Selasini aishauri CHADEMA kuhusu maridhiano, asema CHADEMA lazima imshirikishe Rais Samia

Selasini aishauri CHADEMA kuhusu maridhiano, asema CHADEMA lazima imshirikishe Rais Samia

NAFIKIRI SHIDA IKO HAPAA: NANI ALIWAMBIA VIJANA KUFANYA FUJOOO ZILEEE.MAANA MSINGI WAMAPATANO LAZIMA AJULIKANE NI NANI ALIWATUMA VIJANA WALE.KAMA NI CHADEMA ISEME NI SISI .KAMA NI WANAHARAKATI WASEME NI SISI. UKISHASEMA NI MIMI NILIWATUMA ,HAPA SASA TUNAKAA CHINI TUNALIDHIANA KWAMBA SIKU NYINGINE USIFANYE VILEEE NA PIA MLICHOMA SHELI NA MALI ZA SERIKALI.KWA HIYO SASA UNAKUBARI KULIPA FIDIA? MHHHHHHHHHH.MZIKI UKO HAPOOOOOO
Bangi zimekukaa nyingi kichwani!.
Tafuta kilevi kingine, hiki kinakudhuru.
 
Nilijua tu hawa watu wanafanya kazi za kutumwa na CCM, na wamepewa mission kuja kuwavuruga Chadema.

Chadema mnapaswa kuwa makini sana na watu walioondoka na kisha wanaomba kurudi. Wengi huwa ni mamluki wametumwa na wanalipwa kuja kuwavuruga.

The most effective person CCM watataka kumpanda ndani ya Chadema ni yule anaejifanya ametubia makosa yake anaomba kurudi Chadema. Be very careful na watu hao.

Selasini akiwa ndani ya Chadema hana mamlaka ya kutoa maoni kwa jambo ambalo linapaswa kutolewa msimamo wa chama. Kama ana maoni kama haya anapaswa kuyatoa ndani ya vikao vya chama. In fact hili ni jambo hata Heche au Lisu hapaswi kulisemea as an individual, sembuse Selasini? Kwa jambo kama hili Selasini anapaswa kufukuzwa toka Chadea kwa sababu anapandikiza mbegu za kukigawa chama.
Mnakigeuza CDM kuwa CCM2. Sio dhambi kwa mwanachama wa chama cha siasa kuwa na mawazo binafsi yanayotofautiana na msimamo rasmi wa chama chake. Aidha, si dhambi kuyaweka hadharani ili yajadiliwe. Hamna mtu asiyejua kuwa anachosema 30 sio msimamo wa CDM. Kumkataza kuyasema ni kutaka wanachama wawe kama nyumbu ambao kazi yao ni kuwaimbia mapambio ya chama chao. Badala ya kumsimanga na kutaka afukuzwe, hoja zake zijadiliwe.

Mbona Lissu alimtetea Msigwa alipozungumzia ubadhirifu ndani ya chama chake kwa kukitaka CDM kizijadili kwa sababu zina mashiko?

Mnasahau kuwa Lissu alipinga waziwazi msimamo wa chama chake kuhusu Maridhiano na hakuchuliwa hatua yeyote?

Msigwa alipinga waziwazi msimamo wa wenzake kuhusu suala la Ngorongoro na hakuchuliwa hatua.

CDM ilionyesha ukomavu wake wakati ule kwa kuruhusu hizo tofauti za mtazamo ndani yake. Kwa kufanya vile walijitofautisha na CCM.

Amandla...
 
Mwanachama wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Joseph Selasini, amesema haiwezekani kukataa maridhiano bila kwanza kuwepo mchakato wa kuyafikia.

Amesema mchakato huo unapaswa kuwa na wajumbe, mwenyekiti na ajenda za kujadiliwa, ambapo pande zinazohusika zinaweza kukubaliana au kupendekeza mabadiliko kabla ya kufikia uamuzi wa mwisho.

Soma pia: Baada ya Miezi Miwili kurejea CHADEMA, Selasini ataka Heche achunguzwe na Selasini arudi CHADEMA baada ya kukihama NCCR

Selasini amesema Watanzania wanahitaji kuzungumza ili kufikia maridhiano, akisisitiza kuwa maridhiano ni matokeo ya mchakato wa majadiliano na si jambo linaloweza kukataliwa kabla ya mchakato huo kuanza.

Hivi hao wanaotaka chadema afanye maridhiano,"mardhiano gani? Nadhani chadema hawana tatizo la kuridhiana na serikali au ccm. Chadema siku zote wako very straight. Wanachotaka uchaguzi uwe huru na wa haki. Ikiwa hivyo sidhani kama kuna haja ya kuridhiana. CCM na serikali yao nao wanajua Uchaguzi huru na haki kwao ni over impossible kwa sababu kwa utawapunguzia ulaji kwa hiyo ccm wanapetipeti kujifanya wanajua kutawala. Chadema watakuwa hovyo kufanya maridhiano na mtu anaye kuulia wanachama waki kila wakati tena kwa kuwapiga risasi na kuwatupa kama wanyama.
 
Mnakigeuza CDM kuwa CCM2. Sio dhambi kwa mwanachama wa chama cha siasa kuwa na mawazo binafsi yanayotofautiana na msimamo rasmi wa chama chake. Aidha, si dhambi kuyaweka hadharani ili yajadiliwe. Hamna mtu asiyejua kuwa anachosema 30 sio msimamo wa CDM. Kumkataza kuyasema ni kutaka wanachama wawe kama nyumbu ambao kazi yao ni kuwaimbia mapambio ya chama chao. Badala ya kumsimanga na kutaka afukuzwe, hoja zake zijadiliwe.

Mbona Lissu alimtetea Msigwa alipozungumzia ubadhirifu ndani ya chama chake kwa kukitaka CDM kizijadili kwa sababu zina mashiko?

Mnasahau kuwa Lissu alipinga waziwazi msimamo wa chama chake kuhusu Maridhiano na hakuchuliwa hatua yeyote?

Msigwa alipinga waziwazi msimamo wa wenzake kuhusu suala la Ngorongoro na hakuchuliwa hatua.

CDM ilionyesha ukomavu wake wakati ule kwa kuruhusu hizo tofauti za mtazamo ndani yake. Kwa kufanya vile walijitofautisha na CCM.

Amandla...
NI sawa, lakini si kila jambo la chama linapaswa kusemwa hadharani na wananchama, hasa pale inapotokea wanaenda kinyume na msimamo wa uongozi wa juu wa chama.

Kutoa ushauri juu ya mambo ambayo hayana msimamo wa chama ni kawaida. Na pia ni muhimu kuangalia nani anayatoa. Haya aliyosema Selasini kama yangesemwana mwanachama wa kawaida wala sio nongwa

Kwa hiyo inabidi uwe na busara nakuangalia angle zote.

Wamarekani weusi wanakuambia, mweusi mwenzangu akiniambia "Hi nigger, what's up" sina tatizo. Sasa ngoja mzungu aniambie maneno hayo hayo atakiona cha moto!
 
Jinga kabisa zee la hovyo.

Huyo Samia alichaguliwa na nani?
 
Wakati huyu mzee anarudi CHADEMA mkumbuke kuwa kipindi hicho hicho ndio mchungaji Msigwa alikuwa amerudi pia kukawa na wanachama wengi hasa wa kutoka CHAUMA wakawa nao wanarudi CHADEMA kwa fujo. Na mbaya zaidi mpaka kiongozi mmoja wa juu wa sasa wa CHADEMA (jina namuhifadhi) akawa anampigia debe hadharani Halima Mdee eti arudishwe kwa sababu chama ni watu. Haya sasa watu wenyewe ndio kama hao wakina mzee Selasini.

Kwa mtizamo wangu mimi wa kulaumiwa sio mzee Selasini bali viongozi wa CHADEMA ndio wa kulaumiwa mwanzo mwisho. Nilihoji humu jamvini hivi inakuwaje baadhi ya wanachama ambao wengine waliondoka kwa kukiumiza na kukidhalilisha chama halafu kirahisi tu mtu anarudi wengine kwa kutweet, wengine wanaitisha vi "youtube tv" na vi "media" vya uchochoroni n.k. anajitangazia mwenyewe kuwa amerudi CHADEMA. Nikauliza hivi CHADEMA haina muongozo wa namna mwanachama aliyeondoka/aliyefukuzwa anatakiwa kuufata ili arudishwe kuwa mwanachama. Na pia ni nani anatakiwa atangaze kuwa mtu fulani karudishiwa unanachama wake yaani ni viongozi ndio wanaotakiwa kutangaza au ni watu wenyewe waliorudishiwa uanachama ndio wanajitangaza wenyewe. Zaidi nikawaomba viongozi watoke hadharani walilizungumzie hili kwa kutoa msimamo wa chama. Wao wakakaa kimya wakaichukulia kama "issue" ndogo sana hii. Pia nilishauri kiongozi akirudi aishie huko huko kwenye tawi/msingi na asipewe wadhifa wowote hata uongozi wa tawi/msingi kwa kipindi cha miaka mitatu mpaka mitano huku akiwa chini ya uangalizi wa kina kuhusu mienendo yake.

Lakini pia sikuwaacha viongozi wa CHADEMA hivi hivi lakini nashukuru niliwapa zawadi yao nikawaambia wao ni kama kenge tu kwani hawasikii mpaka damu ziwatoke masikioni. Na pia niliuliza inakuwaje hao viongozi wanainyooshea CCM kidole kwenye baadhi ya mambo wakati wao jambo dogo tu la wanachama kurudi linawashinda hata kulitolea muongozo au tamko. Aisee kuna wanachadema walinishukia kama mwewe lakini sikujali kwa sababu nilikuwa nimewashauri mambo ya maana sana na nilijua tu siku si nyingi kibuyu kitalia. Sasa kipo wapi si kibuyu kimeshalia huko mtafutano kila kona.

Anyway ya CHADEMA tuwaachie wapararune huko maana mgeni kashaingia ndani hadi chumbani kaleta balaa baba na mama wanajikuna. Na mbaya zaidi mpaka sasa hivi hakuna kiongozi yoyote wa juu aliyetoa tamko kuhusiana na Selasini na hata kwa viongozi na wanachama wote maarufu waliorudi kwenye hicho chama. Na tawi/msingi wake Selasini alipojiungia nao kimya wakati wale viongozi wa kanda waliotisha "press" juzi juzi tu hapa wala siku tatu hazikupita baada ya tamko lao wakala umeme.

Na wewe mzee Selasini na wazee wengine mliopo kwenye hivi vyama vya siasa bila kujali upo CCM, CHADEMA, ACT, CUF, TLP, n.k. hebu muwe washauri huko ndani zaidi hata ikitokea umetoa boko linaishia ndani kwa ndani kuliko kujitoa ufahamu na kuja hadharani kujifanya washauri wazuri huku mnatoa maboko. Hii inawafanya wazee wote waonekane wa ovyo na vijana wakiwadharau mnalalamika kukosewa adabu.

Ni mtizamo tu.
 
NI sawa, lakini si kila jambo la chama linapaswa kusemwa hadharani na wananchama, hasa pale inapotokea wanaenda kinyume na msimamo wa uongozi wa juu wa chama.
Msimamo wa uongozi wa juu wa chama ni kuficha tuhuma za ubadhirifu?
Kutoa ushauri juu ya mambo ambayo hayana msimamo wa chama ni kawaida. Na pia ni muhimu kuangalia nani anayatoa. Haya aliyosema Selasini kama yangesemwana mwanachama wa kawaida wala sio nongwa
Selasini ni mwanachama wa kawaida na alitumia yake kukishauri chama chake. Bila shaka alitumia uzoefu wake katika vyama vingine.Kwa hiyo inabidi uwe na busara nakuangalia angle zote.
Wamarekani weusi wanakuambia, mweusi mwenzangu akiniambia "Hi nigger, what's up" sina tatizo. Sasa ngoja mzungu aniambie maneno hayo hayo atakiona cha moto!
Unachanganya neno "nigger" na "nigga". Hamna mtu yeyote anayekubaliwa kumuita mwingine "nigger" hata kama na yeye ni mweusi. Neno linalotumiwa na wamarekani weusi peke yao ni "nigga". Hata hivyo wako wamarekani weusi wengi tu wanaopinga matumizi yake na mtu yeyote.

Amandla...
 
Back
Top Bottom