Hao Lowassa na papa fisadi ni wapambe wako maana wanakupamba kwa kila namna ili ukamuondoe mbaya wao kule Kyela.
Mimi sijakulink kabisa na hao mafisadi bali kilichokulink na hao mafisadi ni unachoandika hapa cha kuwatetea kwa nguvu zako zote bila kujali maslahi ya nchi yetu na kuthubutu kusema eti tufukie mashimo na kusonga mbele bila kutafutia ufumbuzi madudu chungu nzima ambayo yanaitafuna nchi yetu kila kukicha. Unayoyaandika yanaonyesha kabisa hufai kupewa wadhifa wowote ndani ya nchi yetu hata ujumbe wa nyumba 10 haukufai.
Katika kipindi hiki ambacho nchi yetu inapita katika wakati mgumu kuliko wowote ule hatuhitaji Wabunge wa kufukia mashimo ili tu tusonge mbele wakati huko mbele kuna kiza cha kutisha na nyuma pia kuna madudu ya kutisha. Hatuwahitaji kabisa ndani ya Bunge letu Wabunge wenye kutaka kufukia mashimo kama wewe utakavyo.
Mzee wa NATO (No Action Talking Only), sisi huku tunaita wazee wa kubwabwaja. Kazi kujaza posts JF huku hakuna kinachofanyika. Afadhali hata sisi wengine tumehamasisha CHADEMA hapa Kyela na wamepata vitongoji vitano.
Kama unataka wafukia mashimo njoo huku Kyela uwasaidie, vinginevyo tegemea kubwagwa chini bwaaa! Mtavimba sana 2010.
Unaonaje wewe ukawe mfukia mashimo kwa kugombea huko kwenu?
Wewe isikie tu Kyela, hatuna habari na hao akina Lowassa au RA. Kyela hainunuliki. Mengi amejaribu kutaka kutununua kwa kugawa pikipiki lakini zimeishia kuchukuliwa na matapeli ambao hawawezi hata kumshawishi mtu mmoja. Wengi wao ndio hao walibwagwa na CHADEMA juzi.