Selelii awazima Lowassa na Rostam

Selelii awazima Lowassa na Rostam

SteveD,

Hapana, sio kwenye makampuni tu bali hata serikali. Mfano ni hapa UK kwenye money for peerages na Blair. Kulikuwa na ushahidi lakini prosecutor akaona uwezo wa kushinda ni mdogo, akaamua kuiachia case.

Hicho ndio ninachoongelea mimi, ni tofauti na kuwaachia wahalifu ambao wamehukumiwa au kutumia pesa nyingi kumhukumu na kumfunga mhalifu. Kama unaona uwezo wa kumfunga ni mdogo, ni bora kutumia hizo pesa kwenye mambo ya maana.

Kama tumekubali suala la akina RA mwamuzi ni JK, ifike mahali tumwachie yeye na sisi wananchi tutoe hukumu yetu 2010.
mtz kwanini lakini unapenda kupotosha ukweli, suala peers na gharama zake za kesi unaweza kuzilinganisha na billioni zetu za umeme na maafa yake kiuchumi na hizo gharama za kesi.
Hili la peerage ukililinganisha na suala la Posho mara mbili nitakuelewa, lakini sio hili la Richmond na Mikataba mingine inayo hushusiana na Hii au uhujumu uchumi tena wa taifa changa kama tanzania.
haya mahesabu ya u-engineer yatakuwa questionable sasa, labda ikiwa hizo hesabu zimeingiliana na siasa.
 
Mtanzania,
Kwanza samahani maanake niseme ukweli kwamba maandiko yako mengi sana yamekaa ki CCM sana na mara nyingi umekuwa against hizi kuhudi za kuendelea kuwaumbua hawa mafisadi. I can only ask - What's UP!

Mkuu hoja ni UFISADI, na haiwezi hoja hii kutupwa kapuni pasipo kuwashughulikia mafisadi. Nitazidi kusema Mapinduzi yoyote huanza na wananchi ambao wako tayari kuzungumzia uovu huo mbele ya sheria inayokataza ama kupuuza juhudi hizo. Lowassa na Rostam ni baadhi ya wahusika na kwa sababu wao ni wana CCM, chama kinachoongoza ni lazima mkazo wetu ubakie ktk target hiyo. Wengine wote ni wafuasi tu ambao wamekubali hali halisi kama vile kule South kuna weusi waliojiunga na jeshi la Kaburu na kufanya hata mauaji. Mkazo wa ANC ulikuwa kukiondoa chama tawala madarakani na hapo ndipo wewe unapoingiza upinzani ktk fikra zangu..

Inanisha mshangao sana unapokazania YAISHE! hii lugha ni ya kukata tamaa ambao haitakiwa kwa mpiganaji na nikutokana na hofu hiyo ndio maana mnawapa chat wapiganaji 11. Binafsi sioni sababu kwa nini isiwe wapiganaji millioni ukiwa nawe upande wao.

Mkandara,

Mimi sina matatizo na sisi wananchi kujadili mafisadi kwenye vijiwe vyetu. Tatizo langu lipo kwa wale wanaotumia pesa zetu kujadili jambo moja miaka mitatu bila maamuzi ya maana.

Vikao vingapi vya bunge vinazunguka na mduara wa Richmond bila kufikia tamati? Hapo ndipo mimi nina matatizo napo. Kama hawana uwezo wa kuwashughulikia mafisadi ni bora waelekeze nguvu kwenye kazi wanazoweza kuzifanikisha.

Hizo tuhuma zako zingine labda ni mawazo yako tu. Tulivyojadili posho mbili mbili, hivi ni UCCM kupinga posho mbili mbili?
 
SteveD,

Kama tumekubali suala la akina RA mwamuzi ni JK, ifike mahali tumwachie yeye na sisi wananchi tutoe hukumu yetu 2010.

- Ni haki yetu wananchi kuendelea kuongea kuhusu Richimonduli, regardless Facts za Yona na Mramba zilikuwepo lakini baada ya kuzomewa na kurushiwa mawe kule Mbeya kwa Rais wetu, ghafla wakakamatwa ili kutunyamazisha kwa hiyo hatupungukiwi chochote kuendelea kujadili Richimonduli,

- Na kama kweli kuijadili kwetu ni waste of time basi mafisadi wasingehangaika kama wanavyohangika sasa hivi kujisafisha na kitu ambacho hakina maana na kutowajibishwa kwao na Rais na waziri Mkuu wake hakuondoi chochote juu ya integrity ya kamati ya Mwakyembe on the ishu!

Respect.

FMEs!
 
Mtanzania,
Kwanza samahani maanake niseme ukweli kwamba maandiko yako mengi sana yamekaa ki CCM sana na mara nyingi umekuwa against hizi kuhudi za kuendelea kuwaumbua hawa mafisadi. I can only ask - What's UP!

Mkuu hoja ni UFISADI, na haiwezi hoja hii kutupwa kapuni pasipo kuwashughulikia mafisadi. Nitazidi kusema Mapinduzi yoyote huanza na wananchi ambao wako tayari kuzungumzia uovu huo mbele ya sheria inayokataza ama kupuuza juhudi hizo. Lowassa na Rostam ni baadhi ya wahusika na kwa sababu wao ni wana CCM, chama kinachoongoza ni lazima mkazo wetu ubakie ktk target hiyo. Wengine wote ni wafuasi tu ambao wamekubali hali halisi kama vile kule South kuna weusi waliojiunga na jeshi la Kaburu na kufanya hata mauaji. Mkazo wa ANC ulikuwa kukiondoa chama tawala madarakani na hapo ndipo wewe unapoingiza upinzani ktk fikra zangu..

Inanisha mshangao sana unapokazania YAISHE! hii lugha ni ya kukata tamaa ambao haitakiwa kwa mpiganaji na nikutokana na hofu hiyo ndio maana mnawapa chat wapiganaji 11. Binafsi sioni sababu kwa nini isiwe wapiganaji millioni ukiwa nawe upande wao.

Mkandara,

Hakuna ubaya sisi wananchi kujadili ufisadi kwenye vijiwe vyetu; mimi tatizo langu ni hao ambao wanatumia mapesa ya wananchi kujadili jambo moja miaka mitatu. Bunge lifike mahali kama halina uwezo wa kuwawajibisha hao watuhumiwa basi wasonge mbele na mambo mengine ya nchi.

Hayo ya mawazo ya KICCM naona ni vijembe vya kisiasa. Hapo juzi nilipinga posho mbili mbili au nayo ni mawazo ya KICCM?

Hao wapiganaji 11 hatima yao iko kwa wananchi sawa na wanasiasa wengine wowote. Mijadala ya JF na magazeti ya Nipasha na Majira hayawezi kuwaokoa. Kitakachowaokoa ni delivery ya ahadi zao walizotoa mwaka 2005.

Kipenga kikilia itakuwa mshike mshike.
 
Nafikiri kwa kesi hii SteveD/Mkandara na Mtanzania mko sahihi kwa upande mmoja wa shilingi Vs mwingine.

Alichokisema SteveD ni kweli kuwa wakati mwingine ukihukumu kesi kama hii na kumfunga Ex-President, utakuwa umeokoa mamilioni ya fedha kwa siku za mbeleni. Alipoingia Rawlings wa Ghana, nilipewa habari kuwa Mafisadi kadhaa walichapwa risasi na kuweka mfano wa nini kinaweza kuwapata mafisadi.

Ila upande wa pili wa shilingi kuna maneno ya Mtazania. Kwa nchi nyingi duniani ambazo viongozi wa zamani wanaondolewa kwa njia ya uchaguzi, sijawahi kuona kiongozi wa zamani akihukumiwa na kufungwa. Sanasana watahukumiwa watoto, mkewe, mawaziri, wapambe nk. Ukiangalia hata German, Mzee Helmut Kohl, aliwekewa mizengwe mingi sana na mmoja wao alikuwa ni huyu mama anayetawala sasa Angela Merkel. Pamoja na kuwa na ushahidi na yeye kukubali kupokea HONGO kutoka kwa kampuni ya mafuta ya Ufaransa - ELF.
Hapa ndipo unaanza kukubaliana na Mtanzania kuwa, kumshabikia huyu mtu ni kupoteza muda na pesa. Sanasana inabidi uweke au kubadilisha sheria ili kuthibiti haya mambo mapema zaidi kabla hayajatokea.

Mwisho kwa mawazo yangu, ingebidi tuanze kumulika pesa za michango ya UCHAGUZI. Ikibidi tuweke miiko na mipaka ya upokeaji pesa. Haya mambo ya pesa zinatoka sijui kwa Waarabu, Iran, Japan, Canada, etc ni kujivisha wenyewe kitanzi. Viwavi jeshi kwa tamaa ya kuwa RAIS, wataenda kuchukua/kupokea hela hata za Mafia wa Mexico na Chaccobamba kama siyo Columbia kwenyewe......
 
mtz kwanini lakini unapenda kupotosha ukweli, suala peers na gharama zake za kesi unaweza kuzilinganisha na billioni zetu za umeme na maafa yake kiuchumi na hizo gharama za kesi.
Hili la peerage ukililinganisha na suala la Posho mara mbili nitakuelewa, lakini sio hili la Richmond na Mikataba mingine inayo hushusiana na Hii au uhujumu uchumi tena wa taifa changa kama tanzania.
haya mahesabu ya u-engineer yatakuwa questionable sasa, labda ikiwa hizo hesabu zimeingiliana na siasa.
August,

Ukisoma ujumbe mmoja na kuja na conclusion yako utachanganyikiwa sana hapa JF. Ulichoandika hapo juu sio sahihi kabisa. Hakuna nilipolinganisha mambo ya Richmond na masuala ya peerages kwa UK.

Please soma majibizano yangu yote na SteveD kabla ya kuandika ulichoandika hapo juu. Hayo maandishi hayakuwa na uhusiano kabisa na Richmond, sana sana yalikuwa na uhusiano na case ya Chiluba.
 
Mtanzania,
Hayo ya mawazo ya KICCM naona ni vijembe vya kisiasa. Hapo juzi nilipinga posho mbili mbili au nayo ni mawazo ya KICCM
Kwa hiyo nayo unafikiri tusonge mbele!.. tatizo langu kwako ni huo msemo wa tusonge mbele wakati nchi inaliwa mbele na nyuma. when are we going to say enough is enough!..
Leo hii imefikia hata baadhi ya wajumbe wa chama CCM kujiengua ktk chama hicho.. unafikiri huu ni uamuzi rahisi mkuu wangu..
Kama wewe ni Mpiganaji kwa njia yako pigana na Ufisadi mahala popote regardless, na sii kuchagua baadhi kwa sababu fulani yumo ktk mashtaka hayo.. Hapo ndipo tunapogomba mkuu wangu.
 
SteveD,

Hapana, sio kwenye makampuni tu bali hata serikali. Mfano ni hapa UK kwenye money for peerages na Blair. Kulikuwa na ushahidi lakini prosecutor akaona uwezo wa kushinda ni mdogo, akaamua kuiachia case.

Hicho ndio ninachoongelea mimi, ni tofauti na kuwaachia wahalifu ambao wamehukumiwa au kutumia pesa nyingi kumhukumu na kumfunga mhalifu. Kama unaona uwezo wa kumfunga ni mdogo, ni bora kutumia hizo pesa kwenye mambo ya maana.

Kama tumekubali suala la akina RA mwamuzi ni JK, ifike mahali tumwachie yeye na sisi wananchi tutoe hukumu yetu 2010.
samahani kama nimechanganya, lakini haya maneno hapo juu au nilio quote yameandikwa na nani na yana maana gani katika hii thread?
 
Tumeona ya akina Chiluba dola $13m kutumika kufukuzia case ya laki tano. Nikipewa chaguo, nitazitumia hizo $13m kujenga shule au hospitali kuliko kumfukuzia mtu mmoja ambaye hata sina uhakika wa kumfunga.

Je, una uhakika kwamba katika hizo $13 millioni hazikubambikwa pesa chungu nzima za kifisadi!? Hebu tupe breakdown ya hizo $13 millioni zilivyotumika ili tuone kama matumizi yote yalikuwa ni ya halali. Kesi ya OJ ambayo ilichukua muda mrefu na ilikuwa na wanasheria wengi kuliko kesi ya Chiluba gharama za kesi hizo hazikufika $13 millioni. Na gharama za wanasheria Marekani ni kubwa mno kuliko zile za Zambia. Sasa hii kesi ya Chiluba na gharama kubwa hizo hujiulizi kulikoni!? Umewekewa hapo $13 millioni basi umeamini uhalali wa gharama hizo bila hata kuhoji.

Kwa maana nyingine wewe unaona wavunja sheria waendelee tu kupeta mtaani kwa sababu kuwafungulia mashtaka Serikali itaingia gharama kubwa kuliko kile walichokivunjia sheria! Na hapo unataka kuwa Mbunge 2010 wakati hata kutetea utawala wa sheria bora unashindwa kufanya hivyo!

Kwa kukumbusha tu kwenye ufisadi unaowahusu hao wapambe wako Lowassa na papa fisadi Rostam tunazungumzia $212 millioni ($172 milliono za Richmond na $40 millini za Kagoda)
 
samahani kama nimechanganya, lakini haya maneno hapo juu au nilio quote yameandikwa na nani na yana maana gani katika hii thread?

Ungesoma alichoandika SteveD na kisha majibu yangu na utajua nilikuwa naongelea nini. Katika mijadala yote ya JF kunakuwa na mini threads kibao yaani mjadala unaongelea jambo moja, unaenda kwingine na unarudi ulikoanzia.

Kama nilivyoandika mwanzoni hapo tulikuwa tujadiliana na SteveD kuhusu theory ya Satisficing na ndio likaja suala la Chiluba na money for peerages.

Nilichoshangaa ni accussation kwamba nalinganisha Richmond na money for peerages.
 
Je, una uhakika kwamba katika hizo $13 millioni hazikubambikwa pesa chungu nzima za kifisadi!? Hebu tupe breakdown ya hizo $13 millioni zilivyotumika ili tuone kama matumizi yote yalikuwa ni ya halali. Kesi ya OJ ambayo ilichukua muda mrefu na ilikuwa na wanasheria wengi kuliko kesi ya Chiluba gharama za kesi hizo hazikufika $13 millioni. Sasa hii kesi ya Chiluba na gharama kubwa hizo hujiulizi kulikoni!? Umewekewa hapo $13 millioni basi umeamini uhalali wa gharama hizo bila hata kuhoji.

Kwa maana nyingine wewe unaona wavunja sheria waendelee tu kupeta mtaani kwa sababu kuwafungulia mashtaka Serikali itaingia gharama kubwa kuliko kile walichokivunjia sheria! Na hapo unataka kuwa Mbunge 2010 wakati hata kutetea utawala wa sheria bora unashindwa kufanya hivyo!

Kwa kukumbusha tu kwenye ufisadi unaowahusu hao wapambe wako Lowassa na papa fisadi Rostam tunazungumzia $212 millioni ($172 milliono za Richmond na $40 millini za Kagoda)

- He! he! he! jamani Demokrasia ina gharama zake na pia heshima kwa sheria pia ina gharama zake, bora kugahramia sheria kwa gharama yoyote ile kuliko kuacha kabisa hata kama ni dola $ Millioni 100 zitumike tu as long as matokeo ni msingi wa uongozi na sheria kwa taifa la mbele, kwenye hili kusiwe na mjadala wala compromise!

Respect.

FMEs!
 
Kwa kukumbusha tu kwenye ufisadi unaowahusu hao wapambe wako Lowassa na papa fisadi Rostam tunazungumzia $212 millioni ($172 milliono za Richmond na $40 millini za Kagoda)

Labda unisaidie nini maana ya wapambe wako?

Kama kuni link mimi na akina Lowassa kunakupatia usingizi zaidi basi kalale vizuri lakini furaha yako hiyo hata siku moja haitageuza facts.

Utabaki tu kuwa sawa na mlevi wa gongo ambaye kesho yake anaamka na kukuta matatizo yake yako pale pale kama livyoyaacha jana kabla ya kulewa.

Mtu ambaye hajamwibia mtu, hata urushe matope kiasi gani, hayawezi kumchafua. Sana sana watu watakushangaa na kukuona ni kichaa.
 
samahani kama nimechanganya, lakini haya maneno hapo juu au nilio quote yameandikwa na nani na yana maana gani katika hii thread?

August,

Nafikiri anachikisema Mtanzania nimekifafanua hapo juu. Huo ulikuwa mfano tu kama ambavyo mie nimetumia wa German. Mzee Kohl alijiuzuru tu na hawajamfanya kitu. Bush ana madhambi kibao na Dick Cheney ndiyo kabisa ila usije ukafikiri watakuja kushitakiwa.

Putin na ubabe wake, alimtisha hadi mtoto wa Yeltsin, ila mzee mwenyewe hakumgusa na Mlevi huyu na Ujinga wake wote, kafa na kuzikwa kwa heshima zote kama Rais wa nchi.

Mkapa na ubakaji wake wote, atakufa na mtamzika kwa heshima zote, na sahau JELA. Hilo hilo linamsubiri Kikwete. Utaweza kubadilisha hili, mara utakapokuja kwa mapinduzi. Vinginevyo, hawa jamaa huwa wana ndugu zao huko majuu watawasaidia tu. Kama USA/Canada wanafaidika kwa ubovu wa Kikwete, unafikiri watamuacha? Lazima watowe mfano kuwa huwa wanajali watu wao wanaosaidia nchi zao ziibiwe kwa jina la Demokrasia.

Hebu kula break kwa kuangalia kuanzia 0:57 ujikumbushe Rais wa Super Power Russia....

[ame]http://www.youtube.com/watch?v=xMThTEA4M0o[/ame]
 
Kwa maana nyingine wewe unaona wavunja sheria waendelee tu kupeta mtaani kwa sababu kuwafungulia mashtaka Serikali itaingia gharama kubwa kuliko kile walichokivunjia sheria! Na hapo unataka kuwa Mbunge 2010 wakati hata kutetea utawala wa sheria bora unashindwa kufanya hivyo!

Hii labda kama tunataka kujenga Banana republic.

Mjadala mzuri sana huu....

FMES nakubaliana na wewe tujenge utawala wa sheria kwa gharama zozote

Demokrasia ina gharama zake na pia heshima kwa sheria pia ina gharama zake, bora kugahramia sheria kwa gharama yoyote ile kuliko kuacha kabisa hata kama ni dola $ Millioni 100 zitumike tu as long as matokeo ni msingi wa uongozi na sheria kwa taifa la mbele
 
Sikonge,
Mifano ya German na Bush hailingani kabisa na hii ya kwetu. Marekani ina control mafuta yote ya Iraq na all contract za ujenzi wa nchi hiyo upo chini yao... yaani uvamizi wao ni kwa faida ya Marekani.. Bush is a hero kiuchumi. Kila wanapowapa gharama za vita hiyo, hata siku moja hawatawapeni faida zinazo tokana na vita hiyo kwao. Na laukama wangejali gharama kuliko kile walichokusudia basi bila shaka wangeondoka Iraq mwaka wa kwanza tu. America siku zote interest zao comes first.. na ndivyo ilivyo kwa nchi zote za kibepari.

Germany ni yale yale.. Mfuko wa Germany huwezi kuulinganisha na Tanzania hata chembe ya wilaya moja.. Kuna mchumi mmoja alinambia kwamba je unajua kwamba Norway ambayo inaongoza duniani kiuchumi kama ingekuwa state moja ya Marekani leo hii ingekuwa state ya 46 kiuchumi!..
sasa wewe pima nguvu ya Marekani au Germany kisha linanisha na maisha ya Uwanja wa fisi wetu (Tanzania).
 
- He! he! he! jamani Demokrasia ina gharama zake na pia heshima kwa sheria pia ina gharama zake, bora kugahramia sheria kwa gharama yoyote ile kuliko kuacha kabisa hata kama ni dola $ Millioni 100 zitumike tu as long as matokeo ni msingi wa uongozi na sheria kwa taifa la mbele, kwenye hili kusiwe na mjadala wala compromise!

Respect.

FMEs!

Kama ni utawala bora, mawaziri na marais wote kunzia Nyerere aachie madaraka wangelikuwa ndani. Kila ukiwachunguza ni ujambazi mtupu. Wanatumbua pesa za wananchi bila kunawa.
 
Masa na BAK,

Mko sawa kabisa. Ila wakati mwingine tuwe tunaangalia ukweli na hali halisi.

Naombeni jina la RAIS mmoja duniani aliyeondolewa kwa njia ya Demokrasia na ameishia JELA. Jina moja wandugu zangu mnikumbushe. Hata Kenya hapo, walishtakiwa hadi watoto wa Moi, yeye anapeta tu hadi kesho.

Mkandara: Una maana kuwa German ni tofauti na Tanzania? Kwamba kwa sababu ni German, basi wao UNAWEZA kupokea HONGO na ukaachwa bila kuhukumiwa? Sidhani kama ni hivyo mkuu wangu. Anyway, ntajaribu kuulizia sheria za German kwa watoa na wapokea hongo zikoje.....

Mwisho kwa USA, kama wanaleta faida kubwa kwa nchi, si wangelitumia kujisifu na kuupalilia uchumi wao unaolegalega? Hii ya kwenda China kukopa fedha ili wanunue Mafuta ndiyo hiyo faida wanayoleta? Au hiyo ni faida inayoingia kwenye mifuko ya akina Bush Family? Kila mtu anafahamu na ndiyo maana Republican walishindwa kwani ilibidi wabebe madhambi ya Bush. Watu wanamwaga damu, pesa zinakwenda na wanaofaidika ni wachache. Pamoja na kuyafahamu haya, leo Obama hawezi wala kuthubutu kusema "awashitaki akina Cheney/Bush". Na hili ndiyo mie nasema kuwa hawa Mapig fish, popote pale wanajua kuteleza utafikri wameumbwa kwa Mlenda......
 
Sera ya CCM kwa muda mrefu sasa imekuwa ni kulindana. Kama sio kulindana tusingekuwa na ubabaisha kwenye hili suala la Richmond mpaka leo. Rostam, Lowassa na Kikwete walikuwa kitu kimoja kwenye uchaguzi wa 2005.

kweli!

Urafiki wao haukuanzia barabarani kama Lowassa alivyosema. Wana siri zao. Wanalindana. Ukimwangusha mmoja naye anaweza kuwaangusha wenzake. Hivyo wataendelea kulindana.

Kweli!

Kamati ya Mwakyembe ililmpibu JK, JK amekula pozi. Anavuta subira mpaka 2010 ipite, hapo ndipo JK atakapoweza kuamua urafiki wao ufe. Until then itakuwa ni ngonjera tuu.

kimsingi Kamati Teule ilimpa nafasi JK kuonesha ni kipi kwake muhimu, urafiki au sheria? Akaamua kuminyia na kumtoa Lowassa kafara. Hata hivyo amegoma kabisa kumtoa kafara Rostam kwani kati ya Lowassa na RA ni RA ndiye aliyeuteka moyo wa JK. Lowassa is dispensable, RA is not.
Bunge ndicho chombo cha kutunga sheria. Kama wanaona rais anazembea katika kuchukua hatua wangeenda a step further. Lakini bunge letu linajali zaidi maslahi ya chama kuliko maslahi ya taifa

Another truth; nafurahia we start getting to the core of the matter. Kama wabunge wako serious kuhakikisha wanaweza. Lakini watu kama Zitto hawaamini wana nguvu hizo. Wanaamini kuwa Rais ndiye mkuu wa mihimili yote na wao kazi yao ni "kushauri" tu na serikali ikigoma hawana la "kufanya". Ni aibu kwa kweli.
. Wanaendeleza sera za kulindana. Mduara unaendelea. Wapiganaji nao wanawaandama mafisadi lakini kwa sababu za kulinda maslahi yao wanamsifu fisadi mkuu, JK. Unafiki.

Ni kweli ndio sababu ya kuandika ile makala ya "Wapiganaji CCM wanapigania nini?". Hadi hivi sasa basi sijapewa jibu zaidi ya ukweli huo hapo juu. Maslahi.

Kamwe hatutaweza kushinda vita dhidi ya mafisadi kama hii vita haitapata support kutoka juu, kwa rais mwenyewe. Na rais huyo anatakiwa awe msafi, asiwe na mikono yenye damu ya ufisadi. Kwa sasa mikono ya JK imechafuka. Hivyo kuanzia sasa hadi uchaguzi wa 2010 kutakuwa hamna progress yoyote ya maana katika vita hii ya ufisadi.

Inahuzunisha lakini uko karibu na ukweli zaidi kuliko watu wengi wanaojadiliana. Inauma lakini hatuna budi kuungalia machoni na kuuita kwa jina lake.

Sanasana kutakuwa na majeruhi katika vita vya kujipanga kugombania ubunge, ufisadi ukitumiwa kama silaha mojawapo.
.

Hii inatakiwa iwe ni nukuu ya kuanzia wiki hii kweli.
 
Masa na BAK,

Mko sawa kabisa. Ila wakati mwingine tuwe tunaangalia ukweli na hali halisi.

Naombeni jina la RAIS mmoja duniani aliyeondolewa kwa njia ya Demokrasia na ameishia JELA. Jina moja wandugu zangu mnikumbushe. Hata Kenya hapo, walishtakiwa hadi watoto wa Moi, yeye anapeta tu hadi kesho.

Ukweli na hali halisi give me a break mzee!

Umetaka jina la raisi ambaye ameishia jela, nina wasi wasi huangalii habari za kimataifa zaidi ya kushinda JF! LOL

Aliyekuwa Raisi wa Taiwani Chen Shui-bian alimehukumiwa kifungo cha maisha na kupigwa faini ya $US6.1 million. Kwa makosa ya kugushi, matumizi mabaya ya madaraka, na kula rushwa. Hukumu ilitolewa tarehe 11 Sept 2009.

Sema kingine, EL na RA wanatakiwa wawe lupango!

Link

http://www.wsws.org/articles/2009/sep2009/taiw-s23.shtml

Tusitetee ujinga, eti waachwe tuendeleee acheni hizo ebooo!
 
Mkandara,

Hakuna ubaya sisi wananchi kujadili ufisadi kwenye vijiwe vyetu; mimi tatizo langu ni hao ambao wanatumia mapesa ya wananchi kujadili jambo moja miaka mitatu. Bunge lifike mahali kama halina uwezo wa kuwawajibisha hao watuhumiwa basi wasonge mbele na mambo mengine ya nchi.

Tatizo si hao wanaotumia miaka mitatu kujadili jambo moja bali tatizo ni kuwa na Rais ambaye anawaogopa mafisadi waliombeba na kumuweka Ikulu. Ingekuwa kama tuna Rais ambaye ameweka mbele maslahi ya Taifa na kutowaogopa wale waliomchangia mabilioni ya shilingi ili aibuke kama Rais wa nchi yetu hii issue ya Richmond ingekuwa imeshamalizika zamani kama ambao walistahili kufungwa na kufilisiwa wameshafilisiwa au kuachiwa huru na tunasonga mbele na issues nyingine, lakini kutokana na kuwa na Rais ambaye ameshindwa kutumia madaraka makubwa tuliyomkabidhi ya kutetea maslahi ya nchi yetu ndiyo maana hadi hii leo bado tunajadili issues chungu nzima ambazo ziko tangu 2006 kama vile mikataba ya uchimbaji wa madini ambayo haina maslahi kwa Watanzania ambapo wageni wanachukua 97% na kutuachia sisi 3% bado tunajadili EPA hadi hii leo Rais ametwambia kwamba mafisadi waliohusika na EPA wamerudisha shilingi 70 billioni lakini wakati huo huo ameshindwa kutuwekea hadharani majina ya akina nani waliorudisha pesa hizo na kiasi walichorudisha. Na hizi kesi huko mahakamani hazipewi uzito wowote na baada ta October 2010 zote zitatoswa kwa kisingizio kwamba hakuna ushahidi wa kutosha dhidi ya mafisadi. Kagoda ambayo papa fisadi Rostam kachota $40 millioni hata kuhojiwa tu TAKUKURU imeshindwa kumuhoji. Meremeta nayo ambako $155 millioni zimeyeyuka katika thin air nayo sasa tunaambiwa ni usalama wa Taifa hivyo haiwezi kujadiliwa Bungeni. Kiwira ambayo pamoja na Mkapa kuiba Kiwira eti Pengo na watetezi wengine wa mafisadi wakasimama Bungeni na kwenye kikao cha NEC kutaka kumtetea Mkapa kwamba ni mtu safi kabisa! wakati ukweli tunaujua.

Kama unataka kuwa Mbunge 2010 kwa style hiyo ya "kusonga mbele" bila kujali yale yanayojiri ndani ya nchi yetu ambayo yana kero kubwa kwa Watanzania miaka nenda miaka rudi basi hutufai kuwa Mbunge kwa sababu utataka kulisukuma Bunge eti "lisonge mbele" bila kuyashughulikia maswala muhimu ambayo yanawakosesha raha Watanzania walio wengi kwa kuona kwamba nchi yetu haina utawala wa sheria bora.
 
Back
Top Bottom