kukaripiwa. Huwezi wewe ukiwa ndani ya timu kwenda kubwabwaja nje kitu ambacho kinapaswa kujadiliwa ndani ya timu na kusemwa na viongozi wa timu. Selasini sio msemaji wa Chadema.

Afukuzwe tu, arudi alikotoka
 
Huyu Kenge anataka mchakato wa kupata maridhiano na nani?
Serikali na wananchi au serikali na vyama vya siasa?
Je anataka waridhiane nini; kuhusu serikali kuua wananchi au wananchi kupewe maiti wao walio uawa na serikali?
 
Mil 2 oyeeee
 
Hakika, na anajidanganya sana kudhani kuwa anaweza/ataweza kuendesha siasa nje ya mfumo wa chama.
 
Mnaridhiana kuhusu nini wewe si ulikua NCCR ulipomaliza kukiua umerejea tena kufanya biashara ya kuiua chadema wao wanasema mkiti wao aachiwe ili yeye ndie aongoze hayo maridhiano sio wewe 30 ukae na yeriko mkishapewa posho mseme mnataka maridhiano mana pia hamweleweki mara mnasema michango imeliwa mara mnasema maridhiano haya yote mtafanya ila mjue watanzania sio wajinga....Endeleeni kujilisha upepo nyie watu washenzi sana njaa njaa zenu zinaiumiza nchi miaka na miaka...

Mbona hamtoki kufanya hizo press zenu mkiona watu wametekwa?? mbona hamsemi kwamba barabra nchi yetu hii zimeoza zote mbona hamsemi miji michafu haijapangwa?? mbona hamsemi shida na ugumu wa maisha wa watu wengi nyie mnasema michango imeliwa mara mtu kahongwa na Nileshi halafu hapo hapo mwingine anasema Nilesh kaibia serikali dola mil 40!! hivi serikali ikiibiwa ndio mchange akalalamike kwenye media??? hupo ujinga kiasi gani?? hiyo si jinai?? kama serikali inajua mtu kala hela kwanini hajakamatwa?? mnatufanya sisi mazoba kweli!! Huu mradi ni sawa na ule wa chauma utaishia kulala doro kuleni hela hizo za laana maana ni za umma hizo mnakula mnapayuka kizazi chenu kinapata laana maana kuna wamama wamekosa huduma wakafa kwasababu hela hazikuepo kuwanunulia madawa ukahongwa wewe upayuke una laniwa moja kwa moja....
 
umeeleza ukweli mtupu mtupu mwenyekiti mpya wa Chadema taifa katika muda usiokua mrefu ujao 🐒
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…