Selelii awazima Lowassa na Rostam

Masa,

Ndiyo maana nikaomba JINA. Nilikuwa nimesahau kabisa hii kesi na nikawa nakumbuka zaidi kesi za EUROPE na America. Nashukuru kwa hiyo link ambayo kwa njia moja au nyingine, inamjibu pia Mkandara kuwa kwa kutowa RUSHWA, unaweza kwenda JELA MILELE. Ila hata German na sheria zao, walimgwaya Kohl.


Masanilo, nafikiri ni ndoto za Watanzania wengi sana wasiopenda Mafisadi kuwa na system kama za hawa Wa-Asia. Si unaona mwenyewe kuwa Uchunguzi ulianza wakati jamaa bado yuko ofisini? Sasa hebu muone Mwana sheria mkuu wa Tanzania au Rashid Othman akianza kumpeleleza Kikwete sasa hivi kwa ombi la Mbowe/Dr. Slaa au Chadema. Si unaona kabisa ni ndoto?

Sasa kuliko kusema tu kujifurahisha, tuwe tunaangalia hali halisi ya sheria za Tanzania, katiba na mihimili ya dola imekaakaaje. Sintategemea Hosea au AG au Polisi au UWT waaanze leo kumpeleleza Kikwete....... Inauma ila ukweli ndiyo huo. Tumefuata sana siasa/sheria za West ambazo huwa zinawalinda sana viongozi wa zamani. Kama tungelifuata za ASIA, hata wewe unafahamu kabisa kuwa leo hii akina Kingunge, Lowassa, Rostam na wengine wengi na kama sikosei Mkapa, wangelikuwa wanaishi na Babu Seya kama siyo majina yao kuwa yamepewa tittle mpya ya HAYATI.
 
sikonge nafikiri katika mada au thread hii hatuzungumzi kumfunga kiongozi wa juu wa serikali yetu tukufu, bali hawa waliochini waliomfikisha Rasi hapo alipo, pia kumbuka chochote katika maisha kina mwanzo, tanzania na kukosa kwetu maendeleo tumechelea saana kuchukua hatua katika mambo mengi ambayo hatimaye yatabadilisha hali iliyopo Sikonge na sehemu zingine za tanzania, barabara hata za single lane, umeme hata wa phase moja, darasa lenye ceailing board, dawati nk nk.
Pia kuna njia zingine za kuzui gharama kwa kesi kama hizi, mfano kutaifisha mali ya wahusika, kufuta mafao ya uzeeni, kuwafungia watu hao kushikilia nafasi za kiuongozi iwe wa kisiasa au makampuni nk.
 
Sikonge na Mtanzania,
Wakuu zangu sote tunatazama picha tofauti kabisa na hivyo itakuwa kazi ngumu sana kuwafahamisha..
Tatizo la Ufisadi wa Lowassa na Rostam ni mikataba mibovu ambayo inatugharimu sana toka kukosekana kwa umemehadi malipo tunayoingia. Nitendo hivi haviwezi kuyamaziwa tu kwa sababu ati Nyerere pia alitumia fedha npasipo kunawa..well kama alikuwa nakula ndizi mbivu alikuwa na haja gani kunawa!.. Ustaarabu wakuu zangu ustaarabu.

Sikonge wala usigusie kabisa mapato ya Marekani na kutazama mahitaji yao kuwa kigezo cha uchumi wao. Marekaani wamefikia kukufuru ktk matumizi na wanatumia vitu ambavyo sii lazima ktk maisha yao. Leo tu kuna ng'ombe wa maziwa mmoja kauza mnadani kwa Usd 1.2 millioni..Sasa kama ni swala la uharibifu sisi tungepiga kelele hadi kesho..Hiyo ndio Marekani mkuu wangu. Nitarudia kusema hatuwezi kuiga kunywa kwa Tembo, tutajipima mazuri na mabaya yetu kwa mifano inayofanana nasi.

Hayo ya Germany huyo kiongozi alijiuzuru kwa sababu chama chake kilipokea michango kinyume cha sheria na sii yeye. Na uchunguzi ulifanyika lakini ilishindikana kukiua chama kizima kwa sababu hakuna Upinzani..Kohl alijuzuru na kuchukua lawama zote kwa sababu mambo hayo yalifanyika chini ya Uongozi wake lakini sii kwamba yeye alichukua fedha za michango na kujineemesha.
Bush all he did was for the interest of America..hakuchukua kitu na kama angefanya hivyo ungeyasikia mengi makubwa kuliko hayo..Mikopo inayotokana na China ni kutokana na mali zinazotoka China nasii China kulipia madeni ya mafuta ya Marekani. China wenyewe hawana mafuta iweje wawape fedha Marekani kununua mafuta!.. mkuu wangu ebu rudi nyuma kidogo ukasome hizi habari maanake itakuwa kazi kubwa sana kufahamishana.
 
Ni kweli ndio sababu ya kuandika ile makala ya "Wapiganaji CCM wanapigania nini?". Hadi hivi sasa basi sijapewa jibu zaidi ya ukweli huo hapo juu. Maslahi.
Nilikujibu kwenye post no 24, kwa vile michango ilizidi 100 sio rahisi kuikumbuka yote, hivyo nimekuwekea tuu tena hapa for reference.

And by the way, kumbe aliyemfadhili Kamanda wa wapiganaji, Sitta kuupata Uspika n kumpigania tangu ndani ya CC alikuwa ni RA!
 
Mkandara,
Kweli tunaongelea picha mbili tofauti. Kama ungelikuwa umeelewa ninachikisema, basi ungeligundua tunaongelea kitu kile kile. Unachokisema wewe kwangu mie nakiona kwa sasa kukifanya Tanzania ni ndoto. Hebu angalia ile habari katuma Masa na mie nimeweka kipande juu ya Taiwan.

Labda nije na swali moja tu kwako na kwenu wengine wote:

Maadamu swala la Rishmonduli linajulikana in and out na linazidi kuburuzwa hadi leo na kila mtu anafahamu kuwa hili swala limeunga kwenye Kitovu ca Muungwana, je tufanyeje? Na unapojibu, kumbuka katiba ya Tz ambayo inaweza kumpa Rais wake hata Udikteta kama akitaka.........

Pia kumbuka Dowans, juzi jamaa wa KODI walijifanya MUCH KNOW, wamefikia wapi pamoja na kutumia sheria? Wasiwasi wangu ni kuwa kiongozi SHUJAA aliyeagiza Dowans ipigwe mnada, unaweza kukuta leo kashafukuzwa kazi na sisi hapa tupo tunaamini kuwa kuandika sana JF kutabadilisha mambo.
Ndiyo maana naungana na Kishoka katika kutafuta njia ambayo inaweza kubadilisha mambo hapa Tz. Kujificha ndani ya CCM, CUF, CHADEMA itakuwa yaleyale maana kule kuna wenyewe na NGO zao.
 



Quote:


Bila ya kuubomoa mfumo wa utawala wa kifisadi uliowaunda. tunaweza vipi kuwaondoa mafisadi wa sasa na kuwazuia wa baadaye?



MMKJJ, kwanza baada ya kukubali ufisadi ndio mfumo unaounda utawala wetu wa sasa, yaani ni system, halafu tunataka kugombea kisu huku walioshika mpini ndio hao hao, unategemea nini?.There is always one and only way ya kuchange system, system kamwe haibadiliki, lazima ibadilishwe, kama system imeundwa na mafisadi na kuendeshwa na mafisadi ili kuzidi kufisidi, hao wa kuibadilisha ni kina nani kama sio kutaka kuja kuibadilisha ili wapokezane zamu za kufisidi, na unawazuiaje mafisadi wa baadae wakati wengi wa wanasiasa wetu wanaingia kwenye siasa kama ajira kupigania nafsi zao?.Wanatakiwa wapatikane watu wa Calibre ya Dr. Slaa wengi wa kutosha na sio hao waimba mapambio kwa jina la makamanda.Hapa inatakiwa kitu kama the 'Bolshevic ya Octoba 1917' ama 'The American ya 1886' vinginevyo ni tunacheza makida makida.
 
.


And by the way, kumbe aliyemfadhili Kamanda wa wapiganaji, Sitta kuupata Uspika n kumpigania tangu ndani ya CC alikuwa ni RA!

- Mkuu hivi ulikuwa hujui kwamba Sitta, originally alikuwa Mtandao? Tunachojali ni anachofanya sasa kwenye uongozi wake na sio yaliyopita maana si ndwele!

Respect.


FMEs!
 
Tuendeleze mapambano na yeyote atakayeungana nasi tutapokea msaada wake maadam lengo ni kuiweka habari hii juu hadi siku wananchi wote wanatakapo jiunga nasi na kumwondoa CCM iwe 2010 au 2015.
Siku zote mnapokuwa na sababu will hufuata, ndio kama ule mfano wa Apartheid.. Wapo wazungu walioungana na wananchi na wakabezwa sana lakini mchango wao ktk nguvu ya kueneza machafu ya Apartheid ilikuwa kubwasana kiasi kwamba imekuja tambuliwa tu baada ya kujikomboa.
Kwa hiyo kuwabeza Wapiganaji ni kuwamaliza nguvu, kisha tunashindwa kuelewa kwamba pasipo hata wao leo hii swala la Ufisadi lingekwisha zimwa kabisa na Dowans wangekuwa mitamboni tukilipa Mabillioni. kama lilivyo swala la Buzwagi.

Mkuu wangu Tanzania hatuna Upinzani wa kweli hivyo ni kuokota okota kila tunachokipata kuendelea na harakati hizi hadi siku hata huyu JK pengine na nitaendelea kuomba Mungu kwamba siku moja atamuja mrudia Mungu wake..Lawama alizokuwa nazo hapa duniani nina hakika hatakuwa na kheri akhera..
Na mwisho mkuu wangu hakuna swala lolote ambalo nabii au mpiganaji alikubali kushindwa.. unapofikia hali hiyo umekubali kutawaliwa na hata historia ikibadilika vipi, bado wajukuu na vitukuu vyenu vitakuja pigana vita hii hii ambayo wewe na mimi tungeweza hata kujitetea..
Kusema ovyo mkuu kunasaidia hasa ktk nchi hizi za kimaskini. Hatuhitaji ushahidi, leo hii nikitangaza kuwa Semilong mazishi, tapeli basi watu watakupa za kisogoni..Amini maneno yangu kazi ya Wapiganaji inaanza kufanya kazi ndani ya chama CCM na watu kama Mtanzania watakuwa na wakati mgumu sana mbeleni..shutuma unazoziona humu zitaendelea pasipo watu kuachia hata kama sii kweli..
Amini maneno yangu.
 
Ukweli na hali halisi give me a break mzee!

Sawa Mkuu, nakupa Break Mzee wangu ................



Umetaka jina la raisi ambaye ameishia jela, nina wasi wasi huangalii habari za kimataifa zaidi ya kushinda JF! LOL
Naangali JF na michuzi tu. Si mwenyewe unafahamu Sikonge jinsi kulivyochoka? Hayo ma CNN na BBC yenu huku tunayasikia tu na sanasana kuangalia ninikimesemwa kwenye JF na Michuzi.

Mzee, ukimuweka EL na RA LUPANGO, basi kipato changu cha miezi sita nitachangia chama chako au kampeni za Urais/ubunge wako. Hili nakuhakikishia kabisa ntakuwa mpambe wako namba moja Sikonge kwa gharama zangu mwenyewe.......

Tusitetee ujinga, eti waachwe tuendeleee acheni hizo ebooo!

Hakuna anayeleta UJINGA hapa. Hata tukisema tukae kimya na mbaki nyie ambao hamleti UJINGA, sidhani kama mtakuwa na Matikiti maji mawili katikati ya Miguu ili mumpeleke EL na RA Lupango kwa sasa.

Na labda nikupe motisha zaidi. Ukiwatia hawa watu Lupango, basi naenda Zenji kukutafutia mtoto huyo, haki ya mama vigogo wakikuona watakuwa wanaacha njia na mashangingi yao wakimkodolea macho......
 
- Mkuu hivi ulikuwa hujui kwamba Sitta, originally alikuwa Mtandao? Tunachojali ni anachofanya sasa kwenye uongozi wake na sio yaliyopita maana si ndwele!

Respect.

FMEs!
Who pays the piper... Matokeo ya maamuzi ya Sitta kuhusu hoja za viporo tumeyaona, nakuhakikishia haya ni ya Musa tuu, ya Firauni tutayashuhudia kikao kijacho na amini usiamini, tutabaki midomo wazi!.
 
Hii nayo vipi? Halafu mtu aseme Rostam Azziz atakamatwa kwa wizi tu, hawa VIBAKA waliobaka hadi wanawake na kuwachomea nyumba na vyakula vyao hawajaguswa, nani aje awaguse akina EL na RA? Dowans na Richmond nayo itamaliza miaka 18 hakujafanyika kitu.

Naanza kuamini maneno ya GT kuwa USALAMA WA TAIFA Tanzania wanafanya kazi nzuri sana ya KULAZA WATANZANIA. Kama siyo hao basi ni Bagamoyo na vipande vya miili ya Albino.


Hii imetoka: https://www.jamiiforums.com/jukwaa-la-siasa/43894-mwanamke-wa-kimasai-wa-loliondo-atoa-ushuhuda.html
 
Sikonge,
Usiulize nani, kazi hii ni yako wewe, mimi na wengine wote...Tunachotakiwa ni kuendelea kupiga makelele tu, mara nyingi Simba hukimbia...hakufa mtu..kifupi ukipiga makelele hupungukiwi kitu, kesho mapinduzi yakitokea hutakuwa nyuma kusimuliwa..Kumbuka tu kuongezeka kwa kelele zako kunaongeza uvumi wa mayowe napia kundi linakuwa kubwa.
Rostam sii Mungu walishindwa kina Kaizali itakuwa huyu kweli.. Hivi unawajua Mabepari na nguvu ya matajiri waliokuwepo tanzania toka Uhuru... Hayo, Patel pekee huwezi kumweka kiti kimoja na Rostam, na mwaka jana tu hakuna mtu aloamini Patel, Yona na Mramba watafikishwa hata mahakamani... Tumepiga makelele kwa miaka mingapi..
Kwa hiyo huwezi jua kesho wewe Sikonge ndiye unaweza kuja na mbinu ya maana zaidi ikiwa tu utafikiria positive ya kwamba inawezekana. Na hata kama hukubaliani na fikra hizi basi kaa kimya fanya yako mwenyewe kivyako kuliko kujaribu kuwakatisha wananchi nguvu kwa sababu zako mwenyewe. Hukubaliani na Wapiganaji washauri ni njia gani wazichukue ukielewa wazi siasa za Bongo.
Huyu mkuu wetu Mwanakijiji ambaye namjua mimi mwaka jana sii huyu tena..Na hakika kupooza kwake kumechangia sana kupoteza elimu nzima ya mabadiliko ya kifira. Sisi tunaotazama upande huo tunafahamu mchango wa watu kama yeye na list ni kubwa sana ambayo ndio inayoijenga JF kuwa kijiwe chenye kutisha!
 
Nilikujibu kwenye post no 24, kwa vile michango ilizidi 100 sio rahisi kuikumbuka yote, hivyo nimekuwekea tuu tena hapa for reference.

Nililisoma jibu lako hilo. Lakini sidhani wanapigania "survival"... rejea hotuba ya Pengo kule Mwanza kwenye mazishi ya Mayala.

And by the way, kumbe aliyemfadhili Kamanda wa wapiganaji, Sitta kuupata Uspika n kumpigania tangu ndani ya CC alikuwa ni RA!

sidhani kama hii ni habari ngeni. RA aliwafadhili watu wengi tu ili aweze kuwa control. Wengine ndio hao sasa wamekata kamba.
 
MMKJJ, kwanza baada ya kukubali ufisadi ndio mfumo unaounda utawala wetu wa sasa, yaani ni system, halafu tunataka kugombea kisu huku walioshika mpini ndio hao hao, unategemea nini?​


swali zuri hilo

.There is always one and only way ya kuchange system, system kamwe haibadiliki, lazima ibadilishwe, kama system imeundwa na mafisadi na kuendeshwa na mafisadi ili kuzidi kufisidi

Kuna ukweli hapo. Hata hivyo ipo njia zaidi ya moja ya kubadilisha system; kuwabadili walioitengeneza.


, hao wa kuibadilisha ni kina nani kama sio kutaka kuja kuibadilisha ili wapokezane zamu za kufisidi, na unawazuiaje mafisadi wa baadae wakati wengi wa wanasiasa wetu wanaingia kwenye siasa kama ajira kupigania nafsi zao?.

that is the nature of politics and that is why we have term limits. Siasa ni jaribio la wananchi kuendesha maisha yao na kusahihisha makosa hayo kila baada ya kipindi fulani a.k.a uchaguzi.

PHP:
Wanatakiwa wapatikane watu wa Calibre ya Dr. Slaa wengi wa kutosha na sio hao waimba mapambio kwa jina la makamanda.

Unnecessary dismissiveness! Anayetaka wapambanaji malaika, watimilifu na wakamilifu kwa kila jambo itambidi asubiri kiyama au Yerusalem mpya ikishushwa kutoka mbinguni maana humo "hakutakuwa na kilio wala huzuni". Lakini ni hapa hapa; tutapata mashujaa waliojeruhiwa na viongozi walioanguka. Ni sehemu ya maisha yetu wanadamu. Ndio maana nilipuuzia sana hoja za Sofia Simba kwa sababu hatupiganii nani msafi au nani ni msafi zaidi!

Hapa inatakiwa kitu kama the 'Bolshevic ya Octoba 1917' ama 'The American ya 1886' vinginevyo ni tunacheza makida makida.

Ya Marekani ni 1776.. na si lazima ifanane na hayo; tunaweza kuwa nayo kama ya Poland, Ukraine, Georgia hata ya siku za karibuni ya Lebanon - mapinduzi ya mierezi!
 
Mwanakijiji,
Niliangalia film moja jinsi akina MAMA walivyowalazimisha WAPIGANAJI wa Liberia kukaa chini na kuongea. Wengine wakajifanya eti wamechukia na wanataka kuondoka. Wakawafungia mlango na kuanza KULIA. Wale jamaa kuona akina mama wako ngangari ikabidi warudi kwenye kikao na vita ikasimama.

Kufika uchaguzi, umoja wao ukaingia msituni na kumfagilia huyu mama aliye Rais sasa na walirudi nyumbani na kuzitundika NDUMBA ZAO (just T-sirt) na kusema ikibidi basi tutazivaa tena, na tukishavaa, basi hatuogopi kitu wala hatutishwi.

Nina imani wangelikuwa wanaume, basi wangeliitiwa FFU. Labda kuna haja ya Tanzania ije iokolewe na Wanawake maana sisi Wanaume tumechezea kazi.
 
Mkandara,
Si kwamba nakata tamaa. Ila naona tunakuwa WAVIVU kufikiri. Yaani na idadi kubwa namna hii, hadi leo bado tunaongozwa na watu kama 10 tu Tanzania na wametudhibiti hata hatuwezi kukohoa? Mie nina imani tunaweza kufanya mabadiliko na bila kumwaga damu. Mie yangu ni 'tuache kulialia na tuanze kutafuta njia za kujikomboa na Waarabu/Wahindi/Wacanada ambao wametuganda kama kupe.

Kwanza ni kutumia mbinu za CCM juu yao wenyewe:
-Devide and Rule.
-Kupakana matope.

Nina uhakika wana nyingine nyingi ila na sisi tukitumia hizi mbili tu, basi tutafika mbali. Kwenye ile makala ya Loliondo nimependekeza kwa CHADEMA kutengeneza film fupi, wanunue PROJECTOR moja kali sana inayoweza kuonyesha hata mchana na wawe wanapita kwenye vijiji, wanahutubia kidogo (bila kujifagilia) na kuwaambia wananchi kuwa mliambiwa mkichagua wapinzani tutavuruga amani? Haya angalieni wenzenu amani waliyo nayo. Na nyie hapa kwenu siku wakigundua madini/Mafuta (hapo mwaweza kuanza hata kuzusha kuwa wilaya fulani kuna utajiri fulani na wawekezaji kutoka nje wataletwa hapo na wanachi watakiona wanachokiona sasa Wamasai wa Loliondo) basi mtahamishwa kama wenzanu hawa kwenye film. Unamaliza na kuwaonyesha film kama ya nusu saa na mnaondoka kwenda kijiji kingine.

Haya Mkuu, nimeshatoa mapendekezo yangu.

Hebu CHADEMA mpitie na hii hapa: https://www.jamiiforums.com/jukwaa-la-siasa/43858-aibu-ya-tanzania-yaanikwa-uwani.html
 

Usikate tamaa. Kama bado una nia na malengo, ni wakati mwafaka kwako kutembelea HAPA
 

Hao Lowassa na papa fisadi ni wapambe wako maana wanakupamba kwa kila namna ili ukamuondoe mbaya wao kule Kyela.

Mimi sijakulink kabisa na hao mafisadi bali kilichokulink na hao mafisadi ni unachoandika hapa cha kuwatetea kwa nguvu zako zote bila kujali maslahi ya nchi yetu na kuthubutu kusema eti tufukie mashimo na kusonga mbele bila kutafutia ufumbuzi madudu chungu nzima ambayo yanaitafuna nchi yetu kila kukicha. Unayoyaandika yanaonyesha kabisa hufai kupewa wadhifa wowote ndani ya nchi yetu hata ujumbe wa nyumba 10 haukufai.

Katika kipindi hiki ambacho nchi yetu inapita katika wakati mgumu kuliko wowote ule hatuhitaji Wabunge wa kufukia mashimo ili tu tusonge mbele wakati huko mbele kuna kiza cha kutisha na nyuma pia kuna madudu ya kutisha. Hatuwahitaji kabisa ndani ya Bunge letu Wabunge wenye kutaka kufukia mashimo kama wewe utakavyo.
 
Usikate tamaa. Kama bado una nia na malengo, ni wakati mwafaka kwako kutembelea HAPA

Mami SteveD,
Huko tayari mie nipo. Nasubiri tu kuona MIIKO ya viongozi na malengo ya kuibadili katiba ya Tanzania/madaraka ya Rais. Yakikaa sawa na kama kweli chama kitakuwa na demokrasia ya kweli, basi MIE ni mwanachama.

Mie sitaki kabisa mambo ya kwenda kwenye NGO za watu au vyama vya watu. Kama si Mwinyi, Mkapa na sasa Kikwete kupokea hela za Waarabu, leo tusingelikuwa na kesi ya Dowans na Loliondo.
 
Hii labda kama tunataka kujenga Banana republic.

Mjadala mzuri sana huu....

FMES nakubaliana na wewe tujenge utawala wa sheria kwa gharama zozote

Na wewe Ze Comedy wa JF, Banana Republic si ni kule kwenu Mwanza ambako watu wanaua Albino wakifikiri watatajirika? Badala ya muda wote unaotumia hapa JF kukandia watu wenye mawazo ya kusaidia kwao, laiti ungetumia kusaidia kuelemisha kwenu ingelikuwa heri.

Lakini kama kawaida ya wababishaji wengine, unachojua ni kusagia wenzako huku wewe hufanyi lolote la maana zaidi ya kujaza tumbo lako kwa fadhila za Wazungu majuu.

Nashukuru wadau mbalimbali ambao wamenipongeza kwa kuamua kula sahani moja na mbabaishaji kama wewe. Pia nilikuwa nafikiri uko USA kumbe uko Ulaya na sasa data zote ninazo. Kilichobaki ni kupambana hapa hapa. Ukichafua wenzako na wewe tutakuchafua.

Kama wewe unafaa zaidi, kagombee huko kwenu uokoe hao ndugu zako na mawazo yao ya kizamani.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…