Selection ya kidato cha tano kuna mengi ya kujifunza

Nikiwa advance shule yetu ilikuwa ni sayansi full na kozi ni mbili tuu.

Mwanafunzi anakuja na div.2 nzuri au three ya mwanzo ila concepts nyepesi za form 2 hazielewi kabisa. Imefika necta ya form 6 wamepiga zero za kutosha na division 4.
Waliokuja na div 1 atleast ndio waliambulia three za kwenda vyuoni. Hizi Combination za science watu waende na hizo div.1 tuu.

Kama mtu kqshindwa kupata one O-level either kwa sababu za mazingira huko advance mazingira ndio magumu automatically tena ambapo waalimu hawapo na sometimes wanaamini mmekua watu wazima so mjipambanie

Ila special cases zipo wapo waliotoka o level na div 3 wakakomaa advance wakafaulu vizuri, wapo ila wachache
 
Una hoja usikilizwe
Ila A level sio masihara jmn
Hasa Sayansi
 
Naona mwanao hakufanya vizuri. Pole sana.
 
Kuna uhusiano gani kati ya kusoma Art na umaskini au Sayansi na kutokuwa maskini???!!!!
 
Niende kwenye mada; mwaka huu TULIPATA habari kuwa wanaopangwa SAYANSI yaani PCM na PCB ni wenye daraja la kwanza tu tena wavulana ni 7-15 na WASICHANA ni 7-17...

Huu uongo uliutoa wapi?
 
Asnte Sana kwa UZI wako mkuu Ila
Kwa mwanafunzi ambae Ana flat C
PHYSICS-C
CHEMISTRY-C
BIOLOGY-C
MATHEMATICS-C
Huyu hawezi kusoma mchepuo/tahasusi ya science
Huyu lazima apangiwe ARTS COMBINATION
Huu uongo mmeutoa wapi? Wewe ni muongo jasiri. Nina kijana amepangiwa PCM na ana DCC
 
Siyo lazima aliyekuja na I atatoka na I na siyo lazima kuwa aliyekuja na II hawezi kupata I.....
 
Msijali itatoka batch 2, kujazia nafasi ambazo zimeachwa nimeongea na mtu wa ndani kabisa.
 
Huoni ni kuna shida? Mwenye point 10 yaani CCD anaenda ufundi [VOCATIONAL] halafu mwenye point 9 anaenda ARTS??

Hii ina make sense? Halafu WANASEMA wanahamasisha watoto wasome SAYANSI?
Selection inafata Selform alijazaje.. Tusiilaumu serkali.. Mm Kuna mwanafunz alipata 1.7 but hakuchagua kwenda f5... Alijaza kwenda chuo kwa ajili ya certificate na alienda... Na hakujaza kibahat mbaya....
So tusikariri kuwa ukipata dv1 lazima uende f5. Ni uchaguzi wa mtu
 
Una hoja, mtoto wangu tayari alishaanza form five private wenyewe wanaita introduction na amesharudi Nyumbani na serikali imempangia shule pia wakati kimsingi Wazazi tumeshakubaliana atasoma private.

Kula kulala hawawezi kukuelewa hoja ya msingi sana.
 
Sitasahau nilikuwa mwanasayansi nguli wa familia nkapangwa HGK, mama akaniambia ukifika kule utabadilisha, kufika shule kombi za sayansi zimefutwa, kuna HGE, EGM, HKL, HGL. Na mzee baba mwenyewe HGK shule ipo mbali, nikaenda kwa mkuu wa shule akaniambia sasa hapa kwanza tuliangalia masomo uliyofaulu sana, wewe huko Sayansi hapawezi na makarai yako kwanza una F ya hesabu. Nikasema kwa hasira nitasoma hiyohiyo niliyopangiwa. Mungu mkubwa sina mpango wa kuajiriwa.
 
Kuna kijana Ana C - Physics, B-Chemistry, A- Biology,,kapelekwa HGL ambako ana C- History, B-Geography na C- English ,,Kagoma kwenda shule
Mbona nikipiga mahesabu ana div. 1? Imekuwaje? Anapoint zaid ya 15 au? Basi hii haijakaa sawa
 
Hana hoja. Kwanza serikali huwa inakuja na batch ya 2 baada ya kutathmini waliosajiliwa. Hoja zingine kaandika hisia . Kwamba PCM na PCB ni wenye daraja la kwanza tu tena wavulana ni 7-15 na WASICHANA ni 7-17...ni uongo mtupu kwani wapo watoto wenye division 2 mpaka 20 wamechaguliwa tena kwa DCC
 
Kuna kijana Ana C - Physics, B-Chemistry, A- Biology,,kapelekwa HGL ambako ana C- History, B-Geography na C- English ,,Kagoma kwenda shule
Kama shule ina PCB aende akabadilishe, kama haina atafute uhamisho
 
NASHUKURU KWA KUNIELEWA HOJA YANGU...

Lazima ifike wakati WATENDAJI WETU WAACHE UVIVU WA KUFIKIRI..

Unapangaje SELECTION bila kutambua UWEPO WA SHULE ZA PRIVATE ZA KIDATO CHA TANO NA SITA??? halafu wanatoa taarifa shule hazitoshi.....

Kwa Akili ya KAWAIDA KABISA wanafikiri KEMEBOYS, MARIAN, FEZA, MARRY MAZINDE na nyinginezo nyingi zitakosa wanafunzi wa kidato cha TANO kiss wote wameenda SERIKALINI!!!!🀣🀣🀣🀣🀣🀣🀣🀣🀣🀣🀣🀣
 
Kama shule ina PCB aende akabadilishe, kama haina atafute uhamisho
Sidhan kama wataruhusu kubadilisha combi, kutoka Arts kwenda Sayansi,kuyokana na vigezo walivotumia katika selection, mana watoto wengi wamepelekwa combi ambazo hawakutegemea, wanakuwa wamepoteza mda wao kusoma sayansi
 
Sidhan kama wataruhusu kubadilisha combi, kutoka Arts kwenda Sayansi,kuyokana na vigezo walivotumia katika selection, mana watoto wengi wamepelekwa combi ambazo hawakutegemea, wanakuwa wamepoteza mda wao kusoma sayansi
Kigezo ni hizo alama alizopata
 
Kwa kigezo gani km mnajari First Selection ya Mwanafunz zungatie Minimum Qualifications achaneni na mambo ya kufikirika

KUSOMA ADVANCED
Minimum Qualifications inahitajika C 3 kwenye Cheti cha Mwanafunzi na ili aweze kufanya km School candidate bhs itahitajika Ufaulu usiopungua D kwenye Masomo ya Combination yake.

Sasa km Minimum Qualifications ni hizo kwanini mtu ambae Kapata C flat au CCD kwenye Combination yake mkatae asisome First Priority ya Combination zake.

Kifupi Swala la Mitihani ni Jambo Pana sn mtu Unaweza kuwa Vizuri Mathematics na Chemistry lkn matokeo yakitoka Mathematics Una C na Chemistry Una C na kwa Bahati nzuri Masomo ambayo haupo vizuri unakuta umefanya vyema may be History Una B Kiswahili Una B.

Km mnajua anaeenda kusoma ni Mwanafunzi kwanini msiheshimu Chaguo lake mfano aliweka PCM hata km ana D au C ya Physics mpeni nafasi Yeye ndy anajua Uwezo wake . Anaweza kuwa na C mathematics lkn trend ya Ufaulu wake ni Constant hata km Unampa mitihani 10 yote anauwezo wa kupata C au C+ na sio kumpeleka HKL Kwa sababu tu ana B history na kishwahili wkt hii kwake sio Outstanding Performance na hata km utampa Mtihan Mwingne anaweza kushuka kutoka B mpk C au D na sio kumaintain.

Tupende kuzingatia chaguo la Mtu tuache Mihemko yetu Binafsi Kwa kigezo cha kuangalia Performance ya Mtihan Moja tu (National Exams) na sio Performance ya Kila Siku. Tufate Minimum Qualifications kuwapangia wanafunzi first selection zao itasaidia Sana.

Asnte Sana kwa UZI wako mkuu Ila
Kwa mwanafunzi ambae Ana flat C
PHYSICS-C
CHEMISTRY-C
BIOLOGY-C
MATHEMATICS-C
Huyu hawezi kusoma mchepuo/tahasusi ya science
Huyu lazima apangiwe ARTS COMBINATION
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…