Mara baada ya Mwananchi kupitia JamiiForums.com kulalamikia huduma ya Kazi za N-CARD katika kuweka fedha, inayowalazimu kupanga foleni wakati wa kuitumia katika Kivuko Kigamboni, ufaafanuzi umetolewa na Selcom.
Selcom imeandika "Ni rahisi sana. Utaingia kwenye app yako ya Selcom, kisha uchague ‘Kutuma Pesa’. Baada ya hapo chagua ‘Tuma kwenye Kadi’, halafu uchague ‘Selcom N-CARD’. Weka namba ya kadi, kisha weka kiasi cha pesa unachotaka kutuma. Ukikamilisha hatua hizo, utakuwa umefanikiwa kuweka salio kwenye N-CARD yako."